Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali y teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kufunga chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) baada ya kubaini matatizo mbalimbali baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo.
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama la!.
Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ilikuondoa matatizo amelazimika kuifunga kwa muda huo wa siku tatu ilikufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.
Awali vyombo vya habari vilitoa taarifa mbalimbali juu ya Mochwari hiyo ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuatarisha afya za wananchi.
Mochwari ya Tumbi Kibaha na vipaumbele hovyo
Mimi ni mdau katika hii sekta nimefanya kazi mochwari napafahamu vema palivyo , ni sawa na kukaa kuzimu kwakuwa muda wote uko na wafu wa kila aina.
Hospital ya Tumbi inajulikana kwa kupokea majeruhi na maiti nyingi za ajali zinazotokea kila siku kwenye barabara ya Morogoro lakini vitengo vya dharura upasuaji na mochwari viko hoi.
Utawala wa miaka 10 wa JK haukuliona hili? Wale waliomjengea lami pale Msoga kwenye barabara zote mbili za kufika kwake hakushauriana nao kuhusu hali ya Tumbi?
Kampeni zilizotumia mabilioni ya kuwanunua wapinzani Kuwalipa wasanii na kufanikisha wizi wa kura hawakuifikiria Tumbi?
Yale Mavx V8 wanayoenda nayo pale kwa shughuli mbalimbali hawaoni aibu?
Leo Kigwangala anaenda pale ameziba pua na kuamuru mochwari ifungwe, amewakumbuka waliokuwa wanashinda pale kutwa kucha?
Maiti za kuanzia leo mpaka itakapofunguliwa zitahifadhiwa wapi?
Jitofautisheni na awamu iliyopita lifanyike jambo la dharura kutengeneza yale majokofu huku mkijipanga kujenga mochwari kubwa na ya kisasa.
Acheni kuuza sura kwenye visimbuzi.
Kama mnadhani mochwari ni gesti house kalaleni pale siku moja ndio mtawajua wazalendo wakweli wa nchi hii ni akina nani.