Echisute
JF-Expert Member
- Oct 16, 2018
- 496
- 476
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimeona siyo mbaya tukatafakari kwa pamoja kwa sababu nchi ni yetu wote bila kujali itikadi za vyama!
Rejea kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa kiti cha uraisi mwaka 2015, CCM iliwakilishwa na watia nia takribani 20 huku mwenyekiti wa wakati huo Ndg. J. Kikwete akiwa na jina lake mfukoni na wana CCM wenyewe kwa maana ya walio wengi wakiwa na mtu wao hadi kupelekea mvutano mkubwa sana uliosababisha mmoja wapo wa watia nia kuokota embe dodo chini ya mti wa mwarobaini.
Ni ukweli usiopingika kuwa Ndg. J. M Kikwete akiwa ndiyo mwenyekiti wa kipindi hicho alipambana sana kwa kutumia uzoefu wake katika siasa kukinusuru chama kisimfie ndani ya uenyekiti wake kwa sababu ulitokea mpasuko wenye nyufa kubwa sana ndani ya CCM hadi waliokuwa viongozi waandamizi ndani ya chama kutimka na kuunga juhudi mkono za vyama vya upinzani wakati huo kwa pamoja vikijulikana kwa jina la “ UKAWA”.
Kwa mara ya kwanza katika siasa za vyama vingi CCM ilipata wakati mgumu sana hadi ushindi wa aliyeokota embe dodo chini ya mwarobani bado watanzania wanaojitambua wanajua ni ushindi uliopatikana kwa hila, nguvu, na vitisho vya dola ukijulikana zaidi kama “ GOLI LA MKONO”.
Swali: Je, huyu mwenyekiti wa sasa itakapofika 2025 ataweza kuikabidhi CCM kwa wana-CCM wenyewe?
Karibu kwa maoni!
Sent using Jamii Forums mobile app