Nahitaji majibu kwa maswali yafuatayo.

Nahitaji majibu kwa maswali yafuatayo.

Ukitaka kujuwa kuhusu ibada za kale za kontinenti linaloitwa Afrika kwa sasa, soma kuhusu Pyramids za Egypt na Sudan.

Karibu ibadani

*Muhubiri ni Kiranga.
*Mwongozo ni akili.
*Maandiko yatumikayo ni Logical reasoning. hii siijui kwa kiswahili.
 
Kwenye kitabu kimoja cha imani, wanaelezea kundi la watu kadhaa waliokutanika kwa kuwa wanadukuduku la kuona wanamfikishia Mungu maoni yao moja kwa moja, wakaadhimia kujenga mnara utakaofika kwa Mkuu, Mkuu alipoona nia yao ni kubwa kuliko uwezo, AKAWASHUKIA, ila hakuwadhuru sana, aliwatingisha ndimi tu, tofauti na ALIVYO-MSHUKIA nyota ya asubuhi aliponuia kupanda kilima, huyu alimtingisha sana akapata kizunguzungu akaangukia duniani.
Labda Mkuu yupo karibu KUTUSHUKIA maana mara kwa mara tunamtafuta kwa nguvu.

reary ter mi mo.jpg
 
Kama ana nguvu zote, ujuzi wote na uzuri wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao atakuja hitaji kushukia watu, kuwachoma moto watu na kuwabadilishia lugha ili wasielewane?

That's poor design right there, especially for such a master.
 
Nimekutajia mifumo mingine hapo juu, ili kufanya unachotuambia katika mfumo huu wa dini kipate utofauti na mifumo mingine, inabidi unipe tabia au sifa ya dini inayoitofautisha dini na mifumo mingine ya maisha ya mwanadamu.

La sivyo unanipa mwanya wa kukujibu jibu lisilo na maana kwa kufuata definition yako ya "dini mi mfumo wa maisha ya binadamu".

Kwa sababu unanipa mwanya wa kukujibu kwamba dini yangu ni kukusanya hadithi za makatuni (sehemu ya sanaa na utamaduni, mfumo wa maisha ya binadamu).

Au dini yangu ni kutaka maendeleo ya viwanda (uchumi, mfumo wa maisha ya binadamu)

Au dini yangu ni uvuvi wa dagaa (uchumi, mfumo wa maisha ya binadamu)

Hujanipa definition ya dini inayoweza kusaidia kupeleka mjadala mbele.

Labda kwa sababu hata wewe mwenyewe huelewi dini ni nini na hujachukua muda kutaka kujiuliza hilo ama hata ukichukua muda huna uwezo wa kujibu swali hili ama kwa kutokuwa na ustadi au uvivu tu.

Kama unaweza kujibu jibu.

Kama huwezi kuniambia dini ni nini, kwa maana ambayo itakuwa zaidi ya "mfumo wa maisha ya binadamu", jibu ambalo linalundika dini na sanaa, uchumi, siasa, utamaduni etc kiasi cha kulifanya jibu lisiwe na maana, then wewe unayeuliza mimi ni dini gani unaonekana hata huelewi dini ni nini.

Na hivyo jibu lolote utakalopewa litakuchanganya.

Kabla ya kuniuliza mimi ni wa dini gani, niambie kwanza dini ni nini?

Je, ukisema "dini ni mfumo wa maisha ya binadamu", je , binadamu anaweza kuishi bila dini?

Bado nitarudia kukupa jibu hilo hilo Kiranga. Leo ukienda dukani kununua simu mpya ndani ya box utakuta kijitabu kinamaelezo yote jinsi yakutumia hiyo simu, pia ukinunua tv, gari au kitu chochote. Na vile vile hata ukiwa unafanya hizo sanaa ulizo zitaja hapo juu (uvuvi, viwanda n.k) pia ni lazima upate maelekezo jinsi yakutumia. Na sisi kama binadamu Mungu ametuleta hapa duniani (kama unaamini kua na wewe pia umeletwa) ametuletea kitu vha kutuongoza jinsi yakuishi hapa, tuishije, tuanze wapi, tufanye nini, usiku tufanye nini mchana tufanye nini, tuwape nini wazazi, tuwafanyie nini raia na tunaowaongoza, masikini na wagonjwa tuwafanyie nini, wanyama n.k n.k mambo ni mengi sana. Yote hayo tunayapata kwenye kitu kinaitwa dini "dini ni mfumo wa maisha ya mwanadamu"
 
Last edited by a moderator:
"enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, na wapumbavu kuchukia maarifa? Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; tazama, nitawamwagia roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu" (mithali 1:22-23)
 
Kama ana nguvu zote, ujuzi wote na uzuri wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao atakuja hitaji kushukia watu, kuwachoma moto watu na kuwabadilishia lugha ili wasielewane?

That's poor design right there, especially for such a master.

Usiwe unaishi bila kujua ulitokea wapi, uko wapi, unatakiwa ufanye nini, na utaenda wapi hapo baadae...."watu hatari kuliko wote ni wale wajinga" - Henry Ward Beecher
 
Bado nitarudia kukupa jibu hilo hilo Kiranga. Leo ukienda dukani kununua simu mpya ndani ya box utakuta kijitabu kinamaelezo yote jinsi yakutumia hiyo simu, pia ukinunua tv, gari au kitu chochote. Na vile vile hata ukiwa unafanya hizo sanaa ulizo zitaja hapo juu (uvuvi, viwanda n.k) pia ni lazima upate maelekezo jinsi yakutumia. Na sisi kama binadamu Mungu ametuleta hapa duniani (kama unaamini kua na wewe pia umeletwa) ametuletea kitu vha kutuongoza jinsi yakuishi hapa, tuishije, tuanze wapi, tufanye nini, usiku tufanye nini mchana tufanye nini, tuwape nini wazazi, tuwafanyie nini raia na tunaowaongoza, masikini na wagonjwa tuwafanyie nini, wanyama n.k n.k mambo ni mengi sana. Yote hayo tunayapata kwenye kitu kinaitwa dini "dini ni mfumo wa maisha ya mwanadamu"

Hujajibu swali.

Kwa nini mungu muweza yote, mwenye ujuzi na upendo wote aumbe ulimwengu wenye mabaya kibao?
 
Last edited by a moderator:
Usiwe unaishi bila kujua ulitokea wapi, uko wapi, unatakiwa ufanye nini, na utaenda wapi hapo baadae...."watu hatari kuliko wote ni wale wajinga" - Henry Ward Beecher

Mimi naweza kuwa mjinga, kama ndivyo, wewe mbona unashindwa kujibu maswali ya mjinga?

Ama wewe ni mjinga kunizidi mjinga mimi?
 
Hujajibu swali.

Kwa nini mungu muweza yote, mwenye ujuzi na upendo wote aumbe ulimwengu wenye mabaya kibao?

Ndio ni yeye ndie aliefanya hayo na mwisho ametupa AKILI ili tujue kama kuna mazuri na mabaya. Wanaojua hua wanaitwa wenye akili na wasiojua huitwa wajinga
 
Mimi naweza kuwa mjinga, kama ndivyo, wewe mbona unashindwa kujibu maswali ya mjinga?

Ama wewe ni mjinga kunizidi mjinga mimi?

Ndo mana nikakwambia kama umeamua usielewe hata tukiitana watu wote kwenye dunia hii hutaelewa cz umeamua
 
Nitaelewaje wakati maswali yangu hutaki/ huwezi kujibu?

Ni wapi ulipokua na mashaka zaidi kwenye swali lako? Au kua unaamini hakuna Mungu au unataka kujua kwanini Mungu aliumba mabaya au unataka kujua nini?
 
Ulijuwaje kama ni mabaya?

Kitu chochote ambacho hukipendi, ni kibaya kwako.

Maumivu, njaa, vifo etc ni vitu vibaya kwangu.

Kwa nini mungu huyu anayesifika kwa kuwapa watu uwezo wa kuchagua wafanye wanachotaka, mazuri na mabaya, hakunipa uwezo wa kuchagua kama nataka kuzaliwa dunia hii au sitaki?

Na mwishowe, nikazaliwa ulimwengu ambao umejaa mabaya?

Surely huwezi kusema tsunami liliopiga Phillipines au tetemeko la ardhi lililopiga Haiti ni kitu kizuri, na kwamba kama ungekuwa na uwezo wa kuzuia haya usingezuia.

Sasa kwa nini mungu hazuii?

Kwa sababu anataka ila hawezi?

Au kwa sababu anaweza ila hataki?
 
Ni wapi ulipokua na mashaka zaidi kwenye swali lako? Au kua unaamini hakuna Mungu au unataka kujua kwanini Mungu aliumba mabaya au unataka kujua nini?

Nimekuambia unieleze dini ni nini umejiumauma kulundika vitu lukuki vinavyoweza kuitwa "mfumo wa binadamu wa maisha" pamoja, na kusema hiyo ndiyo definition ya dini, inaonekana hata wewe mwenyewe huijui definition ya dini.

Nimekuuliza, kama mungu yupo na ndiye huyo mnayemsema mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye uzuri na rehema zote, kwa nini kaumba ulimwengu huu wenye mabaya mengi sana?

Sijajibiwa.
 
Makampuni ya simu unaingia nayo mkataba.

Wao wanatengeneza simu na huduma zake, wanazitangaza, wewe unaziona, unazichunguza, unajiandikisha, unawekeana nao mkataba fulani wa hiyari.

Hawaji na kuku force tu uwe na simu ya kampuni yao.

Kuna hiyari pale, hujalazimishwa kuwa na simu yao.

Kwenye swali langu la mungu, anayetakiwa kuwa mpenda "free will", hakuna hiyari. Tunajikuta tumezaliwa tu, hakutupa mkataba tukubali au tukatae kuzaliwa, hakufanya advertisement ili tuone maisha yalivyo mazuri na kutupa nafasi ya kuuliza maswali yetu yote kuhusu maisha na kisha tuchague kama tunataka kuzaliwa au hatutaki.

Halafu huwezi kumlinganisha mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye mapenzi yote na makampuni ya simu. Makampuni ya simu yana mipaka ya nini yanaweza kufanya.

Mungu wako anatakiwa asiwe na mipaka hiyo.

Mfano wako uko fyongo.

Tafuta mwingine.

Nikuulize swali, Je una watoto? Kama unao, kwa nini uliruhusu wazaliwe huku ukiwa unatambua kuwa walitakiwa kuona kwanza yanayoendelea hapa duniani. Mfano mwingine, Je wakati wazazi wanakuanzisha shule ulipata nafasi ya kujua uzuri wa kuwa shuleni au kipindi ukiwa mdogo walifanya kukulazimisha?.
 
Hujajibu swali.

Kwa nini mungu muweza yote, mwenye ujuzi na upendo wote aumbe ulimwengu wenye mabaya kibao?

Mungu hakuumba mabaya, ila aliumba binadamu ambaye akaruhusu Ibilisi amtumie katika kuanzisha mabaya katika ulimwengu huu. Na mwanadamu wa kwanza kutumiwa katika kufanikisha mabaya akiwa ni mwanamke ambaye alipokubali kufanya ubaya, shetani akamtumia kama wakala Ku facilitate Mme wake naye afanye ubaya. Tokea hapo, shetani amekuwa akitengeneza mabaya na kutafuta mawakala wa kibinadamu ili kuhakikisha mabaya hayo yanatendwa na binadamu wenzao. Mfano ni suala la ngono ya tofauti na maumbile, fikiria kama wasingetumiwa binadamu, si watu wangeshituka?.
 
Karibu ibadani

*Muhubiri ni Kiranga.
*Mwongozo ni akili.
*Maandiko yatumikayo ni Logical reasoning. hii siijui kwa kiswahili.

Hiyo logical reasoning chanzo chake ni wapi? Je, aliyesababisha mwanadamu awepo duniani, kama asingemfanya mwenye hiyo logical reasoning unadhani Leo hii kungekuwa na kuhoji huko?
 
Nimekuambia unieleze dini ni nini umejiumauma kulundika vitu lukuki vinavyoweza kuitwa "mfumo wa binadamu wa maisha" pamoja, na kusema hiyo ndiyo definition ya dini, inaonekana hata wewe mwenyewe huijui definition ya dini.

Nimekuuliza, kama mungu yupo na ndiye huyo mnayemsema mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye uzuri na rehema zote, kwa nini kaumba ulimwengu huu wenye mabaya mengi sana?

Sijajibiwa.

Dini ni mfumo asiokubali Kiranga ila sisi wengine tunafurahia kuufahamu. Na Kiraka ni mtu asieelewa chochote kuhusu dini. Unaswali lingine?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom