Naibu Waziri Juliana Shonza na Waziri Mwakyembe, ujumbe huu unawahusu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Nimepitia mitandao mingi kuhusu kile kinachomtokea Mwanamuziki Diamond kwa kulaumiwa eti hakutenda haki kumtuhumu Naibu waziri Mh Juliana Shonza kwa kule kueleza hadharani kutoridhishwa na kufungiwa nyimbo zao ambapo pamoja na mengine Diaomond alilalamikia kutojulishwa na kuambiwa kwa njia rasmi za kiofisi kuhusu suala hilo na badala yake kulisikia kwenye vyombo vya habari.

Inasikitisha sana. Nani yuko juu ya sheria hapa ? Ina maana Diamond kama raia wa nchi hii hapaswi kulalamika hadharani kwa kuwa jambo linamuhusu Mh Waziri ? mbona yeye na wenzake nyimbo zao zilitangazwa kufungiwa hadharani na bila kuarifiwa rasmi ina maana mawaziri wao tu ndio wanastahiki heshima ?

Leo hii ukiwa waziri unataka uwe Malaika mdogo usujudiwe ? wapi wangesemea mambo yao na kusikika ikiwa chombo kilichotakiwa kiwateteee cha Omoja wa wasanii ndio kwanza kinajikomba kwa serikali ni wapi pengine ?

Diamond alieleza concern kubwa kuwa maandalizi waqnayoyafanya yanatumia gharama kubwa kwa nini kazi zao zinafungiwa bila kujali nguvu zao walizopoteza mara unastukinza waziri na vyombo vya serikali vinafungia tu ?

Juweni kuwa kuna mahali hakuko sawa, wasilaumiwe wanamuziki na kuwaacha BASATA KUTEKELEZA WAJIBU WAO WA UDHIBITI WA KAZI ZA WASANII HATIMA YAKE SERIKALI INAVURUGA NGUVU ZA WAJASIRIAMALI HAWA BURE. Kuna tatizo mahali kwa nini wasanii watumie gharama zao kubwa mpaka kufika mahala wakatoa nyimbo zisizofuata maadili kwa gharama zao halafu BASATA wanaponaje ? Mnaona ni sawa kweli ?

Diamond asionmewe bure alichokisema ni haki yake kusema na asiandamwe.


Ukiwa kiongozi unatakiwa uwe mfano wa wengine, Kama waziri Shonza hakuona busara ya kuwajulisha akina Diamond kwa njia za siri basi Serikali na yeye mwenyewe wasilalamike kusemwa hadharani. Ni hayo tu.


Kishada.
 
Serikali inashindwa kutambua kuwa kwa sasa wasanii wanalipa kodi kama huyo Diamond lazima ziwepo taratibu za kumfahamisha,alafu wasanii wa sasa wanauelewa si kama zamani kwaiyo mambo mengine unatumia busara,sheria na kanuni zilizopo, wewe unamfungia unatangaza redioni na yeye anaenda kukujibu kupitia redio unasema afate taratibu alalamike kwa barua mbona wewe ukufata hizo taratibu au zinatumika upande mmoja tu na mwingne azitumiki?!!
 
Viongozi Afrika ni Miungu watu.

Katika Nchi zote za Kidemokrasia, rafiki yangu asiyepungukiwa na kumbukumbu hupenda kuita "Nchi za mkumbokrasia" hakuna Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni hai.

Artlist kwa wenzetu wanajitahidi, kwa baadhi ya Mataifa. Hao wakifika Afrika hujiona kama wapo motoni.

Ni Wizara mahsusi kwa ajili ya kufungia magazeti, kazi za wasanii na kadhalika. Lengo lao ni kubana uhuru wa habari (kutoa-kupokea), kuanzisha vigenge vya kutafuta nini kimesemwa-na nani mtandaoni na mengine mengi ya sampuli hii.

Nb; Siungi mkono uandishi usiozingatia ethics za uandishi. Sanaa isiyoheshimu hadhira na utamaduni wao. Waandishi kanjanja nk.

Kazi ya Wizara ni Ulezi. Siyo uonevu.
 
Kila kundi katika jamii linaguswa na hii ni hatari huko tuendako.

Wasanii hawa wana nguvu hasa kwa vijana kuliko hata wanasiasa na tusisahau vijana hawa ndio wengi katika nchi hii.

Watu wamekosa maono kabisa.

Arrogance destroys foresight.
 
Acheni hizo, kwahiyo nyie mnaona alivyokua anaijibu serikali ni sawa? Anatakiwa ajifunze aache mipasho kama mtoto wa kike
 
Kila kundi katika jamii linaguswa na hii ni hatari huko tuendako.

Wasanii hawa wana nguvu hasa kwa vijana kuliko hata wanasiasa na tusisahau vijana hawa ndio wengi katika nchi hii.

Watu wamekosa maono kabisa.

Arrogance destroys foresight.
Hawa waonesha vyupi wana nguvu gani mkuu? Hebu watupishe huko, hawa si ndio walikuwaga wanamwaga radhi kwenye kampeni za ccm? Wacha cha moto wakione walifikri ule wimbo wa kuisoma namba ni wa wana UKAWA peke yao? Tena namwomba Shonza wakileta jeuri awapige marafuku kutumbuiza kwenye viwanja vya TZ pia awafungie na passport zao wasivuke mipaka kabisaaaa (ha ha ha haaaaaaa,, sijui inawezekana?)
 
Huu mfumo mpya wa kufukuza kazi na hata kufungia kazi za wengine kupitia redio na luninga na sio barua rasmi za kiofisi sio rasmi na haufai hata kidogo! Ni wangapi kati yetu waliokuwa wanaisikiliza station ya redio aliyokuwa nw siku hiyo? Itakuwaje kama kina diamond walikuwa nje ya nchi na hawakumsikia nw?

Kiukweli nw waziri alitakiwa kuiagiza mamalaka au idara inayohusika na sanaa kuwaandikia barua wa wito na kisha barua za kuifungia miziki yao na sio redio na tv!
Nw akiri tu kuwa kachemka kwa kuiingilia basata kazi zake kwani yeye alitakiwa kuwa mtu wa mwisho kama wasanii hawa wangeikaidi basata! Diamond et al mkazie tu huyo nw kwani hakufuata taratibu za kiofisi bali mahaba yake binafsi!
 
Kila kundi katika jamii linaguswa na hii ni hatari huko tuendako.

Wasanii hawa wana nguvu hasa kwa vijana kuliko hata wanasiasa na tusisahau vijana hawa ndio wengi katika nchi hii.

Watu wamekosa maono kabisa.

Arrogance destroys foresight.
utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !
 
Back
Top Bottom