Nahitaji Tissue Culture Banana

Nahitaji Tissue Culture Banana

saluti

Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
25
Reaction score
35
Habari Kiringeni.

Mimi ni mkulima wa mazao na mifugo tofauti tofauti. Nina mpango msimu huu kuanzisha kilimo cha migomba katika eneo la ekari 2.5. Nahitaji kufanya kilimo hiki kisasa (4th Generation Farming).

Kwa msaada ambaye ana taarifa zinakopatikana vipando (tissue culture) na gharama zake, ushauri pia unakaribishwa.

Nawasilisha.

Shalom Aleichem!
 
jaribu uende sua uulize wataalamu. uganda wanafanya hii kitu ila hapa migomba haijapewa kipaumbele. ukifanikiwa tunaomba utupe mrejesho.
 
Ahsante sana Mkuu nitakwenda SUA kuona kama wanazalisha na wana-commercialize.

Kwasababu tatizo Tafitishi nyingi Tanzania zinaishia kwenye makabrasha.

Wadau kiringeni naendelea subiri maoni yenu,

Naomba Kuwasilisha!!
 
Habari Kiringeni.

Mimi ni mkulima wa mazao na mifugo tofauti tofauti. Nina mpango msimu huu kuanzisha kilimo cha migomba katika eneo la ekari 2.5. Nahitaji kufanya kilimo hiki kisasa (4th Generation Farming).

Kwa msaada ambaye ana taarifa zinakopatikana vipando (tissue culture) na gharama zake, ushauri pia unakaribishwa.

Nawasilisha.

Shalom Aleichem!

Ndugu yangu
Nilifanya project kama hiyo 2013 kuotesha 3 heka migomba hapa Kisarawe na nilihangaika sana kupata tissue za banana, nilienda pale mwenge njia ya kwenda coca cola kuna kituo cha kilimo pale opp Nabaki africa nimesahau jina lake ila huwezi amini palivyochoka, labda ujaribu kama watakuwa wamejitambua..

Mwisho wa siku ilibidi ninunue migomba tu kwa hawa wauza miche barabarani
 
Aisee!!!

Tunahitaji kubadili fikra ili tujikwamue.

Katika Tafitishi zangu za chumbani(desk research) nimeng'amua hapa Dar maeneo ya Mikocheni kuna kituo cha kilimo-

Mikocheni Agricultural Research Institute nadhani ndicho unamaanisha mkuu!!

Nitajongea........
 
Maruku Agric Research Kagera wanafanya tissue culture
Unapanda wapi hiyo migomba na kwa nini unataka vipando vywa tissue culture
 
Mkuu nahitaji kuotesha Pwani.

Faida za vipando tishu tofauti na vipando jadi (suckers) ni:

*Hukua na kukomaa haraka.

*Stahimilivu kwa vimelea na Magonjwa.

*Hukomaa kwa pamoja (uniformity) Faida kibiashara.

Ahsante Dan,
 
Ndugu yangu
Nilifanya project kama hiyo 2013 kuotesha 3 heka migomba hapa Kisarawe na nilihangaika sana kupata tissue za banana, nilienda pale mwenge njia ya kwenda coca cola kuna kituo cha kilimo pale opp Nabaki africa nimesahau jina lake ila huwezi amini palivyochoka, labda ujaribu kama watakuwa wamejitambua..

Mwisho wa siku ilibidi ninunue migomba tu kwa hawa wauza miche barabarani
jubilant + saluti

Hii Taasisi siku hizi ipo vizuri sana, wanaweza kukusaidi walau ni wapi unaweza kupata hivyo vipandio...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nahitaji kuotesha Pwani.

Faida za vipando tishu tofauti na vipando jadi (suckers) ni:

*Hukua na kukomaa haraka.

*Stahimilivu kwa vimelea na Magonjwa.

*Hukomaa kwa pamoja (uniformity) Faida kibiashara.

Ahsante Dan,

Jaribu Kuwasiliana na wizara ya Kilimo kitengo cha Utafiti uulizie kama bado Maruku bado wanazalisha tissue culture
But all in all you don't have struggle for tissue culture any clean planting materials can do, good thing ukanda wa pwani hakuna Bxw, wala Radopholus similis ambao ni kikwako kikubwa na hence the need of tissue culture
 
Mkuu nahitaji kuotesha Pwani.

Faida za vipando tishu tofauti na vipando jadi (suckers) ni:

*Hukua na kukomaa haraka.

*Stahimilivu kwa vimelea na Magonjwa.

*Hukomaa kwa pamoja (uniformity) Faida kibiashara.

Ahsante Dan,
pia kama unapanda shamba kubwa hii ni njia nzuri. sababu kwa ekari zako 2.5 ni kama migomba 2000 ambayo si rahisi kupata kwa kununua.
 
Hakika Giant!!

kama vile upo kwenye fikra zangu.

Kibiashara lazima uwe na lengo la kuwa na ugavi unaokidhi mahitaji ya soko.

Kwa vipando jadi -leo umevuna mkungu mmoja kesho miwili mpaka wiki nyingine. Kwa kweli haina tija kiuchumi!!

Bado vipando tishu ni chaguo mosi.Hakika!!
 
habari zenu,
mimi binafsi nilianza project hiyo mwaka jana,nlifika pale kituoni kwao mikocheni ,nilitoa order ya miche ya awali kama 1000 hivi,nikaambiwa nisubiri miezi sita itakuwa tayari,nikajipanga na pesa ambapo walisema mche mmoja ni Tshs 3000...nilikuwa nafanya ufuatiliaji wa hapa na pale kwa njia ya simu,baada ya miezi 3 nilienda kuona wamefikia wapi nikaambiwa ile miche iliuzwa(iliuzwaje uzwaje wakati nilitoa order na wakakubali,hawakunipa maelezo yakujitosheleza)...nikaambiwa nisubiri miezi mitatu mingine nikasubiri ,nikapewa miche 125 tu ambayo ilikuwa aina mchanganyiko(mimi nilitaka mzuzu tupu) lakini waliniahidi katika zile aina hakuna bokoboko...nikaichukua nikaipanda,(nilipanda january 2013)...sasa imeshazaaa,imestawi vizuri ila katika miche 125 ,75 ilikuwa bokoboko....na imestawi vizuri,je bokoboko hapa mjini dar namuuzia nani?inatia hasira saaana(nimeifyeka machipukizi yake yote na nikivuna nang'oa hayo mashina yote,sitaki kuiskia bokoboko,hata mimi binafsi tu sili ile ndizi)
Sikuishia hapo,mwaka huo 2013 nilifika sua,nikaongea na professor Msogoya,alinishauri vizuri yule baba...na akaniambia sua hamna tissue culture ila kuna njia fulani wanatumia pale,wanatreat vile viazi(kama kiini flani cha mgomba) wanaua wadudu halafu wanazalishia miche,nikatoa order yangu,nayo ilichukua miezi sita kupata miche 500 tu,(ila safari hii nilipata na yote ilikuwa mzuzu)...nimetoa nyingine ya 500...nachukua ndani ya miezi 3...bei ni ile ile 3000tsh kwa mche!
natarajia kuwa nahamisha machipukizi kutoka yale mashina ya mwanzo mpaka nijaze ekari zangu 10.
kitu kingine nilichojifunza,machipukizi yanakuwa haraka sana kuliko tissue culture plants na hii miche mingine ya kuotesha nayonunua.
Kingine cha kuongeza sua kuna foleni ya miche,toa order yako mapema,na miche inapatikana kwa wingi wakati wa kiangazi,kama una irrigation system nakushauri uchukue wakati huo...wakati kilimo ukianza ni purukushani unaweza usikute mche hata mmoja.
Kuna mtu alinidokeza kuna mtu ana lab Arusha,yeye alimuona kwenye maonesho fulani ya kilimo,huyo mtu anafanya large scale production ya tissue culture plants,hata miche 3000 unapata in one go,lakini hakuwa na namba ya huyo mtu,nimeulizia sana kuhusu huyo mtu mwenye lab sijampata(labda hayupo lol)...ila nimeshachoka kumtafuta,ntaendelea kusubiri sua.
other than that,kila la kheri!
 
Superb!! what a worth infos.....

Thanks mkuu pamoja sana katika ujenzi wa Taifa,

Nitayafanyia kazi mawazo, ushauri wenu Ahsante!!
 
Mkuu andishi lako la 2014, sasa ni 2020 hakuna mabadiriko...nina shida sana ya hii miche, hadi nimeona sijuhi niende nchi jirani ila naogopa utaratifu wa kufuattlia vibari. Nimejaribu kwenye mtandao kuona kama naweza kuanzisha maabara yangu binafsi huku nikiajiri mtaalam kutoka SUA ila ndio hivyo tena unaweza kuta wahitimu walisoma kujibia mitihani na kwenye field vichwani watupu!
 
Mkuu nimesikitika sana kuona unasubiri miche ya tushu miaka 4.Hivi ungekuwa umepanda miche yetu ya basil sitayari ungekuwa upo mbali? Hivi unejiaminisha kabisa migomba yetu ya asili ni mibaya? Mbona ndizi zetu zinazaa vizuri tu kama utatunza vizuri!
Tuache exageration ya mambo.
 
Watanzania wanamihemko sana na vitu vya kigeni ilhali vyetu hatujaviboresha.Kuna mbegu moja ya mahindi nilipewa nikaipanda aisee! Nikahitimisha kuwa watanzania tunakurupuka sana Mbegu inazaa vizuri,mahindi makubwa, magumu hayabunguliwi kama ya kisasa,pumba sio nyingi .kuna mbegu bora za asili ila watu wamekariri vya ulaya.Nenda mbeya Kaone mikungu ya matoke ilivomikubwa.
 
Mkuu nimesikitika sana kuona unasubiri miche ya tushu miaka 4.Hivi ungekuwa umepanda miche yetu ya basil sitayari ungekuwa upo mbali? Hivi unejiaminisha kabisa migomba yetu ya asili ni mibaya? Mbona ndizi zetu zinazaa vizuri tu kama utatunza vizuri!
Tuache exageration ya mambo.
Migomba yetu siyo mibaya ila ina magonjwa yanayienea kwa kasi kama mnyauko nk.
 
Back
Top Bottom