Chauro
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 2,968
- 1,476
Naombeni ushauri wenu tafadhali.
Nina binti wa kazi ambae nimekaa nae kwa miaka mitatu,kwakweli ni binti mzuri sana mpaka nilifikia uamuzi wa kumpeleka shule.Lakini ghafla baada ya miezi michache nikamuona amebadilika nilikuwa nikimuuliza anasema yupo sawa na kazi anafanya kama kawaida.
\
kilichotokea jana kamuambia mdogo wangu ana mimba,nikamuomba mdogo wangu aendelee kuongea nae ....hiyo mimba ni ya nani kamueleza ni ya mwanafunzi mwenzake na akimpigia simu hapatikani.Alipomuhoji zaidi kamwambia ameongea na mama yake amemuambia atoe hiyo mimba kwakweli nimepata mshtuko.
nimejiuliza maswali mengi,napata wakati mgumu sana
1.Je nimuondoe nyumbani kwangu? lakini napata huruma ataenda wapi .kusema kweli naifahamu vizuri hali ya familia yake ni duni sana.Kumbuka mama ameshauri atoe
2.Niongee nae nimsaidie niendelee kukaa nae azae mtoto wake maana si support kutoa iyo mimba kwakweli namuona kama mdogo wangu.
Ushauri wenu ni wa muhimu sana, nakumbuka wakati nampeleka shule niliongea nae sana sijui aliona maneno yangu hayana maana huruma iliyoingia moyoni mwangu sijui niilezeje.
NAWATAKIA KAZI NJEMA.