Naibu spika apindisha kanuni tena

The Listener

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
993
213
Ni maajabu nayashuhudia live TBC toka Bungeni Dodoma. Yapata dakika kama mbili hivi zimepita Naibu speaker katoa maagizo wabunge wote walio nje ya bunge waitwe kwa kengele kama utaratibu unavyotaka ili idadi ya wabunge ifikie matakwa ya kanuni. Hii ni baada ya baadhi ya wabunge toka upinzani kumkomalia kuwa kanuni haziruhusu kupitisha hoja ya waziri kama idadi ya wabunge haifiki nusu. Sasa ndo mbinde laendelea hapa. Ntatoa updtaes kadri ya mambo yanavyokwenda
 
SASA HIVI BUNGENI SPIKA AMEAGIZA KENGELE IGONGWE ILI WABUNGE WALIOKO NJE WAINGIE
ni kutokana na baadhi ya wabunge akiwemo Mbatia, Kafulila na machali kuomba utaratibu kuhusu kanuni ya 77
 
TBC kama kawaida wamezima mitambo yao kwa kisingizio cha bad or weak signal kwa hiyo hatujui kinachoendelea. Ama kweli kila kitu kinapindishwa na hawa wakubwa
 
Nusu ya wabunge waliohitajika kwa mujibu wa kanuni ni 176 lakini kwa madai ya watoa hoja idadi yao waliomo bungeni ni kama 110 hivi kwa hiyo speaker ameamua kwenda kuwaokoteza walioko nje. Nadhani na inanipa dukuduku kwamba hata jitihada za kuwapigia simu wale ambao hawakufika toka asubuhi zinafanyika ili 'column' itimie. Naona bado bilabila kwani Tv TBC inaonyesha chengachenga
 
Daaah sasa naona TBC wanaendela na matangazo ya biashara kwa atakayejua kinachojiri/KILICHOJIRI atujuze
 
Ni maajabu nayashuhudia live TBC toka Bungeni Dodoma. Yapata dakika kama mbili hivi zimepita Naibu speaker katoa maagizo wabunge wote walio nje ya bunge waitwe kwa kengele kama utaratibu unavyotaka ili idadi ya wabunge ifikie matakwa ya kanuni. Hii ni baada ya baadhi ya wabunge toka upinzani kumkomalia kuwa kanuni haziruhusu kupitisha hoja ya waziri kama idadi ya wabunge haifiki nusu. Sasa ndo mbinde laendelea hapa. Ntatoa updtaes kadri ya mambo yanavyokwenda
aisee tbc wamezima mitambo
 
Huyu Mgogo mwenzangu Ndugai, anatia iabu..

"Muwaha nhaule ulichikomaza nhayiyo?"
 
Inasemaji iyo kanuni?

kanuni inataka kuwepo kwa nusu ya wabunge ili kuweza kupitisha maamuzi bungeni lakini kwa jinsi mahudhurio yalivo Mbatia anasema amehesabu na kuona wabunge waliopo hawazidi mia na kumi wakati nusu inapaswa kuwa mia sabini na tano
 
Naibu Spika ameagiza waondolewe hewani... Sijui wameamua 'kuzichapa au vipi' Cable ya Signal nimeambiwa imechomolewa fasta wala hawakusubiri watolewe online kawaida.
 
Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano Mh Job Ndugai leo amepindisha kanuni waziwazi kufuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa kuteuliwa, ndugu James Mbatia kuhusu kuahirisha bunge.

Mheshimiwa Mbatia alitoa hoja hiyo mara tu waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh chizza kumaliza kutoa majumuisho ya bajeti ya wizara yake.


Mh Mbatia alisema kwa kuwa idadi ya wabunge waliopo bungeni haifiki nusu ya wabunge ambao ni 176 kwa muda huo, kanuni haielekezi bunge kuendelea kufanya maamuzi ya kupitisha bajeti ya wizara hiyo.


Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge Mkosamali pamoja na Machali lakini Naibu spika aliamuru bunge kuendelea na kikao hicho. Kuona hivyo mnadhimu mkuu wa upinzani Ndugu Tundu lissu nae alisimama kuendelea kuomba kanuni hiyo kufuatwa lakini dhahiri shahiri Naibu spika alionekana wazi kutopendelea suala hilo kufanyika.
 
Back
Top Bottom