Nahitaji msaada wa kiroho

Nashukuru ndugu ila naona kama jamii imenitenga ninapofanyia kazi imenitenga hata zuri linageuzwa kuwa baya,sina tena ujasiri wa kuthubutu kama ilivyokuwa awali ndg
 
Upo katika kipindi cha mapito (karma)
Zama ndani sali na make peace with your past. Fanya matendo mema, mtafute Mungu zaidi whatever that means to you. Linda hisia zako, imarisha akili yako, roho yako mbwagie Mwenyezi Mungu
Utazaliwa upya hakika ukifanikiwa kupita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Ctr
Nafahamu napitia katika kipindi kigumu, ushauri wako nitaufanyia kazii, nashukuru kwa kunitia moyo ndg
 
Pole sana ndugu. Matatizo kaumbiwa binadamu watu tunapita ktk wakati mgumu ila tunatofautiana viwango vya mapito tu.

Mpaka maroho hayo yanakufutilia hivyo ujue sio bahati mbaya kuna kitu juu yako ambacho ni cha kipekee wamekiona (mfano bwana yesu pia kipindi anazaliwa akiwa kama binadamu nyota yake iling'aa sana ikapelekea mama jusi kutoka mashariki ya mbali yaani japan, uchina huko (wachawi hawa kufuatilia nyota hiyo hatujui pengine walitaka kwenda kuiiba bahati mbaya wakajikuta wapo kwa yesu badala ya kuiba nyota wakatoa wao zawadi (manemane na dhahabu).

kwa hiyo watu wabaya wanaweza kusoma feature yako na wakatambua ww unaweza kuwa nani au kuwa wapi hapo badae. Na hapo ndipo wanapokuwinda ili waibebe nyota yako (wakuaribie maisha yako)

Nikutie moyo unayopitia yanaweza kuwa ni matatizo ya kiroho baadhi ya spirits zinakufuatilia isee au ni ugonjwa pia yote yanawezekana.

Ila anza kushughulika na utatuzi wa kiroho naamini utafanikiwa.

Tafuta viongozi wa dini na wakiroho km wadau walivyoshauri watakuombea na utafanikiwa hakika.
 
Hilo
Hilo nyota yawezekana likawa na ukweli maana nilikutana na mtu mmoja akanambia mbona naona kama nyota yako wamechukua? ukiangalia kila mahali ninapokwenda watu wamekuwa wananichukia bila sababu mtu hujagombana nae lakini basi,mwingine anakucheka na kukuona kama mwendawazimu
 
Kwa maelezo yako inawezeakana una tatizo la kisaikolojia "paranoia" jaribu kuwaona wataalam
 
Reactions: Ctr
0

Pole sana.. hasa majini, wachawi na waganga ndio tabia zao hizo ukusanya nyota zile safii za zenye kila aina ya mafanikio (kibiashara, kisiasa, kimasomo, kimvuto na n. k) na kuziweka stoo (spiritual) then wateja wanapoenda (wale wasaka maisha kwa njia za shortcuts... Wanasiasa, wafanyabiashara na n. k) ndio upewa hizo nyota kwa mashart ya kafara mbalimbali na anayefanya vizuri upewa nyota nzuri zaidi.

Wewe huku unakuwa upoupo tu km haupo maan mwelekeo wako wamesha ubeba, unaoneka kituko tu.

Binadamu wabaya sana.
 
Pole sana ndg ila tatizo lako ni dogo sana, kuna watu walikuwa na mattzo makubwa zaidi ya yakwako pale kanisani kwetu, kuna baadhi ya mabinti walikuwa ni wachawi, Uchawi wa kuunganishwa kutoka kuzimu moja kwa moja, mwngne binti wa miaka 12 alikuwa anauwezo wa kuangalia jua la saa sita na likawa kama la saa 11, kiufup shuhuda ni nyingi nyingi sana ambaz ukizisikia lako hautaliona kuwa ni tatizo..!!
Njoo Kanisani POWER OF GOD FIRE CHURCH- Dar, Chanika kituo cha sheratoni..!! Njoo uombewe, uokoke, Ufundishwe kiroho, upokee nguvu ya Roh mtakatifu na moto...! Uone kama watadhubutu kukusogelea tena,!! Namb ya Askofu 0753 230680 na 0672 606508..MUNGU AKUTANGULIE UVISHINDE VITA HIVYO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: Ctr
Tatizo Hilo ni dogo Yesu anaweza mwamini tu. Utaokoka msiba wako utaisha. Onyo acha kwenda kwa mitume na manabii wengi wapiga dili watakuunganisha na madhabahu za kishetani utapotea zaidi. Hapo ulipo anza kuomba then muombe Mungu akutangulie wapi utaombewa.
 
Ndio hivyo aisee,Sasa najiuliza kuna uwezekano wa kuirudisha mkuu
 
Asante ndg nimeupokea ushauri wako
 
Ndio hivyo aisee,Sasa najiuliza kuna uwezekano wa kuirudisha mkuu
Ndio inaweza kurudi hayo ni mambo ya kiroho urudishwa kiroho pia si vinginevyo.

kitendo tu cha wewe kuanza kuitaji msaada wa kiroho teyari Mungu anataka akurudishie kile jilicho potea kwako.

Mimi sina kanisa au msikiti wa kukwambia uende ila hakikisha unatafuta Viongozi wa kiroho mungu akuongoze uweze kutimiza itaji la moyo wako.
Ameen.
 
Reactions: Ctr
Asante ndg nimeupokea ushauri wako
Biblia takatifu kitabu cha Isaya 42:22 kinasema " Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha".
Ukisoma vzr utaelewa, Mtu yeyote ni mtu wa Mungu kwa maana Ameumbwa naye (mwanzo 1:26).. Umefika mwsho sasa wa umateka wako, ipo Nguvu ya MUNGU hisiyo na Gharama inayopatikana bure bila masharti ambayo inaweza kukuvusha, Achana na Waganga, sijui dua, kisomo huko kote unapotea.. We fata ushauri niliokupa Hautakaa uujutie kamwe.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
shukrani ndg
 
Unanichanganya sana katika maongozi yako, mara hao hao ndugu zako wako bega kwa bega na wewe na wanakwenda mpkaa kwa waganga hapo hapo unasema hao ndugu zako wana imani kubwa, sasa mtu mwemye imani inakuaje waende kwa waganga tena kama sio imani haba hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usitafute msaada maana huto pata popote pale, tafuta wokovu kwanza mengine utazidishiwa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…