Naibu Meya ataka wenye ulemavu wasijinyanyapae

Naibu Meya ataka wenye ulemavu wasijinyanyapae

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amehimiza watu wenye ulemavu kutojinyanyapaa kwa kuchukulia ulemavu wao kuwa ni kikwazo katika kufanya kazi badala yake, wafanye kazi na kutumia fursa walizo nazo.

Kumbilamoto alitoa mwito huo jana katika dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na kampuni ya huduma ya chakula, Nemmy Swahilis Food kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua fimbo nyeupe zinazotumiwa na watu wenye ulemavu wa kutoona.

“Tumepata Rais anayeangalia uwezo wa kazi na sio ulemavu wa mtu, kwa hiyo mimi niwasisitize tufanye kazi kwa bidii, bila kujali ulemavu wetu na pengine rais akawaona na kuwateua katika nafasi mbalimbali,” alisema.

Katika dhifa hiyo iliyodhaminiwa pia na hoteli ya Seashells, kampuni ya ukopeshaji fedha ya Jero na pia kampuni ya mitindo ya GND, zilipatikana Sh 825,000 papo hapo na ahadi. Waandaaji wa tukio hilo ambao ni Muna Mwendo na Nemmy Kihange kutoka Nemmy Swahilis Food kwa nyakati tofauti, walisema jamii inapaswa kuwakumbuka watu wenye uhitaji.

“Tuliona tuwakumbuke wenzetu hawa watu wenye ulemavu, tuandae chakula na kuchangisha fedha ambazo zitasaidia kuwanunulia fimbo maalumu za kutembelea, ni kidogo lakini ni jambo ambalo litawasaidia,” alisema Munna.

Mwenyekiti wa Shirikisho la kuendeleza Wasioona Kiuchumi na Kijamii Tanzania, Nuru Awadhi aliishukuru Nemmy Swahilis Food kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu.
 
Back
Top Bottom