Warioba, hawezi kuweka mikono kwenye kunde na nyama kwa pamoja, huku anaandika ripoti ya rushwa, na huku anashirikiana na Mahalu, ameandika ripoti ya wizara zote lakini Elimu na Sayansi, kwa Mkapa, na Mahalu hakwenda, mgombea wake Salim kushindwa Dodoma makelele mengi kuwa viongozi wa CCM wamejaa rushwa hawamjali Mwalimu, leo Warioba kabadilika tena kuna wenzetu humu wanasema anafaaa kuwa rais, ubunge Bunda wamemkataa, hata Mwalimu mwenyewe mentor wake hakumpa urais,
Hivi waandishi wetu huwa hawaweki kumbu kumbu? Kwa nini wasimuonyeshe Warioba, maneno yake mwenyewe baada ya uchaguzi wa rais CCM Dodoma, kwenye TV ili aeleze kuwa kwa nini hayalingani na ya sasa? Kulikoni hasa?
Lowassa, hakufukuzwa na ripoti ya Mwakyembe, ameikimbia ripoti mwenyewe kitu ambacho kinaonyesha incompetence yake na kwamba haikuwa right yeye kuwa Waziri Mkuu in the first place anyways, maana kama leo anakimbia ripoti tu kesho tutamwamini vipi adui wa kweli akitushambulia? Analia lia nini badala ya kukubali yaishe na kuanza upya? Ameonewa na nani hasa wakati serikali tumeambiwa ilikuwa ni yake na washikaji wake watupu, sasa aliyemuonea ni nani hasa? Yeye kwenye uchaguzi wa rais amechafua majina ya wenziwe weee mbona hawakulia? Sasa leo amejichafua mwenyewe na matendo yake halafu anlilia wengine? Hivi bongo ni lini tutajifunza kubeba respondibility zetu wenyewe na kuacha kulaumu kila mtu mwingine badala ya kujiangalia kwenye kiooo na kukubali vivuli vyetu?
Hebu mlio karibu naye mwambieni kuwa kujiuzulu kwake, kilikuwa ni kitendo kizito na chenye heshima kwa watoto wetu wa taifa la baadaye, kuwa kujiuzulu nafasi kubwa kitaifa, sio death sentence, sasa kabla hatujampa full heshima analia lia tu na nwengine wanamlilia tuuuu, aka jamani huko kwenye power kuna nini hasa?