Naibu Waziri Kassim Majaliwa(CCM), atoa amri Sekondari ya Mpwapwa kufanya Tambiko

Atatufaa sana huyu, hata zile mashine za CT scan zinazoharibika kila Mara pale Muhimbili anaweza kuwapeleka wazee wakafanya tambiko na zisiharibike tena.
Hapakazituu, huku Kalandinga huku mtaalamu wa sayansi ya jadi. Hapo Maendeleo ni mbele kwa mbele
 
mpwapwa. Ingawa serikali ya tanzania haiamini katika ushirikina wala matambiko, kuna watu mbalimbali na jamii tofauti zinaamini katika mambo hayo mpaka waziri wa kikwete kwa tiketi ya ccm.

Ni kama hadithi, lakini katika tukio la februari 8 asubuhi, naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, kassim majaliwa(ccm) alitoa maagizo ya kufanyika kwa tambiko muda mfupi baada ya kuwasili eneo la sekondari ya mpwapwa kwa ajili ya kutoa pole na kuwafariji wanafunzi wa kike ambao bweni lao liliteketea kwa moto.


?kabla sijasema mambo mengi, naomba kuagiza na hili liwe ni agizo kwamba, lazima wazee waje hapa ili kufanya tambiko maana haiwezekani nyoka akageuka kuwa moto. Hii ni ajabu kweli, ndugu zangu, isiwe viongozi wa dini pekee yao tu,? anasema majaliwa.anatoa mfano kuwa katika shule ya sekondari ya mahuta, mkoani lindi kuliwahi kutokea mambo kama hayo, lakini walipoitwa wazee walipita na kuimba na hali ikatulia.

?unaweza kukuta wakaja hapa na kuimba tu na wakitoka mambo yote yanakuwa safi, huenda kuna mzee yupo hai au alishatangulia mbele za haki, lakini ana manung?uniko ya miaka mingi kwamba ardhi yake ilitwaliwa bila ya kulipwa fidia?, anasema hivyo akitolea mfano kuwa katika shule ya sekondari ya mahuta, mkoani lindi yalishatokea kama ya mpwapwa.

Mzee mohammed athuman mwile (86) aliunga mkono wazi la waziri na kusema kuwa kuhusu vifaa tambiko huhitaji kondoo pamoja na nguo nyeusi na kwamba kama watajiridhisha kuwa ni tambiko dogo, hakuna haja ya kufanya yote, bali ni wazee kusema maneno yao tu.

chanzo: mwananchi

ushirikina tu huu.karne ya sayansi na teknolojia.inasikitisha viongozi wetu na upeo wao wa kutatua matatizo.
 
Jf imebarikiwa maana ina watu utafikiri ''librarian'' likitokea tukio tu wanafukua hata habari za miaka kadhaa nyuma.

Hongera mkuu walau napata picha ya MR. PRIME MINISTER
 
Inasikitisha waziri mkuu reaction ya kwanza ya watu ni mshirikina. Nasikia pia ni ndugu na mama salma. Binamu yake Salam kikwete
 
Magufuli naye hayuko nyuma. Kuna siku nilimsikia bungeni akisema kuna kijiji kimoja bulldozer lilishindwa kungoa mti hadi ikabidi wakawaite wataalamu wa jadi wakaja wakafanya matambiko ndipo mti ukangoka. Eti aksema ndugu zangu msituone hivi kwenye kazi zetu tunakumbana na mengi! Du ndio viongozi wetu wakuu tulio nao Tanzania! Full imani za ushirikina!
 
Huyu ndo kiongozi sasa,hivi kuna anayedhani mheshimiwa angeenda pale akaanza kuwaambia watu wanaoamini mambo ya matambiko kuwa "sijui sayansi imefanya hivi" angeeleweka?.Muda mwingine ni busara tu katika muktadha husika ndo inayokomboa na si cheo wala we ni nani.
 
Tumepata waziri mkuu mshirikina! Swali linakuja je watu wawili wanaweza kutembea pamoja wasipopatana? Jibu ni hapana! Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na rais mshirikina! Ikitokea hivyo dhana ya hapa kazi tu itabadilika na kuwa hapa ni tambiko tu! Mungu wetu uwasamehe viongozi wetu! Ina maana vetting process haikuliona hili la ushirikina? au wanaona siyo tatizo?
 
Mizengo Alikuwa ana haki ya kulia bungeni maana wahusika alikuwa nao wizarani
 
Back
Top Bottom