NANCA
Member
- Jun 23, 2023
- 92
- 100
Hivi jamii forum ni ukurasa wa watu gani? Hivi Rais au Waziri mkuu na mawaziri wake wanatake time kutembelea ukurasa huu? Au wanadhani ukurasa huu ni wa wapiga kelele na upinzani? Hivi hawajui kua masikini wengi wasomi na wanaokandamizwa na wakoloni weusi ndo wako huku?
Hivi Rais hajui kua kitendo cha kutembelea Jamii forum japo kila siku kitamuwezesha kujua changamoto nyingi sana zinazowakumba watu wadogo na hatimae kuzitatua? Hivi hajui kua kwa kuutembelea ukurasa huu na kutatua changamoto zete kutamwezesha kua maarufu wa kweli hata kushinda uchaguzi 2025 bila hata kutumia nguvu.
Mimi nimshauri Rais Samia na jopo lake wajipe mda japo mara moja kila siku kutembelea jukwaa hili ili kuwafahamu wananchi wake. Badala ya kusafiri hata ulaya na kila kona duniani kututafutia mapesa bila kujua changamoto zetu ambazo zinaweza kutatuliwa bila mapesa hayo mapesa yanakua hayana maana sana.
Kama Rais anahangaika kutafuta mabilioni ili kujenga reli au barabara afu huku labda Kuna mbunge wake au mkurugenzi wake wanaendesha mchakato wa kunitapeli ardhi yangu hayo mapesa na mabarabara kwangu yanakua na maana gani?
Rais na waziri mkuu sisi kapuku mahala pa kuwapata nyie bila kikwazo ni huku mitandaoni na mahala pa heshima pa kuwapata nyie na kuwafikishia kero zetu ni hapa jamiiforum. Maana tukienda kwa wakurugenzi au wakuu wa wilaya na wa mikoa kwasababu wote wapo kiutafutaji na kiuzulumati basi matatizo yetu yanaishia kuwekwa kapuni ila hapa JF yanawekwa hadharani. Hivyo kwa kuingia hapa JF mtakua katika nafasi nzuri ya kutupatia haki zetu
Pia niwashauri JF muweke jukwaa maarum kwaajili ya high government officials ambapo hapo mtakua mnatupia malalamiko ya maana juu ya haki za watu yanayowalenga serikali kuu, na iwe ni page ambayo mtu hawezi post wala kukomenti ila ni nyie tu baada ya kuchuja lalamiko la mtu. Lisiwe jukwaa la kisiasa bali la malalmiko ya wananchi juu ya haki zao labda hapo serikali itaona kero zetu.
Binafsi nipo kwenye mapambano ya haki yangu ya ardhi na nipo njiani kwenda kumiona waziri wa ardhi, mkuu hadi rais. Ktk mapambano haya mkurugenzi na watu wake na huyo anaewatuma waamue kuniachia ardhi yangu au wanaipoteze vinginevyo sirudi nyuma hadi nazeeka na nazikwa. Ata sisi marofa Kama Kama wanavyotuita tunahaki ya kuandaa maisha bora ya wanetu.