Nahitaji wadau/wawekezaji katika madini na gemstone kuna project hapa ya kuiendeleza

Sep 8, 2017
55
259
Habari,

Kwa wale wadau wanaojihusisha na biashara ya madini leo nina jambo hapa nahitaji tuliangalie. Kumekuwa na uhaba au kutokuwa wazi kwa biashara hii ya madini na vito vya thamani mpaka kuonekana kanakwamba ni biashara ya utapeli au ushirikina wakati ni biashara kama biashara zingiaze.

nimeona kuna gap la kukutana kati ya wenye madini na wanunuzi na pia kati ya wamiliki wa migodi ambao wameshindwa kuendeleza migodi yao kwa kukosa fedha za uwekezaji. Wakati huo huo kuna wawekezaji wanatafuta migodi ya kuiendeleza na wengi wao wakiwa ni raia wa nje ya nchi.

Sio hivyo tu uaminifu umekuwa mdogo hasa hasa kwetu waafrika kitu ambacho kinapelekea wageni kukimbia kwa kuogopa kutapeliwa na kukosa ushirikiano thabiti katika biashara hii.

Hii imepelekea hata wageni au wateja wa kununua madini kutoka nje ya nchi kutokuwa na imani ya kuagiza mzigo wa madini au vito vya thamani ni mpaka wafike wenyewe.

Suluhishi ni nini?

Nimeona nije na center ambayo itatambulika na kuaminika kutoka kwa wadau wote wa madini.center hii itakuwa ni soko la mtandaoni la madini na vito vya thamani. Hii itakuwa ni legal na registered company katika biashara hii ya madini.

Kwa dunia ya sasa ya teknolojia nimeona center hii iwe ni katika nwebsite na mobile app ambapo wadau wote wa madini watatambulika na kusajiriwa kutumia system hii (hii ni kuanzia kwa brokers,ma dealers, wachimbaji na wateja wa madini na vito vya thamani) kupitia center hii itajengwa trust na kuondoa wale walanguzi na matapeli wote waliopo katika biashara hii.

Ndani ya website hii kutakuwa na kuuzwa kwa madini na vito vya thamani, pia kutakuwa kunatangazwa fursa zilizopo kama kazi,migodi inayohitaji wawekezaji nk, yanayohusiana na biashara ya madini.

Bila kusahau kutakuwa na mafunzo na utoaji wa elimu kwa wale wanaotaka kuingia kwenye biashara hii ya madini.

Nina imani kwakuwa na center kama hii ambayo itakuwa na website na mobile apps za watumiaji tutaweka biashara hii ya madini katika level nyingine kabisa ya kuaminika ndani na nje ya nchi.

Nimeamua kuiita center hii MADINI HUB kwa maana ndio kitakachokuwa kitovu cha shughuli zote za madini kupitia online.

Unaweza tembelea kuona website hii kupitia www.madinihub.com

Kwa mawasiliano zaidi 0677 818283

View attachment 1909060View attachment 1909061View attachment 1909062
 
Back
Top Bottom