Naichukia Polisi, Sababu ni Hii hapa

buluwaya

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
207
45
polisi ya tanzania naichukia kuliko hat kinysi. na sababu kubwa niliyo nayo ni hii hapa

[h=1]Unyama, ubabe wa polisi[/h]
01/02/2014 | Posted by Abdallah Khamis | Kitaifa | 0 comments | 210 views

ASKARI polisi Kituo cha Msimbazi, Wilaya ya Kipolisi Kariakoo jijini Dar es Salaam, wameingia katika tuhuma za kumkamata, kumpiga na kisha kumvunja mikono yote Kulwa Kitange (40), mkazi wa Kigamboni, baada ya kijana huyo kukataa kuelewana nao nje ya taratibu za kisheria.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 26, mwaka huu baada ya askari hao waliokuwa doria kumkamata Kitange katika eneo la Jangwni majira ya saa 1:30 usiku, wakimtuhumu kuwa ni jambazi.
Akizungumza na gazeti hili juzi baada ya kupata dhamana, Kitange aliyetuhumiwa kuwa ni jambazi kabla ya kuvunjwa mikono akiwa ndani ya kituo cha polisi, alisema siku hiyo alitoka nyumbani kwake Kigamboni kwenda kupata kinywaji katika eneo la Polisi Barracks Kurasini.
Anaeleza kuwa akiwa katika eneo hilo la Kurasini, alimpigia simu rafiki yake wa kike na kumuuliza mahali alipo ambapo alimuelekeza kuwa yupo eneo la Jangwani na kama anaweza amfuate.
Aliongeza kuwa baada ya mawasiliano hayo na rafiki yake huyo, alimtafuta dereva wa bodaboda ili amfikishe Jangwani.
“Yule mpenzi wangu kwao sipajui, nilipofika Jangwani nikampigia simu, akaniambia nimsubiri anajiandaa. Mahala tulipokuwa tunamsubiria kuna ‘grocery’ na tulikuta pikipiki moja imeegesha, ghafla wakaja polisi wakatuambia tunyooshe mikono juu, tukafanya hivyo,” alisema Kitange.
Alieleza kuwa baada ya kunyoosha mikono juu askari waliokuwa na silaha walianza kuwapekua mifukoni na yeye kukutwa na sh 4,500 pamoja na simu.
Alisema kuwa baada ya kupekuliwa yeye na dereva wa bodaboda walifungwa pingu na kisha kutakiwa kupanda katika gari la polisi kwenda Kituo cha Polisi Msimbazi.
“Walitaka kupakia na pikipiki zote mbili, sisi yetu tukawapa funguo wakapakia, cha kushangaza tulipoenda mbele kidogo wakasimamisha gari na kutuambia tuelewane ili watuachie. Kwa kuwa nilikuwa nimeshalewa nikawaambia mtaelewanaje na majambazi badala ya kuwafikisha katika vyombo vya sheria, nadhani hilo ndilo lililowaudhi,” aliongeza Kitange.
Akiwa katika maumivu makali ya majeraha, Kitange alisema walipofika Msimbazi Polisi waliingizwa katika moja ya vyumba na kuanza kupigwa virungu kwa muda wote wa usiku hadi kuvunjika mikono yote miwili, na wakati wakipigwa virungu hivyo walikuwa bado wamefungwa pingu mikononi.
Aliongeza kuwa siku iliyofuata alimuomba mmoja wa askari amsaidie kuwapa taarifa ndugu zake ambao walifika na kuanza taratibu za kumuwekea dhamana aliyoipata juzi.
Hata hivyo, Kitange anasema baada ya kupata dhamana aliomba fomu ya polisi (PF3) kwa ajili ya kwenda kutibiwa hospitali na kwamba siku ya kwanza alinyimwa, na mmoja wa askari akamueleza kuwa akajitibu kienyeji.
“Alisema akiwa nyumbani alitumia maji ya moto kujichua na hali ilipozidi kuwa mbaya akampigia simu mpelelezi wa tuhuma zake na kumuomba ampatie fomu ya polisi kwa ajili ya matibabu.
“Siku ya Jumatano nilipofika Msimbazi wakaniambia tuende Mnazi Mmoja na nilipofika pale yule askari aliyenipeleka alitaka nimwambie daktari kuwa nimeanguka, lakini nikamkatalia na kumueleza kuwa nimepigwa na askari,” alisema Kitange.
Aliongeza kuwa baada ya maelezo hayo daktari alimpima na kuwashauri waende katika hospitali ya Amana kwa huduma zaidi ambapo alipata huduma za awali na kutakiwa kurudi baada ya wiki moja kwa ajili ya kufungwa plasta ngumu (P.O.P).
Kutokana na hali hiyo Kitange alisema alijaribu kuonana na maofisa wa polisi ili aeleze unyama aliofanyiwa na polisi, lakini alishindwa baada ya baadhi ya askari kumkwamisha.
Hata hivyo, gazeti hili lilifanikiwa kumkutanisha Kitange na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, ambaye aliahidi kulishughulikia suala hilo kwa ufasaha.
Minangi alisema polisi ni tegemeo pekee la wananchi katika suala la usalama, na kwamba kama kuna askari aliyehusika na mateso hayo, lazima atawajibishwa.
“Tumepokea ila kwa sasa sitoweza kukupa jibu la moja kwa moja, ila tunafanya uchunguzi na watakaobainika katika kutenda unyama huu, watawajibishwa.
Tanzania Daima tunaahidi kulifuatilia suala hili kwa karibu kujua hatma ya polisi waliohusika kufanya unyama huu kwa kijana huyo.


CHANZO CHA TAARIFA: Tanzania Daima
 
Polisi kwa kulindanda ndo wenyewe,hao polisi hawatapatikana!,pole yake mr kitange.
 
kweli pombe ni mbaya kwanini akuelewana nao tu yakaisha!!!!?

kuelewana na hawa m.b.wa ni ku-renforce upumbavu wanaofanya. dawa ni kuanza kukomaa nao kila mtu kwa namna yake, hata kama ni kwa gharama analipa huyu bwana kwenye hii stori ya tanzania daima. mi kwakweli kungekuwa na shimo la jehenamu watu wanatupiwa ningekuwa wa kwanza kuwasukuma polisi wa tanzania waende huko. siwapendi kama nini
 
Polisi wa Tanzania si usalama wa raia kabisa ila ni maadui wa wananchi live. Polisi ni polisi tu kuanzia wa ngazi ya chini hadi wa ngazi ya juu lao moja. Huyo RPC aliyeahidi kufuatilia swala hilo subirini muone kama atawawajibisha polisi wenzake!!! Hakuna chochote kitakachofanyika. Sijui jeshi la polisi litakuwa usalama wa raia mwaka gani.
 
Hii inasikitisha na kuondoa amani unapomuona polisi akija mbele yako.
 
Usalama wetu hadi ccm iondoke madarakani,mmesahau kuwa police ni ccm dogs!

na kwa tabia hii ni dogs kweli. dogs kabisa. kuna siku nimepanda bodaboda dereva akawa anaeendesha vibaya nikaamua niendeshe mwenyewe nilikuwa na haraka na pahala penyewe hakuna bodaboba mbadala. yule dereva kakubali. kufika mbele tumemkua huyo dog mmoja kasimamisha pikipiki. tumefuata masharti yote tukasimama. anataka leseni. nimemwonyesha leseni ya gari ndogo. anataka ya pikipiki. kakomaa wewe anataka elf 20. leseni ya pikipiki mie leseni ya pikipiki. mi nikamuuliza umeona nimeanguka nayo. mb.wa kabisa hawa binadamu, sasa nikawa nachelewa miadi. nimeacha pikipiki hadi kwenye atm kwa mguu nikarudi na elf 20 ndo kuondoka pale. eti sasa sikuwa na tatizo; tumetoka naendesha mwenyewe. kwa kweli mimi polisi wa tanzania nawachukia sana.
 
Back
Top Bottom