Naingiwa wasiwasi mno na uungwaji mkono kutoka upinzani, Usije kuwa ni lainisha upigaji kiurahisi

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,622
2,459
Nashindwa kuelewa huu uungaji mkono kutoka Kwa wapinzani kuunga juhudi za Chama tawala katika kulisuka Taifa letu na kuelekea Taifa lenye usawa na maendeleo ya kweli.

Nashindwa kuelewa kama kweli tuna upinzani uliodhamiria kuondoa Uonevu Kwa watumishi wa Umma ambapo wao kama upinzani walikuwa wanapigia kelele Jambo hili miaka mingi SASA!

Nashindwa kabisa kuelewa mwelekeo wa upinzani katika nchi hii, kushindwa kusimama Kwenye msimamo wao kwamba, CCM ndio sumu ya maendeleo na kwamba, kama Bado Taifa letu litakuwa likiongozwa na CCM, hatuwezi kufikia maendeleo ya kweli, na hivyo kupelekea CCM kuitwa ni kirusi katika Taifa letu.

Nashindwa kabisa kuelewa, kama kweli wapinzani huwa wanajielewa, na Je huwa wanatuona Sisi Watanzania ni mazezeta sanaaa au ni kiti gani!

Au shida ya upinzani ni CCM ispokuwa na viongozi wabovu na swala la upinzani ndio basi tena? Najiuliza sipati jibu.

Nashindwa kabisa kuuelewa upinzani wa nchi hii, na either, akili yangu Leo imenituma kufikiri, hawa watu ni masikini Sana na kinachokuwa kinawaliza Liza ni zile furusa za upigaji zinapokuwa zimebanwa kisawasawa ndio wanazidisha kelele!

CCM ni Chama moja matata Sana, ni Chama kinachokaa na Kusoma mazingira ya washindani wao yakoje Kwa Wakati huo, ni Chama ambacho kina viongozi wa kila aina, viongozi ambao wako CCM, wenye mlengo kama za kina Mwl JKN bado wako , wenye mlengo wa kina JK wapo kule, na wenye mwelekeo wa JPM Hayati wapo.

Katika kipindi cha uongozi kilichopita, CCM ilikuwa ikiongozwa na mtu asiyechekacheka na walilia maslahi na majambazi katika nchi hii, ingawa nimegundua pia kwamba, nchi hii wengi wa watu wamepinda tena sio kidogo, licha ya kuwa na kiongozi mkali lakini Bado majizi yaliiba tu.

Tukirudi katika ishu ya upinzani, Kwa namna upinzani ulivyogeuka na kuunga mkono juhudi Kwa haraka hivi bila hata ya kujiridhisha Kwa Yale wayatakayo yatafanyiwa kazi ama la, kumedhihirisha kabisa hawa jamaa ni wasaka tonge tu kama alivyokuwa mkurugenzi wa TPA, ni majambazi Tu na hayatakiwi kuchekewa chekewa tena. Ni upinzani wa hovyo Sana, Je wanajua kweli wanachokuwa wanakisimamia?

Hivi niwaulize swali, ni kitu kipi kinachowafanya wapinzani waunge mkono juhudi za Sasa Ndani ya CCM kama sio kujipendekeza ili maslahi Yao yasibanwe zaidi.

Naishia kusema, Wapinzani sio wa kuwapa nchi hata kidogo, tutapigwa haijawahi kutokea!
 
Hivi niwaulize swali, Ni kitu kipi kinachowafanya wapinzani waunge mkono juhudi za Sasa Ndani ya CCM kama sio kujipendekeza ili maslahi Yao yasibanwe zaidi

Wapi umesikia Wapinzani wanaunga mkono CCM. Shida yenu mnataka kumpotosha mama. Jana kasema asome kila jambo liwe wazi akimwambia CAG. Chawa lazima mfe maana hakuna mtu wa kumnyonya damu.
 
Hivi kibinaadamu, Magufuli kwa aliowafanyia wapinzani kuanzia 2015 mpaka uchaguzi wa 2020, unafikiri wapinzani wamehuzunika na kifo chake??? Mpinzani atakaesema amesikitishwa na kifo cha Magufuli ni mnafiki wa kiwango cha SGR.

Sambamba na waandishi wa habari (Ukiacha TBC na Cyprian Musiba pamoja na ndugu yetu msaka tonge aliekosa uteuzi Pascal Mayalla) walivyobanwa kufanya kazi zao kwa uwazi na ukweli, pamoja na wengine kupoteza maisha yao na kupigwa fine za ajabu walizokua wakipigwa pindi walipoonekana kutokuunga mkono juhudi, kuna mwandishi aliehuzunika kwa kifo cha Magufuli?

Ndugu Max Mello tokea 2015 mpaka 2021, ameburuzwa mara ngapi mahakamani??? Kwa makosa gani hasa yenye mashiko? Na nina amini "EXPOSURE YAKE pamoja na WAFUASI WAKE WA JAMIIFORUMS" ndio ilikua NGAO yake kuu, pengine nae wangempoteza au kumdhuru kama Azory Gwanda na wengine. Ila walijua hayo yangetokea basi dunia ingewaka moto na wafuasi wake JF wasingekaa kimya na wangefanya amsha amsha kwenye social media zote duniani.

Raia wa tanzania tunaasili ya unafiki na uongo.

Magufuli ukiachia mbali kuwakandamiza wapinzani na waandishi wa habari, pia aliwanyima raia "HAKI YAO YA KUCHAGUA VIONGOZI WANAOWATAKA", yeye ndio aliokua akiwaamulia raia nani apite wapi kwenye uchaguzi na nani asipite. Kulikua na haja gani ya kufanya Uchaguzi au kuwahubiria raia wachague kiongozi wanaeona anafaa???

"NOTE THAT" wapinzani sambamba na raia sio wanaunga mkono juhudi za CCM sasa hivi ili kujipendekeza au kwa lolote, ila wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu kwasababu wana Imani nae kwamba atawafuta machozi ya 2015 - 2021.
 
Hao chadema ni kundi la yule bwana yupo ccm hivo wao hutumika kuharibu au kubomoa mradi tu walinde maslahi ya bwana yule wa CCM
 
Dikiteta magufuli alichoifanyia upinzani kwa kweli hatuwezi kusahau haraka kihivyo, so kutokuwepo kwenye hicho kiti huyo chatu wa chatto ni ahueni kwetu vyama mbadala na taifa kwa ujumla.
Kwa hiyo sasa CCM imetubu?
 
Hivi niwaulize swali, Ni kitu kipi kinachowafanya wapinzani waunge mkono juhudi za Sasa Ndani ya CCM kama sio kujipendekeza ili maslahi Yao yasibanwe zaidi

Wapi umesikia Wapinzani wanaunga mkono CCM. Shida yenu mnataka kumpotosha mama. Jana kasema asome kila jambo liwe wazi akimwambia CAG. Chawa lazima mfe maana hakuna mtu wa kumnyonya damu.
Akili ginyu Sana hii, haya niambie ni mpinzani gani ameingia mkono juhudi ?

Hivi kusifia pale panapofaa ni kosa? Mnamwonea wivu mama Kuwa anapata kuungwa mkono si Ndio.

Maovu ya meko yatakuwa wazi, mnafiki yule alikuwa akitumia mazumbukuku Kama Nini kumaliza nchi. Pale mama anapopatia lazima tumor heko, pale anapochemsha lazima pia tumkumbushe.

Kazi ya upinzani ni kutoa hoja mbadala, pe mambo yanapokwenda sawa tunasifia. Ndio maana kipindi Cha kikwete ilikuwa huwezi kuona watu wanazungumzia kero za ajira. Lakini enzi za meko Ndio ilikuwa wimbo. Sasa kama unaona wivu kusifia mazuri wewe ni mchawi.
 
Back
Top Bottom