Mkuu. Nilishaweka uzi hapa unaoitwa"cable za kibalozi". Umetokea wikileaks na unazungumzia misaada Nyerere anaomba Marekani. Waziri wake Malecela ndio aliyekuwa mpiga debe wake wa kuomba misaada. Hiyo ilikuwa mwaka 1974-76.
Sio tu habari za mawasiliano ya kibalozi yanaonyesha Nyerere anaomba msaada wa chakula bali pia msaada wa kujengewa barabara, zahanati na hata majenereta ya umeme na mafriji. Na Malecela aliomba sana waje wenyewe waone jinsi Tanzania inavyohitaji misaada. Na maofisa wa Marekani wakaja na kutoa misaada mingi tu.
Pia, muhimu zaidi, viongozi wa ulaya wakija Tanzania, hasa kutoka Skandinavia na Uholanzi, Nyerere sio tu anaomba msaada ili ailishe wananchi wenye njaa kali vijijini bali pia anawaombea msaada viongozi wa Msumbiji, Angola na nchi nyingine zilizokuwa zinagombania uhuru wao kwa wakoloni ili waweze kujikomboa na kulisha jumuia yao nje ya nchi zao.
Yote tulikuwa hatujui, tunalishwa propaganda na RTD.
Ila Nyerere apologists husema kuwa hali mbaya ya uchumi ilitokana na vita vya kagera. It's BS.
Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app