Naibu Waziri January Makamba anatembelea Bajaj

Naibu Waziri January Makamba anatembelea Bajaj

By
George Smiley
Naibu waziri...

If only mawaziri wengine wangeweza kuwafikiria walipa kodi na kuiga mfano wa Naibu waziri Kijana Ndugu January Makamba.

Hivi mawaziri wetu wanavyopenda anasa wangekuwa kama January tungekuwa mbali sana.

Huyu ndiye Rais nimtakae.
Kuna usemi wa mtu mmoja mwenye busara aliyewahi kusema "Mtu akikupa wazo la kipumbavu akijua wewe unalifahamu la kipumbavu na ukalikubali basi atakuona wewe ni mpumbavu kweli kweli." Ndivyo ilivyo kwa mleta mada hii ambaye bila shaka ametumwa na mhusika yaani Makamba Jr. Sisi hatukubali mawazo yako kwa sababu ni ya kijinga na sisi si wajinga.
Bwana George; yaani huyo ndiye Rais umtakae kwa kupiga picha kwenye Bajaji tu au kuna jambo zaidi ya hapo? Kwanza picha yenyewe imepigwa beach akiwa kwenye anasa zake, hapo amepiga picha tu, kuna Vx inamsubiri tena inaonekana! Hata dereva wa Bajaji hayumo! Zaidi ya hapo kupanda Bajaji si kigezo cha kuwa "Mtu wa watu, asiyependa Makuu" je akitokea mwingine akipiga picha juu ya punda utamwacha huyu na kumchagua yule mwingine?
Mlimpamba hivyo "Sindbad" eti mtu wa watu, mwenye mvuto, kijana, asiyependa makuu na sifa nyingine kibao lakini sasa yuko wapi? Si anapasua anga kila kukicha?
 
Naomba nikusahihishe.

Sema, Makamba, Jr. apinga picha kwenye Bajaj.

Bajaj imesimama, hakuna anayeendesha. Hatutaki ujiko usio na maana.


Hapo mlalilaN umemaliza kila kitu,Hivi waziri au mbunge akipiga picha kwenye baiskeli ya kuchezea mtoto wake utasema waziri anatembelea baiskeli? Tuwasifie viongozi wetu kwa majukumu yao sio kwa picha wanazopiga kwenye garden zao.Bajaj gani inatembea bila dereva au kuna bajaji zinatumia remote tz.Mleta mada acha kutumika hovyo...nyambafu.
 
Picha yenyewe inamwonyesha peke yake yuko wapi dereva anamwendesha kama si choo cha k tunapelekwa
Hamna hata watu pembeni alikuwa anapita wapi hata watu wa pembeni hawapo
dereva wa hiyo bajaji haonekani au ni wa kitu chenye nja kali au anaendeshwa na maruhani ndio hawaonekani au malaika alivyokaa ni pozi la picha
wala sioni ajabu kupanda kwa sekunde ajabu ungekuwa mfumo wake barabara ya kwenda kazini kwake mfano posta unambiwa huyo ni january anapita tumemarks hata bajaji yake anaenda kazini au viwanja au kitaa unamkuta nayo
 
Anajifanya kupiga picha kwenye Bajaji ili apate kuonekana anajali masikini. Kuna siku nilimkuta Chalinze anajifanya ananunua chipsi kavu na vitumbua, lakini alipofika mbele kidogo ya Bwawani akavimwaga vyote nje ya gari.

Radhia sweety sijakusoma muda mrefu,nimemis usemi wako "watu wengine bwana".au ulipigwa ban?
 
Mzushi tuu mbona hata kibajaji chenyewe hakina suka, halafu kakaa pozi la picha kbs, tumechoka kudanganywa, na iyo v 8, pembeni ni ya nani.
 
Hata kwetu kuna kasumba ya kuamini mzungu akiendesha baiskel anafanya mazoezi na mbongo akiendesha anasafiri, na ndivyo nionavyo leo makamba ana nini kikubwa asipande bajaj? na kama anaigiza kwa stahili ya kujizolea ujiko imekula kwake, kwani inawezekana ameona yasimkute ya mh. zitto na hammer yake na ya yule wa kwetu aliyesema akipata ubunge ataweka rehani gari ya mkuu wa mkoa na kupiga mnada na baada ya kupata kanunua bmw kali?
 
sijawahi kuona waziri au kiongozi yoyote wa Tanzania ndani ya kibajaj let alone akitembelea bajaj

na kama hii ni kweli kuhusu January bas hongera zake.

sielewi kwa nini anachukiwa hivi na vijana wenzake mitandaoni
 
Mbona dereva wa bajaji yenyewe haonekani?halafu hiyo picha inaonesha alijiandaa kuipiga ili kuzuga watu.
 
Bajaj haitembei haina dereva unamwona kabisa anatengeneza pozi ili apigwe picha huu ni usanii
 
sijawahi kuona waziri au kiongozi yoyote wa Tanzania ndani ya kibajaj let alone akitembelea bajaj

na kama hii ni kweli kuhusu January bas hongera zake.

sielewi kwa nini anachukiwa hivi na vijana wenzake mitandaoni
Hongera ya kupanda bajaji?kwasababu hujawahi kuona wengine waliopanda?hata ukiona akinya hadharani utampa hongera kwa kuwa hujawahi ona wengine tusishabikie kila kitu huu ni ujinga
 
Usikute alikua naigiza filamu ya bongo movie...!! Hawashindwi hawa jamaa kufanya any drama just to catch audience kwenye mbio zake za 2015...!! Hii nchi hii dah mungu tu ndo anajua tunavyofanyiwa michezo ya kuigiza..!! kazi ipo 2015, bado yanakuja mengi..!! Nahisi wapo watakao swaga ng'ombe toka arusha/bariadi mpaka dar...!!
 
Hizo ni kamba tu Lol!!kwa wale wajinga wata like kumbe hawafahamu kuwa wao ndio waliwao,hapo kakaa kwa hicho kibajaji kama wanavyopiga kampein na kusema maisha bora kwa kila mtanzania na walishapata lakini hakuna kitu na wao wako wanapeta kwenye Mitoyota V8,V6 na Mijinisani lol

Pia niko na wasiwasi huenda ana biashara ya bajaji huenda anvyo kama 100 hivi Lol ngoja wale sasa lakini sound ni hapo 2015 lazima kitaeleweka tu kwani hata Vijana wengi tu ambao wako nje ya nchi watatimba Bongo kukomboa nchi kutoka kwa hizi takataka Ccm Magamba,wateka nyara,wala rushwa lazima kieleweke
 
Karithi usanii kutoka kwa baba yake (Like father like son)
Baba yake wakati alikuwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam alituhadaa na lunch za mahindi ya kuchoma na viazi.

January is trying too hard to impress us; kama sikosei kuna kipindi picha iliwekwa hapa akiwa Ubungo anakula mahindi au chipsi dume.

Lakini mimi binafsi nina amini ana uwezo mkubwa wa kuongoza na kutulea maisha bora zaidi ya Kikwete
 
Kwani picha imepigwa wapi? Hiyo Bajaj inaonekana ni mpya kabisa. Isitoshe Bajaj ni off limits City Center.
 
Ingekuwa ndio maisha yake yako hivyo asingekuwa na haja ya kupiga picha akiwa kwenye bajaji...hiyo ni Kaole!!!!!
 
Watanzania kaeni chonjo na kuweni macho mana danganya toto sasa ndo mda wake mana mbio za kusaka hatamu zi usoni na wajanja wote wataibuka kwa style tofauti. Huyo hana jipya mana mtoto wa nyoka ni nyoka hawezi kuwa mbuzi hata siku moja.
 
Back
Top Bottom