Nahitaji ushauri wenu zaidi juu ya hili

,
sasa akisha 'sutwa' na kina Gea nini kitafuata? staili ya Gea kama itafaa kutumika kama ushahidi, basi sawa...
mimi nadhani cha muhimu ni kuhakikisha muhusika ananaswa kwa ajili ya kupata ushadi wa jinsi anavyomdhalilisha binti ili utumike dhidi yake. Atanaswaje ndio swali la msingi nadhani mleta uzi anataka majibu yake...

Kesi ikiwa na usimamizi na ufuatiliaji wa karibu polisi wanaogopa kuchakachua, hasa ukishirikisha vyombo vya habari au vituo vya msaada wa kisheria.

Hasaa hilo ndilo swali langu kuu, nitumie njia ipi kumnasa bila kupoteza ushahidi, wala kuleta madhara kwa namna moja ama nyingine. Huyu jamaa ana machafu mengi ambayo sijayataja hapa kwa jinsi anavyodhalilisha watoto hawa wa kike.
 
Gea ni police siku hizi??? Kha.

SL hii ni dalili dhahiri kuwa vyombo husika havifanyi kazi inavyopasa, matokea yake ndo haya watu kutafuta njia mbadala angalau na wao kujipatia relief na ndo utakuta watu wamechomwa moto au kupigwa tofauli hadi kufa huko mitaani.

BTW: uliwahi kuifuatilia 'kesi' ya mama mmoja amabaye mwanae wa miezi kadhaa alichukuliwa na baba yake na kwenda morogoro kukeketwa? that ordinary woman was something else aisee, polisi walitaka kumgeuzia kesi, subutu yao...she was smart enough kuwasiliana na vituo vya msaada wa kisheria na vyombo vya habari.
 
Aisee, inasikitisha sana bht kwa hapa tulipofikia, kila mtu amekazana gea gea...itasaidia nini sasa? Manake mbaba atasutwa na kisha ataachwa aendelee na tabia yake chafu ya kuwatumia vibaya mabinti wa watu, hivi kwani kusutwa kunabadilisha tabia ya mtu?

Sijawahi kufuatilia kisa cha huyo mama bt kwa maneo machache uloniambia inaonekana ana msimamo, hana woga na hayumbishwi na chochote, that is good. Napenda sana mtu asiye na WOGA, woga unawafanya watu wengi sana kupoteza haki zao za msingi... Inasikitisha kuona tz imefikia huku.
 
akina Gea mambo yote kwani wale wanakuwa na uthibitisho hivyo baada ya hapo ni polce kwa hatua zaidi
 
jamani kuna watu wakatili sana duniani asa huyo baba kama ni HIV positive maskini watoto wawatu jamani.........si anunue machangu wako kibao uko nje au atafute mtu mzima mwenzie atulie naye
pili hao watoto nao wanakosea utafanyaje kazi sehemu kuna mbaba tu mmama hayuko na hakuna mtu mwingine zaidi yako tu na huyo mbaba unatarajia nn mana ucku mrefu ujue jamani
 
  • Thanks
Reactions: BPM
Nyumba ninayoishi ni apartment ya family mbili, nimeishi nyumba hiyo kwa muda mrefu sasa. Mwezi wa kumi 2011 alihamia mpangaji mwenzangu ktk sehemu iliyokuwa imeachwa wazi na mtu ambaye alihama. Jirani huyu ni mwanaume na anaishi hapa bila mke ingawa mke anaye anadai mkewe huyo yuko mbali naye kwa sababu za kifamilia naye hapa yupo kikazi tu.

Toka alivyohamia hapa ninapoishi naye kama jirani kesha badili wasichana wa kazi za ndani wanne aliepo sasa ni wa tano. Msichana wa pili kabla hajaondoka alinifata na kunilalamikia tabia chafu za mbaba huyu za kumlazimsha amtimizie haja zake za zinaa, nikamshauri aondoke akatafute kazi sehemu nyingine. Jana msichana wa tano mwenye umri wa miaka 17 akiwa ana siku mbili tu alinifata na kunitolea malalamiko kama Dada na mwanamke mwenzie, kuwa mbaba yule anamlazimisha mapenzi kwa kumtisha na Bastola. Nilichomshauri binti huyo ni kwamba tutaweka mtego wa kumuadhirisha ili kuikomesha tabia yake chafu ya kuchezea watoto wadogo. Sasa ndugu zangu hapa ndipo ninapoomba msaada wa ushauri wenu nitumie polisi, majirani, ama mapaparazi?
kuna mawili hapo hao watoto wamekuja kwako kwakua wameshindwa kumhimili mshikaji moto wake ila akitokea atakaye mmudu utashangaa hata kuja kushtaki kwako anajikalia tu na ndio anajiolesha hapohapo mana kuna wadada wa kazi wako kikazi mara mbili wakipata sehemu kama hiyo wakiweza kuvumilia ndio wanakua washatoka kimaisha tayari
 
Aminata ni vitoto vidogo kwa umri na vyenye maumbo madogo ndivyo anavyopenda kuleta mbaba huyu toka huko vijijini, ni mmoja tu ndo walikubaliana na alikaa muda alipogundua kuwa anatamba mtaani akamtimua. hawa wengine wanakaa muda mfupi sana wanaamua kurudi kwao.
 
Tabia chafu sana, mpeleke polis nahis atakuja kutembe mpaka na mabinti zake.

Hao wasichana ni sawa na binti zake kwa umri alionao naweza kadiria 45+ nahisi ni mgonjwa si nyege mshindo tu zinazomsumbua.
 
Back
Top Bottom