Nahitaji wataalamu wa ujenzi wa nyumba

Nahitaji wataalamu wa ujenzi wa nyumba

Jojo123

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
437
Reaction score
715
Hello guys..
Naombeni wataalamu WA Ujenzi au MTU yeyote mwenye uzoefu wa Maswala ya Ujenzi anisaidie mawazo tafafhali.

1. Ninakiwanja ila kina slope (Nafanyaje ili kufanya ujenzi rahisi?)

2. Je! Naanzaje kwa kiwanja kilicho mbali namakazi yangu sina maji ingawa majirani kadhaa wanayo ila nimepata kiwanja katika ya majirani wenye majivuno kila mtu na geti lake ukigonga kuongea nao hawana muda na dharau nyingi.. Nawaza nikiweka hata tofali sizitaibiwa na watu maana siishi uko.

3. Naombeni ushauri naanzaje ujenzi wa 3rooms house

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshapiga hesabu garama ya kufyatua na ile ya kununua tu tofari ipi n nafuu?.

Kama huezi simamia basi n bora save taratibu hela,ikifika kiasi fulani unanunua unapeleka site.
Ukishindwa kila unachosave fungua account weka,ikifka 2m,nunua tofari 1800 za block.

Si rahisi watu kuiba tofari,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungetupia picha ya eneo lako nipate kuona hiyo slope.. ila kuna alternative nyingi za kujenga kwenye slope..
1.kama slope ya kawaida unawenza kujenga msingi wa kawaida, sehemu itayokuwa chini utaijaza na sehemu iliyo juu sana utachimba..
2.kama slope nikubwa sn. Inamaana garama za kupajaza inaweza kuwa kubwa basi sehemu ambayo iko chili badala ya kupajaza ungeweza kujenga chumba au store au parking inakuwa kama underground storey mpaka kupata level ya sehemu mbayo iko juu.sehemu ambayo iko juu hapo msingi wako utaanzia..
Ila kama hujaelewa ni pm ntakusaidia kwa ushauri zaidi bure kabisa thanks and wlcm..

Iphone 5
 
e15a55b0767b98bb487b91e017b9a539.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Look at this slope brother

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo slope ya kawaida.. wakati waujenzi utachimba zaidi nyuma kuweka msingi na udogo huo utakaochimba ndio utakao jaza kwa mbele eleo hilo ambalo utajenga. Sehemu ya eneo lililobaki utali shape kulingana na unataka kuweka nn.. ila slope hiyo ni ya kwaida tu navyooona kwa picha.. fundi mzoefu hapo atapajenga bila shida..

Iphone 5
 
OK brother ,

Vip ushauri wa tofali ni bora kuchukuwa machine na kufyatua up bora kununua??

Je kufyatua mfuko mmoja unatoa tofli ngapi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshapiga hesabu garama ya kufyatua na ile ya kununua tu tofari ipi n nafuu?.

Kama huezi simamia basi n bora save taratibu hela,ikifika kiasi fulani unanunua unapeleka site.
Ukishindwa kila unachosave fungua account weka,ikifka 2m,nunua tofari 1800 za block.

Si rahisi watu kuiba tofari,

Sent using Jamii Forums mobile app
Je tofali za inches ngap ndio bora kwa ujenzo wa msingi na nyumba nzima kabisa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ni fundi. Ninauzi wangu unaitwa ujenzi bora wa nyumba pale jukwaa la matangazo.
Karibu tufanye kazi. Kuhusu majirani kutoa maji tuachie sisi mafundi, watatoa tu lkn lazima uyalipie.

Nitafute kwa 0655173113
 
Look at this slope brother

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiyo slope inaweza kuonekana ndogo lakini kuja kuitafuta level, zinaweza kupotea tofali za kutosha.
Pili kutokana na eneo la hicho kiwanja udongo wake kama ni wa mfinyanzi ule wa kupasuka itabidi ununue kifusi kujaza ili kupata usawa uanze ujenzi.

Ushauri wangu, kama mfuko unaruhusu, ni bora ukafanya upande mmoja ukawa kama ghorofa ili kuepusha kununua kifuzi cha kujaza na kupoteza tofali bure. Unaweza kupata parking au vyumba viwili kama sio vitatu chini kwa upande wenye mteremko mkali.

Changamoto ya huo ushauri wa pili ni gharama za msingi imara na lile zege.

Kuhusu maji, fundi walijenga kakisima kadogo nikawa nanunua maji kwenye magari wanakuja kuhamishia hapo, hii inakuepusha ulinzi wa kukodi simtank na ulinzi. Uzuri hicho kisima ukikijenga utakitumia hata baada ya ujenzi, ni kidogo sana ili kupunguza gharama.
 
Kwani mkuu huo ujenzi wa msingi kama huo (kwa hicho kighorofa cha upande mmoja) unaweza gharimu kiasi gani kwa nyumba ya vyumba vinne?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hongera kwa kupata kiwanja sehemu ambayo watu wamejenga na mageti yao. ni dalili sio maeneo ya uswahili hivyo usihofu kabisa kuweka tofali zako hapo hakuna mwenye njaa atakayeiba tofali zako coz mazingira yanaonyesha na kwa uzoefu wangu watu hawaibi tofali labda uhofie vingine.kuhusu ujenzi wenzangu washachangia vya kutosha chukua ushauri unaokufaa.narudia tena hongera sana kwa kujenga sehemu ambapo majirani wameweka mageti yao.nadhani ni salama zaidi kwa maisha yetu ya sasa kujenga sehemu ambapo kila mtu ana maisha yake.sipendi uswahilini
 
Waswahili wana mambo ya ajabu sana
 
Mm ni fundi. Ninauzi wangu unaitwa ujenzi bora wa nyumba pale jukwaa la matangazo.
Karibu tufanye kazi. Kuhusu majirani kutoa maji tuachie sisi mafundi, watatoa tu lkn lazima uyalipie.

Nitafute kwa 0655173113
Nyie bei zenu kubwa,nashauri jamaa atumie mafundi wa mitaani kutoka eneo la kiwanja maana wanakuaga wazoefu wa maeneo hayo hata bei zao ni kawaida sana.lakini hawa wanaotaka mpaka kukuandalia BOQ Mara quantity survey wanakula hela yote kabla hats msingi kwa kisingizio cha consultancy.

Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom