Nahitaji msaada wa kifedha, nimekwama

Samahani mkuu, umenena jambo jema saba! Kama kuna walau nafasi ya uhasibu mahali hapo waweza kuniunganisha mkuu! Uaminifu ndio nguzo ya maisha yangu...!!! Nisamehe tena..kwa kwenda nje ya mada.
Regards.
Its a teaching role, Maths O-level, if you are comfortable with maths, let me know.
 
mkuu naelewa sana unachokizumgumzia,nashukuru sana kwa ushauri wako!
mkuu back up plan ninayo na pia kuhusu huyo atakayenipa mkopo huo nataka niongee nae tuone ananipa kwa riba kiasi gani na kila baada ya muda gani au ananikopesha/kunipa pesa kwa misingi ipi na ipi! mkuu naelewa sana mambo ya risk na calculated risk! nahitaji kuaminika katika hili! japo naelea business inakuwaga na milima na mabonde ila kulipa mkopo ni lazima by any means!
kuhusu kama nimesoma Mathematics bahati mbaya kaka sijasoma hiyo, nimesoma HGL lakin hata kama itapatikana kazi itakayonifaa kwa masomo yangu hayo na uhasibu chuo japo sikumaliza nitashukuru sana kama utaniunganisha au kunipatia!
 
Its a teaching role, Maths O-level, if you are comfortable with maths, let me know.
Nimekupata vema mkuu! Ingawa nilifanya vizuri kwa kupata highest grade as long as mathematics is regarded o-level...ila sikusoma pure maths high school! Thus, sina hakika sana kama naweza kufundisha maths kwa sasa kwa kuwa ni miaja kadhaa imepita tangu ni-solve ...labda hesabu za fedha tu..ndio ninazojua(accounting)...shukrani sana mkuu.
 

Sorry, ni nafasi ya Maths, teaching.
 
Bwana Hamis pole sana kama unayosema ni kweli, ni wengi tumeyapitia maisha kama yako, tulivumilia tukavuka. Jipe moyo Mungu atafungua milango, japo shida yako ni Pesa hata ushauri ni muhim zaidi ya Pesa unazotaka. Nitakufuata Pm
 
Bwana Hamis pole sana kama unayosema ni kweli, ni wengi tumeyapitia maisha kama yako, tulivumilia tukavuka. Jipe moyo Mungu atafungua milango, japo shida yako ni Pesa hata ushauri ni muhim zaidi ya Pesa unazotaka. Nitakufuata Pm
sawa mkuu nashukuru na nakusubir PM
 
Kubeba zege nyinyi si mchezo. Wengine wana maradhi au vilema vya kudumu vinavyoweza kuwa kikwazo. Ni vema kujua uwezo wake kama anaweza kazi ngumu.
 
Mkuu kazi ya kumpa sina wala sitaki kumpa tamaa lakini hio hesabu niliompa, kama kweli anataka mafanikio basi ajaribu. Kwenye maisha haya hakuna muaminifu kihivyo sio wote lakini asilimia chache sana ndio wakweli. Hata Bill Gate alianza na kazi ya kutumwa mpaka akafika alipo. Sasa huyu anapapara ya nini? Au anaogopa kupiga zege?
 
Nimegundua JF watoto mayai wengi wanaochukulia kazi ngumu ni rahisi rahisi, hopeless thinkers, na wenye mzaha ni wengi. Kama una nia ya kumsaidia mtu kuwa straight forward. Dogo amejieleza vema situation yake. Na hata unayetaka kumpa kazi ya zege ungekua na busara na akili kwa kuanza na swali la UNA UTIMAMU WA MWILI KUHIMILI KAZI NGUMU? Si kila mtu anaweza kazi ngumu. Kingine dogo ameonyesha uhitaji wa haraka wa pesa kutokana na mazingira ya deni tarajiwa la kodi inayoelekea kuisha. Ni vema kumwelewa hapo kwanza. Kuna watu wameonyesha kipimo cha maturity kwa michango yao.
 
Miss Natafuta mimi na wewe tumewahi kuwa in good terms ktk mambo mengi humu JF. Nisikilize mimi, huyu kijana ana shida kweli msaidie. Listen to your positive inner vibes. Achana na baadhi ya watu wa JF humu. Vivulana, less experienced na pretenders ni wengi.
 
Kaka Pole sana kwa yanakusibu!
Tafadhali sana kama kweli unashida hiyo unayosema na si utapeli, Tafadhali sana naomba Jina lako kamili,Jina la balozi wako wa nyumba kumi na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa, namba ya simu na anuani ya unapokaa kwa maana ya mtaa na namba ya nyumba na jina la mwenye nyumba yako.Mimi binafsi nitafika au nitatuma intelijensia yangu na nikithibitisha hayo unayosema yana ukweli mimi binafsi ninaweza kukupa nusu ya hiyo fedha unayohitaji kama mkopo uanze biashara yako na unirudishie bila ya riba.Zingatia maelezo husika na Uni PM.Mwenyezi mungu atulinde na Atubariki wote! Amen!
 
Watu kama nyinyi mmebaki wachache sana dunia hii.,..Hongera mkuu kwa moyo huu....kazi kwake mtoa mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…