Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo adanganya tena

OLEWAO

Member
Jan 27, 2012
89
78
Wadau,

Nimemsikiliza naibu waziri wa elimu katika kipindi cha ITV cha DK. 45. Katika kuipa sifa zisizostahili serikali ya CCM amejikuta akiudanganya umma wa watanzania kuwa kabla ya kuanzishwa shule za sekondari za kata mwaka 2006 (za akina lowassa) mkoa wa Mbeya ulikuwa na shule tatu (yaani Rungwe, Loleza na Iyunga).

Ukweli:

Shule zilizokuwepo ni Rungwe, Loleza, Iyunga, Mbeya Day, Vwawa Day, Mwakaleli, Ileje Day,Chunya Day, Kyela Day.....
mdau mwingine aweza kuongeza ama kurekebisha orodha.

Kama naibu waziri wa elimu hajui takwimu za shule, anafanya nini hapo wizarani?

Naomba kuwasilisha kwa ajili ya kujadili.
 
changanya

Member
Oct 17, 2012
32
4
Huyu jamaa ni mwongo sana anasema kuwa sifa za kidato cha sita ni kitu kipya wakati wizara ilitoa waraka mwaka 2010 na ndiyo uliotumika mwaka 2011 kuchagua wanafunzi waliochaguliwa kidato cha 5 waliangalia sifa hizo sasa inashangaza leo hii wizara inakana kuwa haina habari wakati kuna wanafunzi wengi walioachwa kwa sababu hawakuwa na D 2 licha ya kuwa walikuwa na C 3. Shule za A level hazikupata wanafunzi wa kutosha kutokana na kukazwa kwa mashari ya kujiunga. Hivi JK haoni kuwa hao mawaziri wake hawamsaidii kitu. Wanataka hali iweje ndiyo aone anahitaji kuchukua hatua? Ama kweli Tanzania kila kitu kinawezekana kanuni za mchezo zinabadilika katika kipindi Penalti
 
Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,120

Tatizo ni kwamba Tanzania tunawapa viongozi wetu uwezo wa kutufanya mazezeta. Waziri kama huyu anasema uongo na hakuna lolote atakalofanywa. Vyombo vyetu vya habari vinafanya kazi kwa urafiki bila kuzingatia ukweli. Hatuna waandishi wa habari wanaoweza kumuhoji mtu na kumlazimisha kuzihuzulu. Ndo nchi yetu tutafanya nini!
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,441
51,157
Elimu ni muhimu sana ndio matatizo ya kuwapa vyeo watu wasio na sifa nadhani JK kajifunza kutoka kwa huyo kilaza.....
 
Chebe

Senior Member
Sep 27, 2011
198
30
nakusikitia sijui kwa nini ulipoteza muda wako kumsikiliza huyu kilaza afadhali ungeangalia isindigo the need
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Labda ndugu Mulugo alikuwa anaongelea shule za Zimbabwe kabla haijaungana na Visiwa vya Pemba in 1-1964!

hivi alito excuse gani kuhusiana na issue ya Tanzania ni muungano wa visiwa vya zimbabwe na Tanganyika ???
 
Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
258
Huyo Kilaza alikuwa anazungumzia Malawi siyo Mbeya! Mjinga mwenye akili ndogo anaongoza akili kubwa. Mimi nahisi huyu alienda kucheza kiduku Ikulu, JK akamuona anavyochnaganya miguu, Riz1 kasema Mshua huyu anafaa uwaziri wa elimu ya Ngoma
 
blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
422
Nadhani kwake yeye hajisikii kudanganya, kwa sababu yeye ni mbumbumbu, hajui!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

7 Reactions
Reply
Top Bottom