Ushirombo
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 3,558
- 2,714
Monocotyledon
Spika yako ni Mono?
Spika yako ni Mono?
watu mnajua wasilisha mada kwa mafumbo...ptuuuu
Spika za kizamani ndivyo zilivyo,sema itakugharimu kubadilisha frem,cover lake na hata sumaku pia..hadi nyaya
kiufupi bora ufunge spika mpya
Hahaaa Sina utaalam wa vina na mizani. Mimi nimeropoka tu vinavonikera kwa spika yangu chifu.Bado tuna washairi bora kiasi hiki
Hili ni shairi bora Kabisa
Tafadhali mhusika weka beti , mezani na vina
Hakika ukishindanishwa huna mpinzani
Tatizo redio uliyonayo inaamini yenyewe tu ndio ina uwezo wa kudaka mawimbi hata yale ya masafa marefu kisa ni old versionBasi itabidi nifumue mtambo wa kurushia matangazo nijue tatizo ni Nini.
Mimi ni fundi ila ningependa kufahamu kabla sijakusaidia kutengeneza, Je spika yako brand gani? SAMSUNG, SONY, NDUGULAI, ABODA, au LG????
Hahaaa Sina utaalam wa vina na mizani. Mimi nimeropoka tu vinavonikera kwa spika yangu chifu.
Hahahahahahah!!!!!! Nyie watu siwawezi.Tena juzi imenasa mawimbi ya bagamoyo radio station badala ya yale yalizoeleka kutoka "soko la samaki"
Umeniquote vibaya hiyo brand sio NDUGALAI ni NDUGULAI😂😂😂😀😀😀
Ndugalai ndo nini
Itupe jalalani mlongo... Watoto wa kuchezea watachezeaWadau. Hii spika wakati nainunua nilijua kabisa ni mbovu ila nikajipa moyo huenda itatengenezeka. Lakini wapi.
Chaajabu imezidi kuwa ya hovyo hovyo kadiri muda unavyoenda. Kila mara naitibia maradhi yake inapona kidogo halafu inaanza tena kusumbua. Imefikia hatua mpaka naficha gharama za kuitibu maana mtahisi labda nawafanyieni ufisadi. Gharama ni kubwa mno unafikiri nanunua music system nzima kumbe NI utengenezaji tu wa spika moja mbovu.
Hii spika bhana nimeshindwa kuielewa. Imeanza kuingilia hadi kazi ya calculator - kile kikokotoa hesabu. Yaani imekuwa ya hovyo Sana.
Kwakweli Mimi binafsi naona hainifai Tena. Kuna wakati kijispika kidogo Cha pembeni kilipigwa short za moto zaidi ya Mara 20, cha ajabu hii spika yangu kubwa badala ya kuendelea kuimba vizuri ili itoe sapoti kwaile ya pembeni ndio kwanza ikaanza kukoroma na kuzima kabisa.
Yaani hapa nimechukia Sana. Ilivyo ya ajabu Mimi nikitaka ipige mziki huu yenyewe inacheza mziki mwingine tofauti kabsaa. Jana nimekasirika Sana ilipoanza kucheza mziki wa Afrika kusini Tena kukandamiza kajispika ambako NI kabrand moja na yeye. Vitu vya ajabu Sana.
Jamani nisiwachoshe. Naigawa bure. Kwa Sasa Sina KAZI nayo kabisa. Spika haijielewi. Inanitia gharama za bure tuu. Mwenye kuihitaji hii nimeiweka njiani tuu hapo makao mapya
Wasaalaam