Nahitaji msaada wa vitabu James Chardley Chase

BABA-D

JF-Expert Member
Jul 23, 2015
1,216
996
Kwa unyenyekevu mkubwa naomba msaada wa namna ya kupata vitabu vya JAMES HARDLEY JAMES. Naomba pia kama kuna link za vitabu vya MUSIBA kama KIKOSI CHA KISASI, NJAMA, DAR-ES-SALAAM USIKU, KIKOMO, n.k
 
Kwa unyenyekevu mkubwa naomba msaada wa namna ya kupata vitabu vya JAMES HARDLEY JAMES. Naomba pia kama kuna link za vitabu vya MUSIBA kama KIKOSI CHA KISASI, NJAMA, DAR-ES-SALAAM USIKU, KIKOMO, n.k
Kama unahitaji vitabu vya James Hadley Chase (siyo James Hardley James) vinavyoshikika na kama uko Dar nenda mtaa wa Samora kwa wauzaji wa vitabu walio sehemu nyingi tu mtaa huo kwa nje na pia maduka ya vitabu mtaa huo huo utavipata vipo vya kumwaga na vipya kabisa.

Kuhusu hivyo vingine vya Aristabrus Elvis Musiba kama Kufa na Kupona, Njama, Kikosi cha kisasi, Kikomo, Hofu na vinginevyo naamini jasho litakutoka kabla haujavipata. Mimi baada ya kuvitafuta kwa miaka mingi nilibahatisha kimoja tu cha Hofu hadi nilishajikatia tamaa.

Binafsi bado navitafuta hivyo vitabu vya Musiba ikiwa ni pamoja na vya watunzi wengine kama Bado Mmoja, Tatizo la Kisauni (mtunzi akiwa ni Sospeter J. Chadhoro kutoka Kenya), Pete (Kezirahabi), Mtu ni Utu (George Mhina), Kizazi Hiki (W. E. Mkufya), Dunia Hadaa (Eddie Ganzel?), Ama Zao Ama Zangu (Hammie Rajabu) na Hadithi za Esopo (Chuo cha Kwanza cha Kusomea n.k.)
 
Back
Top Bottom