Lushoto: Wazee wakausha maji kwa tambiko

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Wazee wa Kata ya Kwekanga Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wamezuia chanzo cha maji kutokutoa maji hadi kufanyike tambiko mara baadaya ya Mkandarasi kwenda kuanza mradi bila kuwashirikisha Wazee hao.

Akielezea sakata hilo Meneja wa Mamlaka ya Maji (RUWASA) Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mhandisi Erwin Sizinga, katika mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo amesema walifanya kikao eneo hilo na Wananchi wakawaeleza kuwa kuna chanzo cha maji lakini walipo fanya utafiti wakagundua chanzo hicho hakina maji ya kutosha.

“Mhe.Naibu Waziri tulipata chanzo Kata ya jirani Kijiji cha Makole na kilikuwa na maji ya kutosha lakini siku tuna mleta Mkandarasi yale maji hatukuyaona na tulivyokaa na Serikali ya Kijiji na Wazee wanasema kunataka kufanya tambiko kwasababu kuna mambo yalifanyika kwenye chanzo yamekosewa hivyo wakaomba mbuzi,
njiwa tukawapa pamoja na laki na nusu lakini hadi leo maji hakuna”

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema amesikiliza stori ya kuchinja kondoo na njiwa ili kufanya tambiko “Mimi sitaki kuongea tofauti, wanaoamini wakifanya huenda inasaidia sawa lakini niwaambie tambiko kubwa la vyanzo vya maji ni sisi wenyewe tunaoishi hapa kuacha kulima kandokando ya vyanzo vya maji hakuna tambiko kubwa kama hilo, hilo hatutahitaji kupeleka njiwa wala kondoo”

Sent from my 21061119AG using JamiiForums mobile app
 
Huyo muhandisi wamchunguze vyema
 
Wapingaji Wakuu wa uwepo wa Mungu watakuvaa hatari kama vipanga wakidai hakuna uchawi wala Mungu kumbe nyuma ya pazia ndiyo Washirikina wa kutupwa.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nyuma ya pazia ni maneno matupu tu uliyoamua kuyatunga.
Ni kama mimi nikiamua kusema wewe nyuma ya pazia huamini uwepo wa mungu ila hapa unajifanyisha tu.

Wewe umethibitisha huo uchawi?
 
Back
Top Bottom