Nahitaji Msaada Wenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji Msaada Wenu!

Discussion in 'JF Doctor' started by Calcia, Jun 27, 2012.

 1. C

  Calcia New Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitumia dawa za Malaria aina ya Co-Malafin,nilitumia siku tatu,baada ya hapo,siwezi kukaa juani au sehemu yoyote ile yenye joto!yaani Mwili unachomachoma mpaka vinatokea vipele na vinauma sana,sasa inabidi nitafute baridi au maji nijipakepake au kivuli,nikishafanya hivyo mwili unarudi ktk hali yake ya kawaida na vipele vinapotea,sasa niliamua kurudi hospitali wakanambia ni sumu ya hizo dawa!basi wakanipa dawa za kutoa hiyo,lakini bado,nikarudi tena wakanipa dawa zingine nikatumia lakini wapi,nikarudi kupima damu wakakuta kuna malaria na typhoid nikapewa dawa na ikabidi niombe sindano sababu nimekunywa dawa mpaka nkapata vidonda tumboni,dr akaniandikia sindano,za malaria na Allerge nikamaliza lakini hakuna mabadiliko yoyote!yaani kutoka nje mimi usiku au asubuhi sana kabla ya jua,napata shida sana!nashindwa fanya kazi sababu joto na mimi ni sawa na paka na panya,yaani mimi na kivuli, kivuli na mimi!hata ktk daladala siwezi panda ka watu wamejaa!inabidi nipate siti yenye dirisha ili niliache wazi!sasa naombeni msaada wenu ili niweze pona!naamini ntapata ufumbuzi toka kwenu!nahitaji sn msaada wenu! by Calcia.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ninakushauri uende kwenye Hospitali Kuu ya Muhimbili ukaonane na Ma Daktari Mabingwa kuhusu hayo Matatizo uliyonayo. Sijuwi hivi sasa hao Ma Daktrari kama utawakuta? maana kuna mgomo huko nyumbani wa Madaktari. Pole sana mkuu.

  Au jaribu Dawa yangu ya Tiba Mbadala ya Malaria :

  Jaribu kutumia dawa yangu hii Pata kijiko kimoja cha Asali Safi mbichi ya nyuki uchanganye na kijiko kimoja cha Siki ya Apple(Applle Vinegar) au Siki ya Zabibu uwe unakunywa asubuhi kila siku kabla kula kitu Tumia hii Dawa kwa muda wa mwezi Mmoja itakusaidia kuondosha hiyo Malaria yako Sugu.

  Au Tumia Dawa hii Pata ndimu30 uzikamuwe uzitie kwenye chupa moja kisha hiyo chupa uiweke kwenye jua siku 3 baada ya siku 3 uanze kutumia kila siku unywe kipimo cha kikombe cha kahawa Asubuhi kabla ya kula kitu mpaka umalize hiyo chupa utakuwa umeshapona, kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu inshallah. Jaribu kutumia moja kati ya hizi dawa.

  Tumia kisha unipe maelezo yake umefikia wapi ?
  Pleae Give me a feedback.@Calcia
   
 3. C

  Calcia New Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa maelekezo yako!kwahiyo una maanisha hii hali niliyonayo ni malaria sugu?
   
 4. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Pole. Hospitali kwa kawaida wanatoa tu dawa za kutuliza tatizo na siyo kutibu tatizo, angalia walikupa wenyewe hizo dawa za malaria, zimekudhuru wanadai una sumu zilizotokana na hizo dawa za malaria na wanaamua kukupa dawa zingine za kuondoa hiyo sumu. Sasa kwanini hawakukuambia mwanzo wanapokupa dawa za malalria kuwa hizi siyo dawa bali ni SUMU?.

  Nahisi umepungukiwa maji mwilini mwako kwa kiasi kikubwa. Bonyeza link ifuatayo usome namna unaweza kutumia maji: http://maajabuyamaji.net/new-page/jitibu-kwa-kutumia-maji/
   
 5. M

  Mshiloni Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana,nakushauri kama unaweza nenda hospitali ya Wasabato inatazama na hindu mandal hospital.
   
 6. C

  Calcia New Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana!nawashukuru sana!ila tatizo mie nipo Iringa,asa hiyo hospitali ya wasabato sijui ka ipo huku Iringa.
   
Loading...