pole sana mkuu...![emoji18]
kwanza nakupongeza kwa kuonesha nia ya kuachana na homosexual..
Pili usijickie wa tofauti sana kuhusu kushindwa kujenga mazungumzo na wadada.
Hata madomo zege ambao huo mchezo hawajawahi kuucheza wapo pia,
Napenda nikushauri jambo moja kwanza,
Kabla ya kuanzisha mahusiano na binti yeyote.. Anza kutengeneza mazingira ya kuwazoea wadada,
Tengeneza marafiki wengi iwezekanavyo ambao mtakuwa mnabadilishana mawazo mara kwa mara,
Ukishakuwa na marafiki wengi wa kike hapo hautakuwa na woga wa kuzungumza na msichana tena.
Suala la mahusiano litakuja lenyewe tu, wala hata hautatumia nguvu nyingi.. Utakuwa una uhuru wakueleza hisia zako kirahisi kuliko saivi.
Nakutakia sikukuu njema..