Chapat
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 283
- 202
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amewataka waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanza kutekeleza maelekezo ya Serikali yanayoagiza runinga zote zilizofungwa kwenye hospitali za umma kurusha matangazo yanayohusu elimu ya afya peke yake.
Dk Ndugulile ametoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua changamoto zinazowakabili wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo amesema lengo la Serikali kuweka runinga hizo ni kutoa elimu ya afya na si tamthilia michezo na burudani kama ilivyozoeleka.View attachment 994197 Chanzo: ITV Channel
Sent using Jamii Forums mobile app
Angesema madhara ya kuangalia izo chanel za burudani kwa wagonjwa ni zipi?