Naiiona CCM ikifa kifo cha mende mwaka 2025

Echisute

JF-Expert Member
Oct 16, 2018
267
250
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona siyo mbaya tukatafakari kwa pamoja kwa sababu nchi ni yetu wote bila kujali itikadi za vyama!

Rejea kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi mwaka 2015, CCM iliwakilishwa na watia nia takribani 20 huku mwenyekiti wa wakati huo Ndg. J. Kikwete akiwa na jina lake mfukoni na wana CCM wenyewe kwa maana ya walio wengi wakiwa na mtu wao hadi kupelekea mvutano mkubwa sana uliosababisha mmoja wapo wa watia nia kuokota embe dodo chini ya mti wa mwarobaini.

Ni ukweli usiopingika kuwa Ndg. J. M Kikwete akiwa ndiyo mwenyekiti wa kipindi hicho alipambana sana kwa kutumia uzoefu wake katika siasa kukinusuru chama kisimfie ndani ya uenyekiti wake kwa sababu ulitokea mpasuko wenye nyufa kubwa sana ndani ya CCM hadi waliokuwa viongozi waandamizi ndani ya chama kutimka na kuunga juhudi mkono za vyama vya upinzani wakati huo kwa pamoja vikijulikana kwa jina la “ UKAWA”.

Kwa mara ya kwanza katika siasa za vyama vingi CCM ilipata wakati mgumu sana hadi ushindi wa aliyeokota embe dodo chini ya mwarobani bado watanzania wanaojitambua wanajua ni ushindi uliopatikana kwa hila, nguvu, na vitisho vya dola ukijulikana zaidi kama “ GOLI LA MKONO”.

Swali: Je, huyu mwenyekiti wa sasa itakapofika 2025 ataweza kuikabidhi CCM kwa wana-CCM wenyewe?

Karibu kwa maoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Craig

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
774
1,000
""Ndg. J. Kikwete akiwa na jina lake mfukoni na wana ccm wenyewe kwa maana ya walio wengi wakiwa na mtu wao hadi kupelekea mvutano mkubwa sana uliosababisha mmoja wapo wa watia nia kuokota embe dodo chini ya mti wa mwarobaini"😄😄😄😄😄😄😄 NIMECHEKA SANA JF KWELI RAHA. WANOGESHAJI HAWAISHI.
 

MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
411
500
Mapenzi ya Mungu yalitimia (siku ile ya uchaguzi wa Member Vs Lowassa) kuliokoa Taifa Tena kwa funzo la kujenga nchi upya kwa kuuma Sana, na kwa nionavyo mpaka miaka 10 ya awamu ya tano ipite kila Mtanzania aliyekuwa na miaka 18 ile 2015 atastahili cheti Cha Kuisoma Namba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,808
2,000
mpka sasa nikiangalia pande zote za vyama vya siasa wote ni akina njaa kali labda watokee wanasiasa wapya sio hawa akina njaa kali wanawaza matumbo yao
 

Masanjaone

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
855
1,000
Nataka nianzishe chama cha siasa ila mashart yake ili uwe mwanachama nikuanxia wasiojua kusoma wala kuandika na upanfe wa elimu mwisho ni form4.

Maana nimegunfua wasomi wanawatumia wasio na elimu kuandamana na kupigwa mabom ilihari wao wakila viyoyozi na wake zao.
Nitatafta saini kwa wenye elim ndogo tu.
Sera za chama nimeanza kuziandaa sasa hivi.
 

Echisute

JF-Expert Member
Oct 16, 2018
267
250
Kifupi nikwamba cjaona chama cha kuiondoa ccm madarakani mpaka sasa.

Ova.
Fikirisha ubongo wako kijana, nani kasema wapinzani wataiondoa ccm madarakani? Ccm itaondoka madarakani kwa nguvu ya wananchi, tume huru ya uchaguzi na zaidi ya yote ccm hao hao ndiyo watafanikisha mchakato mzima.

# Time will tell.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
1,277
2,000
hivi bado mnaamini yule jamaa aliyetoka ccm akainunua chadema na sasa karudi ccm alishinda?
 
Top Bottom