Naibu Spika kaacha Bunge la Bajeti ameambatana na Rais, tunapeleka wapi mihimili hii?

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Tulia Ackson ni Mbunge wa kuteuliwa huko Kinondoni, lakini pia ni Naibu spika wa Bunge na kwa Sasa Bunge la Budget linaendelea.

Huyu pia ni mzaliwa wa Mbeya, Mhe.Rais yupo Mbeya na yeye yupo naye kila anapokwenda, nashindwa kuelewa yupo kwa nafasi ya Ubunge wa kuteuliwa Kinondoni au Ni anamwakilisha Spika au ameenda kutembele mkoa aliozaliwa?

Huyu ni kiongozi wa Bunge anaachaje kazi zake? Huu muhimili unatatizo gani awamu hii?
 
mwanakuvi- find, mwanakuvi- get, ukitaka kushiba ni lazima ukae karibu na alie shika sahaman ya chakula!
 
Mheshimiwa hakuchaguliwa na wananchi wa Kinondoni, ubunge wa kuteuliwa ni fadhila ya kikatiba ndo maana yuko na aliyemteua na ndo maana hata kasherehe kadogo Ikulu huwa handuki akifuatana na boss wake kule bungeni.
 
Tulia Ackson ni Mbunge wa kuteuliwa huko Kinondoni, lakini pia ni Naibu spika wa Bunge na kwa Sasa Bunge la Budget linaendelea.

Huyu pia ni mzaliwa wa Mbeya, Mhe.Rais yupo Mbeya na yeye yupo naye kila anapokwenda, nashindwa kuelewa yupo kwa nafasi ya Ubunge wa kuteuliwa Kinondoni au Ni anamwakilisha Spika au ameenda kutembele mkoa aliozaliwa?

Huyu ni kiongozi wa Bunge anaachaje kazi zake? Huu muhimili unatatizo gani awamu hii?

Huyo aliyeko naye ndio bunge lenyewe. Hakuna lolote linajadiliwa bila ruhusa yake. Wale walioko bungeni hamna lolote la maana wanajadili bali kusaka posho. Huyo aliyenaye akiamua chochote kinafanyika bila hata ridhaa ya bunge. Ameona ni bora aendelee na kampeni kuhadaa umma wa wana Mbeya kwamba anawapigania, ili vyombo vya dola vipate urahisi wa kusimamia yeye kutangazwa mshindi nje ya box la kura.
 
First they came for the socialists,
and I did not speak out—because
I was not a socialist.
Then they came for the trade
unionists, and I did not speak out
— because I was not a trade
unionist.
Then they came for the Jews, and
I did not speak out—because I
was not a Jew.
Then they came for me—and
there was no one left to speak for
me.


Tukae kimya maana huyu dada toka alipoteuliwa hatukusema mapungufu yalipo ndani yake, lakini pia ajakubali kuwa Naibu anataman kuwa Spika ndo maana anaanzisha leo ndondo, kesho mchakamchaka,Mara vikoba nk Ana uchu wa madaraka,
 
Kwani bunge limesimama kumsubiri? au ukishakuwa spika huruhusiwi kutembea popote?
Acha wivu man.
Mkiambiwa mna akili ya KUSHIKIWA mnasema mmetukanwa sasa kulikuwa na maana gani wewe kuchangia kma unajua una akili fupi? au unataka na wewe ujipendekeze upewe kitengo maana sasa hivi usipojipendekeza unaishia tu kuvaa HAPA KAZI TU alafu unashindia mihogo lumumba.
Hivi unajua unajua kazi za mihimili hii mi3 na nafasi zake katika nchi? ni bora tu ungesema kuwa ameenda mbeya maan ndio anaandaliwa achukue jimbo kule ningekuelewa sio kuropoka ropoka tu, Bunge la TZ lipo mfukoni mwa mkulu ndio maana hawaoni ajabu ata kupiga kufuli office yao ikitokea wameambiwa na mkulu.
 
Back
Top Bottom