Naibu Waziri Masauni amuagiza IGP Sirro kumsimamisha kazi na kumshusha cheo, Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye Chuo cha Polisi Dar es Salaam kutokana na kukiuka maagizo yake katika ujenzi wa mabweni chuoni hapo.

Pia, Masauni amemuelekeza IGP Sirro kumuondoa Mkuu wa Chuo hicho, Antony Ruttashuburugukwa na kumshusha cheo kutokana na kosa hilo.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa chuoni hapo, Masauni amesema alielekeza katika ujenzi huo watumike wafungwa kufanya kazi za vibarua ili kuokoa fedha lakini mkuu huyo wa chuo hakutekeleza agizo hilo.

“Rais alikubali kutupatia Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, tuliangalia na kuona tunaweza kuokoa Sh210 milioni za kuwalipa vibarua kwa kuwatumia wafungwa.”

“Nilizungumza na kamishna wa magereza akasema hilo linawezekana hivyo nikamuelekeza mkuu wa chuo kufanyia kazi suala hilo lakini leo nimekuja nakuta hali hii hakuna wafungwa,” amesema Masauni

Wakati Masauni anakagua ujenzi huo alikuta vijana wakifanya kazi na alipowahoji walimuleza kuwa wao ni vibarua wanaolipwa kwa siku.

Katika maelezo yake mmoja wa vibarua hao alionekana kutokuwa na utaalam wowote na alipelekwa hapo na mtu aliyemtoa gereji.

Majibu hayo yalionekana kumkasirisha Masauni, “Ina maana wewe umechukuliwa huko hufahamu chochote umeletwa hapa, haya ni mambo gani.”

Chanzo: Mwananchi
 
Naibu waziri halafu engineer hajui kwamba IGP hana mamlaka ya kumshusha cheo huyo bw polisi zaidi ya kumhamisha au kumsimamisha kazi.Huyo bw polisi kushushwa cheo lazima mahakama ya kipolisi ikae na imkute na hatia ambayo mojawapo ya schedule za adhabu iwe hiyo
 
Inchi imekabiziwa kwa watu sio kabisa ccm tafuteni solutions ya huyu kisirani 20/20 tunalimia MENO kwa kweli, hali ni ngumu sana na mbaya mno mtaan
IMG_20191127_171715.jpeg
 
Very unpofessional and unfair. ..
Huyu Naibu inabidi afutwe kazi yeye. ..
Kwani wafungwa wapo chini ya polisi?
Kama taratibu za kijeshi zinakataa kulikuwa na haja gani kukurupuka?
Unaepuka vip gharama kwa kutumia wafungwa. .. kwamba unachukilia labor work ni "zero" ilihali unajua sio kweli?

Watu wa pupa with no brain...
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye Chuo cha Polisi Dar es Salaam kutokana na kukiuka maagizo yake katika ujenzi wa mabweni chuoni hapo.

Pia, Masauni amemuelekeza IGP Sirro kumuondoa Mkuu wa Chuo hicho, Antony Rutashuburugukwa na kumshusha cheo kutokana na kosa hilo.

Akizungumza leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa chuoni hapo, Masauni amesema alielekeza katika ujenzi huo watumike wafungwa kufanya kazi za vibarua ili kuokoa fedha lakini mkuu huyo wa chuo hakutekeleza agizo hilo.

“Rais alikubali kutupatia Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, tuliangalia na kuona tunaweza kuokoa Sh210 milioni za kuwalipa vibarua kwa kuwatumia wafungwa.”

“Nilizungumza na kamishna wa magereza akasema hilo linawezekana hivyo nikamuelekeza mkuu wa chuo kufanyia kazi suala hilo lakini leo nimekuja nakuta hali hii hakuna wafungwa,” amesema Masauni.

Wakati Masauni anakagua ujenzi huo alikuta vijana wakifanya kazi na alipowahoji walimuleza kuwa wao ni vibarua wanaolipwa kwa siku.

Katika maelezo yake mmoja wa vibarua hao alionekana kutokuwa na utaalam wowote na alipelekwa hapo na mtu aliyemtoa gereji.

Majibu hayo yalionekana kumkasirisha Masauni, “Ina maana wewe umechukuliwa huko hufahamu chochote umeletwa hapa, haya ni mambo gani.”

Chanzo: Mwananchi
 
Siasa inasumbua sana kwenye jeshi la polisi, ndiyo maana baadhi ya raia wanawachukulia poa maaskari polisi huku JWTZ ikiheshimika kutokana na hata wakikosea, wanasiasa hawaingizi siasa za waziwazi, hii mbaya sana.
 
Back
Top Bottom