Naibu Waziri Tamisemi amsimamisha kazi Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo amemsimamisha kazi kwa muda Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela jijini Mwanza John Wanga.

Hatua ya Jaffo imekuja ili kupisha uchunguzi wa uhalali wa fedha zilizotumika kujenga uzio wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Amesema nafasi yake itashikiliwa kwa muda na Injinia Jacob Nathaniel hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika.
 
Last edited by a moderator:
John Wanga rudi tu kwenye kupiga ishu za sheria. Mara mwanasheria Ilala, mara mkurugenzi! We pale ofisin kwako ulikua unapiga mishe zako bila bughudha, sasa ona mastress na kudhalilika! Pole sana blaza karibu kijiweni kama vipi
 
Huyu jamaa mpigaji sana namjua tokea alivyokuwa mwanasheria wa jiji Mwanza na mshakji wake Wilson Kabwe
 
ndiyo maana hadi Leo hajajiongeza kujenga barabara ya kiseke hadi Busweru na ile ya National-Busweru kwa sababu akili yake yote ni kuwaza ufisadi na kupiga dili...yaan mvua zimenyesha hadi sasa zimeisha lakini hajajiongeza kuleta greda ya kutengenezea Barabara...!!

kuhusu ule uzio...mkuu wa mkoa anahusika hapa, yy ndiye aliyesema uzio ujengwe ili kujiandaa na uchaguzi mkuu, kwamba wananchi hasa vijana wakose access ya kuingia ndani kushinikiza matokeo ya ubunge yatangazwe....

Magesa mlongo ni kichwa maji sana.
 
kila siku kabla ya chochote huwa naomba kwa Mungu mtumbua majipu asinifikie huku niliko, jamani hela tamu, ukiwa mpigaji huwezi kuacha.
 
Last edited:
Uzio umegharimu takribani sh. 300,000,000/= source Star TV

For rough estimates...
Sqm 1 ni kama 30,000/=

Sasa hapo manake kulitakiwa kuwepo na sqm. Kama 1000 hivi .....

Lol...hiyo hela ni nyingi mno.. Wacha ile kwake
 
Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo amemsimamisha kazi kwa muda Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela jijini Mwanza John Wanga.
Hatua ya Jaffo imekuja ili kupisha uchunguzi wa uhalali wa fedha zilizotumika kujenga uzio wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amesema nafasi yake itashikiliwa kwa muda na Injinia Jacob Nathaniel hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika.
Nisaidieni msinicheke wala kunitukana, kwani Mkurugenzi ndo huyo huyo injinia? Hivi sio kwamba project kama hiyo inapitishwa na madiwani na inakuiwa chini ya mtaalamu ambaye ni injinia? Sasa hapa mkurugenzi anahusika vipi au ndo kuwajibika kwa sababu ya watu wa chini yako?
 
For rough estimates...
Sqm 1 ni kama 30,000/=

Sasa hapo manake kulitakiwa kuwepo na sqm. Kama 1000 hivi .....

Lol...hiyo hela ni nyingi mno.. Wacha ile kwake
Sasa kama walitaka aweke uzio.ili awasaidie ccm kushinda uchaguzi walitegemea nini? Wamwache bwana si aliona ndo fursa ya kupiga hela?
 
Naibu Waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo amemsimamisha kazi kwa muda Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela jijini Mwanza John Wanga.
Hatua ya Jaffo imekuja ili kupisha uchunguzi wa uhalali wa fedha zilizotumika kujenga uzio wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amesema nafasi yake itashikiliwa kwa muda na Injinia Jacob Nathaniel hadi uchunguzi wa tuhuma hizo utakapokamilika.
Mbona kawaacha wale wa manispaa ya Nyamagana ambao walipiga dili la mabilioni kwenye kiliniki ya Makongoro.
 
Kama kuna watumishi wapiga dili kwenye pesa za uma ni wa jiji la mwamza nakupongeza mh.Jafo usiondoke mwanza ingia na nyamagana,jiji pamoja misungwi Utalia.
 
Pole Wanga ila wakati mwingine ni kudhalilishana ule uzio mimi kwa tathimini yangu ni zaidi ya milioni 300.Uzio huo umetusaidia sana kuwazuia CDM wasilazimishe matokeo ni imara kuliko wa JIJI.Hata hivyo yalikuwa maagizo toka juu uzio huo ujengwe kabla ya uchanguzi,INYESHE ISINYESHE UZIO UKAMILKE KABLA YA OKTOBA 2015.Ni amri toka JUU hapo hapo gharama haikuwa issue sana.Any way Wanga usifikili hapa ni MEATU macho na majungu mengi sana nilijua hapa utanasa.Wakimaliza huo ukuta mje na DISPENSARY YA KATA YA KITANGIRI NI AIBU SANA.Mkamateni meya na naibu wake waliopita.
 
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman Jaffo, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauli ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga kutokana matumizi mabaya ya madaraka.

Waziri Jaffo amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa ufujaji wa fedha za ujenzi wa uzio wa halmashauli hiyo uliogharimu Sh. 347 milioni pamoja na kukaidi kuhamia kwenye nyumba ya Serikali ya Sh. 200 milioni.

Naibu huyo wa Tamisemi alitoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi wa manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ambako amesema mkurugenzi huyo ameshindwa kuhamia katika nyumba hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu Sh. 200 milioni na kusababisha Serikali kuendelea kulipia nyumba anayoishi.

Amesema kuwa licha ya Serikali kutoa agizo kwa mkurugenzi huyo kuhamia katika nyumba hiyo lakini yeye aliendelea kupangisha nyumba nzima inayolipiwa Sh. 2 milioni kwa mwezi licha ya kukamilika kwa nyumba iliyojengwa.

Jaffo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe CCM amesema kuwa katika manispaa hiyo kuna matatizo mengi na kwamba kitatumwa kikosi cha uchunguzi kutoka Tamisemi ili kufanya uchunguzi namna ambavyo fedha za ujenzi wa uzio zilivyotumika ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watakaobainika kuhusika na suala hilo.

“Huu ukuta (uzio) hauwezi kugharimu fedha zote hizo, nyie hata kwa madai yenu mnayosema mlifanya haraka kwa sababu ya uchaguzi sio kweli, hamtaweza kushawishi kwa hilo.

“Watanzania wana shida, dawa hospitalini hakuna, wakina mama wanajifungulia chini halafu, milioni 200 imekaa tu haina shughuli yeyote ile, mkurugenzi unapaswa kupisha uchunguzi kufanyika kwanza,” amesema Jaffo.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ulianza tangu mwaka 2013 lakini mpaka sasa mkurugenzi huyo amekataa kwenda kuishi kwa sababu ya kuwa chini ya kiwango na kwamba ipo katika maeneo hatarishi.

Amesema licha ya uongozi wa manispaa hiyo kujipangia kiwango cha Sh. 2 milioni kwa mwezi,kiwango hicho kipo juu ya kiwango cha serikali cha laki nane.

Kwa upande wake mkurugenzi, Wanga katika kujitetea amesema sababu zilizosababisha kushindwa kuhamia katika nyumba hiyo ni kutokana na kuwa katika eneo hatarishi ikilinganishwa na nafasi yake ya ukurugenzi.

“Waziri (Naibu Waziri Tamisemi) tunafanya kazi kubwa za wananchi na kazi zetu mnazifahamu, tunafanya watu wengine hawapendi tunachokifanya, sasa nikihamia katika nyumba ile na ukilinganisha na eneo ilipo ni hatari,” amesema Wanga.
 
Back
Top Bottom