Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo adanganya tena

Wadau,

Nimemsikiliza naibu waziri wa elimu katika kipindi cha ITV cha DK. 45. Katika kuipa sifa zisizostahili serikali ya CCM amejikuta akiudanganya umma wa watanzania kuwa kabla ya kuanzishwa shule za sekondari za kata mwaka 2006 (za akina lowassa) mkoa wa Mbeya ulikuwa na shule tatu (yaani Rungwe, Loleza na Iyunga).

Ukweli:

Shule zilizokuwepo ni Rungwe, Loleza, Iyunga, Mbeya Day, Vwawa Day, Mwakaleli, Ileje Day,Chunya Day, Kyela Day.....
mdau mwingine aweza kuongeza ama kurekebisha orodha.

Kama naibu waziri wa elimu hajui takwimu za shule, anafanya nini hapo wizarani?

Naomba kuwasilisha kwa ajili ya kujadili.

Wakati huo nadhani ye alikua jimboni Zimbabwe, kwa hilo si mlaumu
 
Huyu bwana mbwembwe nyiingi lakini hana lolote. Jina analotumia sasa si lile aliloandikishwa sekondari
 
kati ya sera mbovu hapa tz ni sera za elimu,leo hiki,jioni hiki na kesho kile,yaani hamna consistency wala dira
 
huyo ndo naibu waziri wa elimu kaaaazi kwelikweli. full miyeyusho. Elimu itapanda kweli ngoja tuone
 
Inawezekana alimaanisha mbeya mjini?
Mkuu kama alizungumzia za Mbeya mjini sasa Rungwe alikujaje tena! Mimi nafikili alikuwa anazungumzia shule za Sekondari za Serikali, angesisitiza hilo kuepushwa maswali mengi hapo baadae - wenzetu usema once bitten twice SHY!! SIJUHI MWENZETU KAMA HILO ANALITILIA MAANANI!!!! Bila ya ku-rectify tatizo hilo atakuwa anapata wakati mgumu kutoka kwenye vyombo vya habari, anapaswa kuwa anafanya homework kabla ya kusema kitu kwenye kadamunasi - mimi ndio ushauri wangu wa bure KWAKE.
 
Hahahahahahaah! mambo ya Amiri! hayo ful kudanganya haya wadau wangu endeleeni kufunuka hapo ilikuwa bado Kinyala, Irambo shule ya presda wa Kongo na Sangu pia Manow seminary! bila kusahau Lutengano ya Prof Jay.... naomba kuwasilisha!:confused2:
 
Wadau,

Nimemsikiliza naibu waziri wa elimu katika kipindi cha ITV cha DK. 45. Katika kuipa sifa zisizostahili serikali ya CCM amejikuta akiudanganya umma wa watanzania kuwa kabla ya kuanzishwa shule za sekondari za kata mwaka 2006 (za akina lowassa) mkoa wa Mbeya ulikuwa na shule tatu (yaani Rungwe, Loleza na Iyunga).

Ukweli:

Shule zilizokuwepo ni Rungwe, Loleza, Iyunga, Mbeya Day, Vwawa Day, Mwakaleli, Ileje Day,Chunya Day, Kyela Day.....
mdau mwingine aweza kuongeza ama kurekebisha orodha.

Kama naibu waziri wa elimu hajui takwimu za shule, anafanya nini hapo wizarani?

Naomba kuwasilisha kwa ajili ya kujadili.
Hivi kwanini amekomaa na siasa za Mbeya huyu mbumbumbu?
Haya ongeza hizi: Tukuyu Day, U/usongwe 1997, Mbeya day, Ipinda sec school nk
 
Back
Top Bottom