Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
huyu Nahodha kidogo ana make sense kulingana na maelezo yake..
Mfumo mbovu wa utawala. Manumba alitakiwa awajibike kwa Waziri au IGP sasa kila mtu anateuliwa na Rais no proper channel of command.
huyu Nahodha kidogo ana make sense kulingana na maelezo yake..
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.Mkuu Pasco, nikuhakikishie serikali imelikwepa hili suala si kwasababu ya uchunguzi, ni kwa unyeti wake na jinsi linavyogusa watu wasiogusika.
Waziri mkuu alikwepa, nahodha akakwepa, haji Mponda akaijitoa. Manumba amekubali kubeba mzigo asioujua au anaoujua ndani kuna nini. Leo likitokea lisilotarajiwa na mwenyezi aepushe, Manumba si mhusika tu ni mshiriki mkubwa. Hilo lipo katika kumbu kumbu za wanadamu na ataishi nalo.
Kama taarifa zilikuwa katika Cabinet, ni wazi yeye anajua hilo akiwa DCI. Kwa mtu mwenye akili asingekubali kutupiwa kamba na kuidaka. Ni wazi nahodha sasa anajua na amesoma watu wanasema nini naye anajivua mzigo wa misumari aliojitwika Manumba.
Kama Manumba angetumia fikra kidogo, angewauliza viongozi wenzake juu ya kushindwa kujibu tuhuma au kuzifanyia uchunguzi tuhuma za tishio la mauaji ya Dr Mwakyembe ambayo amekalia ofisini mwake miaka nenda rudi.
Baada ya viongozi wenzake kumkana iwe kwa ukweli uliopo au uongo, Manumba angejiuzulu mara moja. Sasa hivi heshima yake ndani ya vyombo vya dola imekwisha na amebaki kuogopwa tu kama tunavyomuogopa kiumbe yoyote anayeweza kutudhuru.
Pasco, fuatilia upandaji ngazi wa Manumba, angalia alifanya kazi na nani hutakawia kujua kuwa Manumba yupo njia panda akitafakari amtumikie nani kati ya 'mabwana wawili'. Serikali au waliomtuma awasafishe.
Unakumbuka msemo maarufu JF wa mapacha watatu?
Leo mkuu Pasco umegeuka serikali ile ile uliyosema uwezo wake wa uchunguzi umefika mwisho, na taarifa yake ni ya mwisho! Ukasema Sitta ashtakiwe kwa uzushi. Sisi tulijua wanatuchezea akili hawa akina serikali mapema kabisa.
Kwa jinsi wanavyojikanyaga na kujichanganya ndivyo shaka yetu inavyozidi.
Mshauri Manumba, kama anaona anaonewa ajiuzulu. Akiendelea kuwepo tutamuuliza kuhusu majaribio ya mauaji aliyoyaminya ofisini kwake na sasa anakurupuka na hili asilojua au analolijua Kwa kutoa taarifa za kiwango cha darasa la VI B.
Msimamo wa hoja zangu upo pale pale, tunataka ukweli na wala ukweli usifichwe kwa mwamvuli wowote.
Kama ni uharamia, maharamia watajwe na kama ni uzushi, basi wazushi watajwe.
Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.
Mtakumbuka mwanajf Hutaki Unaacha alisema nini kuhusu Dr. Omar Ali Juma!. Hivyo vyovyote itakavyo kuwa huo uchunguzi wa forensic utakuja with nothing new!.
Tumuombee tuu Mwakiyembe apate uponyaji wa haraka na arejee nyumbani bukheri wa afya ili yaliyomsibu yabaki kuwa ni "live to tell".
Between the two devils, choose the lesser!.i don't trust lowassa. he's greedy.
i dont trust mwakyembe. he's a hypocrite.
swali.....which of the two would you be "happier" to stay away from??
i know where my choice lies.
Out of topic: Hivi wenzangu mmenote ukifungua pages zinazofuatia ile starting thread haipo!. Au ni kwangu tuu maana niko mobile?!.
Mkuu Ngumijiwe, sio kidogo ana make sense, he is making all the senses kwa sababu hii ndio mara ya kwanza serikali imekiri inafanya uchunguzi wa kipolisi na uchunguzi huu sio tuu utahusu uwezekano wa kupewa sumu bali madai yote ya Mwakyembe ambayo huko nyuma waliyapuuza!.
Mkuu Pasco, hoja inayosumbua siyo matokeo ya uchunguzi ni mchanganyiko wa mambo mengi na hivyo hatutegemei serikali iliyombakiza Manumba, Mponda na Nahodha madarakani kuja na kitu kipya.Mkuu Nguruvi3, mimi bado nasimama na DCI Manumba, ripoti ndio ile wala msitatajie kipya!. Maadam Nahodha ametoa maagizo mapya ya kufanyika forensic investigations, sasa ni busara tukasubiri hayo matokeo yatakayoweka hadharani mbivu na mbichi!.
Mtakumbuka mwanajf Hutaki Unaacha alisema nini kuhusu Dr. Omar Ali Juma!. Hivyo vyovyote itakavyo kuwa huo uchunguzi wa forensic utakuja with nothing new!.
Tumuombee tuu Mwakiyembe apate uponyaji wa haraka na arejee nyumbani bukheri wa afya ili yaliyomsibu yabaki kuwa ni "live to tell".