Nahitaji msaada wenu hali yangu ni mbaya

Nitalala hata chini lakini sio kwenda kumuongezea mzigo mama yangu aliyenilea kwa tabu hatahivyo sikatai hali ikiwa mbaya zaidi nitarudi wacha nipambane kwanza. Asanteni kwa wote mnaonishauri na kunipa pole
 
Kwani unafamilia au una mke anakutegemea mana kama upo mwenyew mimi sioni kama kuna tatizo lolote dili zipo kibao kitaani endelea kufany uku ukiendekea kutafuta ajira nyingine
 
pole! unasema ulikuwa mwajiriwa siyo napenda kujua pensheni yako vipi, fuatilia nadhani utapata mwanzo ujiajiri!
sikuhizi kazi hakuna na ukipata ni stress tupu!
kaa chini ujipange huo ndio ukubwa na si lazima ukae dar tu
 
Mkuu nilishaapa sitakuja kuingia darasani tena baada ya kuhitimu haka kadegree niliko fanikiwa kukapata!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] najua sana ndo maana nilikuchokoza tu,vipi kwa sasa unapanga foleni atm au bado upo na bahasha ya kaki
 
Haya makosa Mungu aniepushe nayo kwa kweli. Mwaka huu naomba sana Mungu aniwezeshe kukamilisha mabanda nianze ufugaji wa kuku, mbuzi na ng'ombe. Kuajiriwa taabu sana. Ee Mwenyezi Mungu nisaidie mja wako!
 
Mkuu, nimepata suluhisho la kinacho kusibu. Na nilikua ninamsimulia jamaa flani kisa chako hapa bar.... Naomba kesho asubuhi unitumie namba yako ya simu kwa pm, then nitakuunganisha na mkuu aone vyenye atakusaidia kazi ya kufanya kwa shirika lao, ngawa mshara ameniambia utakua ni kati ya 500/700 elfu.
Naomba sana unitumie nambayako mapema ili tuone namna ya kuibaka hiyo nafasi yaku volunteer.
Nami nitakutwangia kilongalonga ili nijue kila kitakachojiri.
 
Bazazi@work
 
Me nataka kujua tu je unatafuta kazi ya ofisini peke yake au kazi yoyote ambayo utaweza kuingiza kipato na upo tayari kupokea kiasi gani kwa mwezi??kuna sehemu zongine inabidi kuweka degree na uzoefu pembeni then unaangalia namna ya kufight kimapato ni muhimu sana nadhani.....shamba je unaweza kukaa na kuangalia mifugo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…