Nahitaji ushauri kuhusu Mkopo wa kujenga nyumba

prado

JF-Expert Member
Feb 7, 2015
216
129
Habari wanaJF, nawapenda, nawakubali sana.

Najua humu kuna watu wa aina tofauti,na wamebarikiwa kitofauti, so every one's view is special and important to me!

Me ni jinsia ya 'KE' umri 24+ mwajiriwa serikalini, mshahara not less than mia5 Tshs, sina familia, bado naishi kwetu. Nataka nichukue mkopo wa kujenga nyumba itakayogharimu 50mil (kuna Uzi nimeona humu JF nikahamasika).

Kwa wale wenye uzoefu na masuala ya mikopo pamoja na makato sababu sina uzoefu na ndio kwanza nimeajiriwa,utaratibu ukoje?!

Halafu am not married nor engaged, is it a wise decision to make my own property au nisubiri nipate life partner ili tushirikiane vizuri katika suala la maendeleo?

Thanks.
 
Mkuu prado, maisha ni mipango. Kumbuka kupanga kabla ya kukopa ili uwe na sababu/lengo maalum. Ukiwa na lengo maalum na ukalitimiza kupitia mkopo,makato hayatakuuma kama kinyume chake. Kuhusu mali binafsi,waweza kumiliki mali binafsi ndani au nje ya ndoa kwakuwa Sheria ya Ndoa inaruhusu jambo hilo. Kikubwa ni kuhakikisha nyaraka zote zihusuzo kiwanja na nyumba zinakuwa kwa jina lako. Kila la kheri!
 
Last edited by a moderator:

Makato huwa wanakata Kama % ngapi ya mshahara?!
 
Mkuu prado, inategemea na benki husika pamoja na kiasi. Kila benki ina kiasi chake cha riba pamoja na kiwango cha kuweza kutolewa. Halafu,mikopo katika benki nyingi hapa Tanzania hulipwa katika kipindi cha miaka mitano ingawa makato ni ya kila mwezi. Hivyo basi,kwanza miaka mitano itakokotolewa kwenye miezi na kupata miezi 60.

Halafu, kiasi ulichokopa kitagawanywa kwa makato yaliyo sawa (kiasi ulichokopa pamoja na riba yake) katika miezi 60 halafu makato ya mwezi kupatikana. Kiasi husika kitategemea mshahara wako ili kujua ni asilimia yake ngapi Mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Maadam prado ushauri wangu kwako tafta biashara ya kufanya chukua mkopo invest kwenye hiyo biashara.

Faida utakayopata ndio uitumie kujenga nyumba, ki ukweli nyumba ya 50m ni sub standard nina uzoefu na nachokuambia sio mara moja au mara mbili.

Nyumba utakayojenga na kufurahi kuwa kwako kwa generation ya nyumba za siku hizi sio chini ya 100+m. Nakutakia kila la heri.
 
Last edited by a moderator:
Hongera binti kwa mawazo mazuri ya maendeleo. Unaweza kuanza tu kujenga nyumba yako hata akija huyo mwenzi wako mbeleni mtakuwa na pa kuanzia. Mikopo yote ni mibaya kutokana na riba, cha msingi angalia wenye riba ndogo. Ukikopa 50m ujue utalipa 80m almost mara mbili ya kile ulichokopa. so ni maamuzi yako mwenyewe
 
Aisee......
 
Kumbe....asante, ndicho nlchotaka kufahamu faida na changamoto za mikopo,since sina majukumu naweza kuamua kuchukua mkopo nyumba ikikamilika napangisha kwa mkoa nilipo kodi si chini ya mil2.5 kwa mwaka then nkaitumia Kama mtaji kufanya biashara itakayonisaidia kuendesha maisha ktk kipindi cha makato,how do you see this?!
 
Kiwanja unacho kwanza au huo mkopo na kununua kiwanja? Kama ndio umeajiriwa kwanza kaa mwaka mzima uone expenditure yako na surplus vikoje. Halafu inawezekana kati ya 15 na 20% ya mshahara wako kuondoka kila mwezi kwa muda wa miaka 3; inategemea na benki.

Halafu huo mshahara ni gross au net pay? Kama ni gross, ukitoa PAYE na NSSF waweza kukuta unabaki na net pay ya 3.3 million. Ukitoa na malipo ya mkopo kila mwezi karibu 600,000 - 900,000 utabakiwa na kama 2.4 - 2.7.

Usisubiri kuolewa ndio ujenge wewe anza tu sasa hivi.

Halafu kwenye huo umri ungeweka range mfano 24 - 35, badala ya 24+ yaani waweza kuwa na miaka 60. Kwani posting yako yaweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Asante sister
 
Mkopo ni mzuri kama unautumia kuzalisha, lakini hata kwa kujenga/kununua nyumba kama ulikuwa na huo mpango sio mbaya sanaa, lakini vitu vya msingi kwenye mkopo ni kujua riba yake, malipo yake kwa mwezi na utalipa kwa miezi mingapi(muda gani) na taarifa hizi utazipata bank unayoenda omba mkopo na linganisha hizo taarifa na mshara wako kwa mwezi utakuwa unapunguzwa kiasi gani pia hiyo kazi ina security ya kuwepo mda wote utakaotakiwa kulipa mkopo ili usije shindwa maliza mkia.
 
Maadam prado ushauri wangu kwako tafta biashara ya kufanya chukua mkopo invest kwenye hiyo biashara.

Faida utakayopata ndio uitumie kujenga nyumba, ki ukweli nyumba ya 50m ni sub standard nina uzoefu na nachokuambia sio mara moja au mara mbili.

Nyumba utakayojenga na kufurahi kuwa kwako kwa generation ya nyumba za siku hizi sio chini ya 100+m. Nakutakia kila la heri.

Umewahi jenga acha kukatisha tamaa watu,ujenzi wa nyumba inategemea place na place
 
Last edited by a moderator:
Habari wanaJF, nawapenda, nawakubali sana.

Najua humu kuna watu wa aina tofauti,na wamebarikiwa kitofauti, so every one's view is special and important to me!

Me ni jinsia ya 'KE' umri 24+ mwajiriwa serikalini, mshahara not less than mia5 Tshs, sina familia, bado naishi kwetu. Nataka nichukue mkopo wa kujenga nyumba itakayogharimu 50mil (kuna Uzi nimeona humu JF nikahamasika).

Kwa wale wenye uzoefu na masuala ya mikopo pamoja na makato sababu sina uzoefu na ndio kwanza nimeajiriwa,utaratibu ukoje?!

Halafu am not married nor engaged, is it a wise decision to make my own property au nisubiri nipate life partner ili tushirikiane vizuri katika suala la maendeleo?

Thanks.

Prado huo mshahara ni laki tano au mil 5?
 
Back
Top Bottom