Naibu kamishna mstaafu afariki Dodoma kifo chenye utata

Nyadunga

Senior Member
Aug 12, 2011
107
64
Dodoma. Naibu Kamishna mstaafu wa Magereza nchini (DCP), Luhusa Chiza (62) amefariki dunia katika mazingira ya utata kwenye hoteli ya Kitemba mjini hapa.

Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, mwili wa Chiza uligunduliwa juzi mchana na mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo alipotaka kufanya usafi.

Taarifa kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji wa Dodoma, zilidai Chiza aliingia Novemba 15, usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema mwili wa Chiza ulikutwa ukiwa na damu puani na kwamba, aliingia chumbani akiwa na msichana ambaye wanamtafuta.
 
Ukistaafu pension kula na wajukuu zako, likizo wakutembelee kwa babu na bibi waambulie hata visoda na visafari vya hapa na pale.

Sasa we staafu alafu tafuta wadada wa mjini, faida ndio hiyo either usingizie pesa ya pension ina majini au ukutwe na umauti kama huyo
 
Eeenh, sasa umri wa miaka 62 ni muda wakufanya mambo ya kipuuuzi. Je, huo c umri wa kukaa na wajukuu ukawapigia stori za ujana? Au alipiga ile kitu inaitwa MKUYATI ikamzidi speed.

R.i.P
 
Ameleweshwa madawa wee mpaka aka R.I.P... Wanawake wa Dodoma hatari sana wana ule mtandao wao unaitwa HITWE ndio wanajiuzia huko kwa wabunge
 
Wanamtafuta binti wa nini wakati nibdhahiri shairi kuwa mzee papuchi imemzidi nguvu akautema. Kapata mavuno sahihi maana mshahara wa dhambi ni mauti. Liwe funzo. Kuna yule mwingine aliyempiga rasasi dereva wa daladala naye nasikia alifia papuchini. Mungu tusaidie sana.
 
Booster mbaya ukiikoleza sana ili ufike kileleni. Haichelewi kupasua mishipa ya fahamu", rip mzee, pensheni imekupoza
 
Wanamtafuta binti wa nini wakati nibdhahiri shairi kuwa mzee papuchi imemzidi nguvu akautema. Kapata mavuno sahihi maana mshahara wa dhambi ni mauti. Liwe funzo. Kuna yule mwingine aliyempiga rasasi dereva wa daladala naye nasikia alifia papuchini. Mungu tusaidie sana.
Sijaona utata kama ilivyoletwa na mleta uzi
 
Back
Top Bottom