Nahitaji msaada wa mawazo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji msaada wa mawazo.

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by sweetlady, Dec 27, 2010.

 1. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Habari wana jamii wenzangu. Nimeolewa, kabla sijapatwa na mkasa ninaotaka kuwaeleza nilikuwa namuamini sana mume wangu. Mwaka jana mwezi wa 6 nikagundua kuwa ana mwanamke (mama mtu mzima ) Kuanzia hapo moyo wangu umekuwa mgumu sana kumwamini ingawaje tulishayaongea na alikiri na kuniomba sana msamaha ila kuna wakati kumbukumbu zinanijia na ghafla najikuta namchukia mno. Niasaidieni cha kufanya coz nahisi nimeathiriwa na tukio kwa kiasi kikubwa sana. Imefikia mahali sifurahii tena tendo la ndoa na kuna wakati naweza kumnyima hata mwezi mzima. Kabla ilikuwa tunashirikiana vizuri tu ila kwa sasa nipo nipo tu. Huwa najiuliza je kama niliweza kumtimizia kila kitu kama mume na bado akanisaliti kwa nini niendelee wakati nmeshagundua kuwa hatosheki? Kweli naishi nae basi tu ila moyoni kwangu hayupo kabisa. Nilishamwomba tuachane kwa upendo akakataa eti tutamwathiri mtoto, eti bado ananipenda ni shetani tu alimpitia na hatampitia tena. Anachonikera zaidi ameanzisha tabia ya kunichunga kama mbuzi, hata nikienda saluni siondoki mpaka aje kunichukua, madai yake eti anaogopa nitamlipizia. Nikiwa kazini cm masaa yote na anafika kunichukua dakika 5 kabla ya muda wa kazi kuisha. Nisaidieni wajameni coz kweli sina upendo na huyu mtu. Hilo jimama alishaliacha na viapo tele kuwa hatarudia tena. MOYO MGUMU KUSAMEHE! NIFANYEJE???
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sweety pole sana. Hebu jaribu kufikiria kama wewe shetani amekuningilia ukammgea X wako au class mate wako enzi hizo mkicheza cheza.

  Halafu huoni jamaa yako ni mwungwana sana ? Sisi wanaume hatukubali kama tumemega hata kama umeshikwa live . Huyo wa kwako ni exception otherwise inawezekana kakudanyanga ili upate wivu zaidi. Anakufuata kazini, cm kibao, saloon darling ,darling......... halafu unaona kinyaa? Anakupenda, to put story very short.
   
 3. Double X

  Double X Senior Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ni vizuri kumpa nafasi tena, na uruhusu moyo wako kwa dhati kabisa kusamehe, GIVE HIM ANOTHER CHANCE.....!!
   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Muhimu hapo ni kuokoa ndoa yenu.
  Tumia nguvu zako zote na busara zako zote umsamehe, yaishe, halafu rejesha mapenzi yako kwake, zidisha kuliko zamani. Yaani hapo, ni kwamba unamdhibiti kwa kumwonyesha mapenzi zaidi badala ya kumchunga au kumchunguza (si ajabu kumchunguza kwako ndiko kulikopelekea maumivu ya kufahamu ukweli). Pia ni vizuri ukatathmini sana ni kitu gani kilipelekea yeye kuanza kutembea nje.

  Kupunguza mapenzi na hisia zako kwake, hakuna tija kabisa, kunapelekea yeye kuzidi kujishuku na kukosa amani na baadaye anaweza kuendelea kulamba nje tena.
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Msamehe ...sidhani kama anaweza kufanya ujinga tena!
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante ndugu yangu, ni kweli baada ya kumgundua aliniweka wazi kila kitu mpaka mara ngapi ameduu na huyo mama ila kinachonifanya niwe mgumu kumsamehe ni kwamba by the time nagundua uhusiano wao huyo mama alikuwa na mtoto mchanga nikamwuliza na mtoto ni wako? Akajibu ndiyo, ila hana uhakika coz mama mwenyewe yupo single na anamegwa na kila mtu. nikamwambia sasa kwa nini unasema mtoto ni wako akajib eti jimama ndo linemiambia ni wangu. HAPO NDO AKANIWUWA KABISA!!! KUMBE HATA SEX ALIYOFANYA SI SALAMA KIASI HICHO? AKADAI ETI SIKUTUMIA KINGA MARA MOJA TU? SASA HEBU NIAMBIE KAMA NI WEWE UNGEMWELEWAJE??
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hii post ungeiweka kwenye Jukwaa la Mahusiano na Urafiki ungepata twice the responce waombe Mods wakusaidie kuihamisha...
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Simchungi na sijawahi kumchunga coz nilikuwa namwamini sana. Yeye ndiye anayenichunga kwa sasa. Hata habari za kucheat sikuzipata kwa kumchunguza. Alikuja tu msamaria mwema akanipa habari kwa ufupi then nikamuuliza akakubali bila kupinga na kuomba msamaha kuwa hatorudia tena. Kweli nimemsamehe usoni ila moyoni nashindwa kabisa kumsamehe na ninajitahidi sana hiyo hali iondoke ila baada ya siku kadhaa inarudi tena.
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  It appears na wewe una jamaa nje ndo maana unamuona anakughasi kwa kukupeleka saloon etc na kukupigia cmu. Maana si bure. Kama ni msamaha amekuomba, anakufata office on time, saloon anakupeleka etc. What do caring and love mean to you. Mwisho wa siku What do women want after all those carings/love from your lovely ones? To me it sounds huyo jamaa amejirudi sana, and that means kama alikua anachelewa nyumbani sasa hv mnaenda wote. Mnataka nini nyie wanawake? Mkipendwa kosa, mkitukosea - tukateleza na cheat nje kosa.......
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sina na wala sijawahi kuwa nae tangu tufunge pingu za maisha! Sasa kwa nini aanze kunichunga baada ya kumfumania? Hakuwa hivyo kabla. Unajua nikimuuliza anatoa sababu gani? Eti anahisi na mimi naweza kumsaliti wewe unafikiri hiyo ni sawa? kumchunga mwenzi wako baada ya kumtenda?
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  NI ngumu kweli . Ukimwacha atahamia kwa jimama na ndio mwisho wa hii stori. Bila shaka utaumia zaidi ukimkuta ndio baba watoto kadhaa wa jimama. La msingi ni kusamehe yaishe mjenge familia.
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole mumie nipigie nikupe ushauri zaid na kukupunguzia mawazo.
   
 13. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pole sana SweetLady... Kama inawezekana msamehe.. Kibiblia tunatakiwa tusameheane saba mara sabini... Na ni kosa kubwa sana kumnyima mwenzio.. Isije ikawa ndio sababu ya kwenda tena nje. Yaliyopita si ndwele... Ganga yanayokuja.. Kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa.. Msamehe Mwaya mlee watoto...
   
 14. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nyeeeeee!:A S-heart-2::A S-heart-2:
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Thanx again ntaendelea kujitahidi mpaka niweze! Ila sijuti kabisa hata nikisikia kahamia kwa jimama. Huwezi amini nipo nae kwa heshima ya mwanangu tu na si vinginevyo. Nampenda sana mtoto wangu na kinachoniuma anampenda sana baba yake so nasikia huruma kumtenganisha nae.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Pole sweetlady.
  Msamehe huyo mr kwa moyo mmoja na usifikirie kurevenge.
  Tunawaamini sana wanaume wetu lakini ukweli ni kwamba wanatusaliti kama sio sana kidogo.
  Ukiwa ndani ya ndoa unaweza ukaona ni ajabu kusalitiwa ila sisi tulio nje tunaona jinsi gani wanaume waliooa wanavyohangaika nje.
  Shukuru kama mshkaji bado anakujali na kukuthamini. Ingekuwa ushaanza kula kipondo ningekushauri ukimbie.
  Msamehe kwa kweli na mtoto akapimwe DNA. Kama wa kwake we lea.
   
 17. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sweetlady msamehe huyo jamaa kwani umeshajua tatizo na amekiri kukosea, hivyo mpokee kama mtu mpya tena na hakika atakuwa mpya. Inawezekana kabisa lile linaloisha likawa ni dogo zaidi ya lile linalokuja, vumilia ili usiingie kwenye mkasa mwingine ambao unaweza kuwa ni zaidi ya huu, dunia inazunguka mama. Jamaa anakupenda nawe mpende tena na rudisha moyo wako kwake na mtashikamana kama mwanzo na hatatamani inje tena.
   
 18. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Naona bibie keshakinai. tatizo mapenzi yakihama yanahama kweli. Huo ushauri hauingii tena. kurudia upendo wa zamani si rahisi jamani. ebu mwanamme fikiria umemkuta mkeo anamegwa, halafu akakuomba radhi, will you really afford her the same love as before? No way! Kibinadamu haiwezekani bali kwa Mungu yote yanawezekana. Nakushauri mwombe Mungu akuondolee uchungu huo yote yawe mapya. Otherwise shit has just hit the fan!
   
 19. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  pole sana mpz,kujikwaa si kuanguka,najua kuna wengi sana wanacheat na hawakubali kosa,tena unaweza kuwakuta red handed bado akasema"it wasnt me"kama umeamua kusamehe basi samehe na kusahau kabisa maana kama hujasahau huo ni unafki tena unapata dhambi(am not judging)unapomnyima unampa ham ya kurudi nyuma,songa mbele dada,fanya jema na wajibu wako kama mwanamke Mungu atakulipia uliapa kwa shida na raha so its beta ukashinda majaribu,lkn mwambie Mungu shida zako maana yy ndie aliemuumba,muombe amfinyange upya na kumrekebisha.
   
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sijasahau na ndiyo maana ninaomba ushauri. Inauma wewe usiombe ya kukute. Nahisi ni kwa sababu nilimwamini sana Mr. sikuwahi kumdhania. Kila siku story zake zilikuwa wife unajua kuna ukimwi? Ndiyo mme wangu, Ok basi tujiepushe na vishawishi then at the end of the day unamfumania!
   
Loading...