Nahitaji majibu kwa maswali yafuatayo.

kama unataka kujua kweli Mungu yupo au hayupo kufa ndo utapata jibu,then ni ujinga kudai Mungu hayupo,hata sayansi inaeleza wazi kabisa kuwa kila kitu kina origin yake,na kuna force na idea zilizotumika behind yake.Hivi ukiona gari au computer katika akili yako unafkri vilitoka from no where?.Kuhusu dini ni kwamba hata kuhusu kumjua Mungu kumbuka hata yesu aliwatuma wanafunzi wake kwenda kueneza injili duniani kote.
so hata Mungu alijua kuwa kuna watu bado hawajamjua hadi leo,then sisi waagrika tusikatae bila wazungu tusingekuwa hapa,pia huwa najiuliza hivi wasingekuja tungekuwaje ,tulivyo wajinga umasikini wetu tunalaumu wakoloni,sa mbona hawapo na ndo tunazidi kuwa waajabu,imefikia wkati ukiongea na wazee wanakwambia bora wakati wa ukoloni.
 
Jibu lako linajibika vizuri sana, shida ni kwamba mungu ni tofauti na Mungu. Ukiwa specific anahitaji majibu kwa yupi, kati ya mungu ama Mungu itapendeza zaidi.

Nimekwambia pick any spelling you want.

Let's say Mungu.

It sounds like you are stalling now.
 
Utajibiwa kama kitu kidogo hivyo kina chanzo chake basi Mungu ambaye naye ni complex kuliko gari na computer atakuwa na chanzo chake (kaumbwa). :ranger:

Na sijawahi kusikia a reasonable retort to this logical observation.

It's good to know that some people are following the argument, as opposed to just blabbering evangelism.
 
bado somo ni refu Mungu angeamua kila mtu asitende zambi

Kwanza kabisa neno sahihi ni "dhambi" si "zambi". Kama unataka nikuchukulie seriously kama mtu unayeweza kujadili habari za theolojia ya juu, angalau uwe unajua ku spell "dhambi" basi.

I mean I have my inner Marcus Aurelius mode, where I could fray above any sort of schoolmastery pedantics, but don't test me on that.

Swali ambalo hujalijibu ni, kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote aumbe ulimwengu ambao una mabaya?

Mabaya si dhambi tu, hata natural disasters , matetemeko, tsunami, vilema etc ni mabaya.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao haya yanawezekana?

I mean mimi pamoja na kwamba sina uwezo wote na upendo wote lakini naona it is a no brianer, ningekuwa na uwezo wote na ujuzi wote ningewapetesha watu waishi bila mabaya.

I am certainly trying to do that as much as I can kwa ndugu zangu.

Kwa nini mungu huyu ambaye upendo wake ni mkubwa mara infinity kuliko wangu, karuhusu dunia yenye mabaya iwezekanike?

hakuna ambaye angetenda ila alikupa uwezo wa kutambua jema na baya na hivyo akatupa uhuru wa kuchagua wapi pa kwenda kumfata yeye au kwa ibilisi. kwa sisi tulioshika njia yake tuna ushaidi wa kutosha ya kwamba Mungu yupo. sijui nimeeleweka mkuu?

Kwa nini mungu huyu anayesifika sana kwa kupenda kuwapa watu uhuru wa kuchagua hajatuuliza kabla ya kuzaliwa endapo tunataka kuzaliwa au hatutaki?
 
Kiranga una maswali ya msingi sana, umeuliza kwa nini Mungu hakukuuliza kama ulitaka kuzaliwa au la, katika kujibu swali hilo nami nijibu kwa swali hili. Je, makampuni ya simu, kompyuta na bidhaa zingine yanauliza kwanza iwapo kuna uhitaji wa simu au chochote wanachotaka kutengeneza? Ama wanatengeneza kwa faida yao wenyewe? Kwa swali lako la kwa nini Mungu aruhusu mabaya. Kwanza Mungu hakuumba ubaya, ila kwa sababu ya kuruhusu uhuru wa kuchagua nini kila kiumbe wake afanye ndio matokeo ya mabaya kupatikana. Angetaka angetuumba kama maroboti. Hebu fikiria usinheumbwa na uwezo wa kureason, unadhani hata sasa ungekuwa unaandika reason hizo unazotoa? Hapana, ungekuwa unafanya kile tu anataka.
 
Last edited by a moderator:
Hizo disaster unazo zisema pia Kiranga saa zingine zinatokea ili binadamu amkumbuke Mungu mara nyingi binadamu wakati washida ndo anakumbuka uwepo wa watu muhimu maishani mwake.
 
Makampuni ya simu unaingia nayo mkataba.

Wao wanatengeneza simu na huduma zake, wanazitangaza, wewe unaziona, unazichunguza, unajiandikisha, unawekeana nao mkataba fulani wa hiyari.

Hawaji na kuku force tu uwe na simu ya kampuni yao.

Kuna hiyari pale, hujalazimishwa kuwa na simu yao.

Kwenye swali langu la mungu, anayetakiwa kuwa mpenda "free will", hakuna hiyari. Tunajikuta tumezaliwa tu, hakutupa mkataba tukubali au tukatae kuzaliwa, hakufanya advertisement ili tuone maisha yalivyo mazuri na kutupa nafasi ya kuuliza maswali yetu yote kuhusu maisha na kisha tuchague kama tunataka kuzaliwa au hatutaki.

Halafu huwezi kumlinganisha mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye mapenzi yote na makampuni ya simu. Makampuni ya simu yana mipaka ya nini yanaweza kufanya.

Mungu wako anatakiwa asiwe na mipaka hiyo.

Mfano wako uko fyongo.

Tafuta mwingine.
 
Hizo disaster unazo zisema pia Kiranga saa zingine zinatokea ili binadamu amkumbuke Mungu mara nyingi binadamu wakati washida ndo anakumbuka uwepo wa watu muhimu maishani mwake.

Kwa hiyo mungu alishindwa kumkumbusha mwanadamu kwamba yeye yupo bila ya kutumia disaster?

I mean how hard would it be for him to paint the sky with his ten commandments every morning for ten minutes so just we know he is there?

That would have been much better than the millions killed.

Is he such a sado-masochistic prick who enjoy to see million dying for something he could so easily prevent?

Kama ni hivyo huyo mungu ni mbaya kuliko Hitler, Iddi Amin na Stalin combined.

At least they can plead human ignorance.

What's his excuse?
 
tukija kwenye uhalisia tu wamaisha ya kibinadamu ukimtoa Mungu binadamu wakati wa shida ndo atakukumbuka na ndo anakumbuka kumbe kuna kiranga ngoja nimkope hiki mara nimuombe hiki ila akiwa nacho niwa chache sana hukumbuka na hata unaona jinsi wanadamu wakiwa kwenye matatizo km magonjwa sugu wanahangaika huku nakule kutafuta miujiza ili wapone tofaut wakat wa raha tu kiufupi tusingekuwa na majanga duniani watu wasinge hisi uwepo wa Mungu wala kumkumbuka Mungu kwa shukrani.
 
Ivi wewe Kiranga huna dini kabisa? Ni kweli na una uhakika?
 
Last edited by a moderator:
tukija kwenye uhalisia tu wamaisha ya kibinadamu ukimtoa Mungu binadamu wakati wa shida ndo atakukumbuka na ndo anakumbuka kumbe kuna kiranga ngoja nimkope hiki mara nimuombe hiki ila akiwa nacho niwa chache sana hukumbuka na hata unaona jinsi wanadamu wakiwa kwenye matatizo km magonjwa sugu wanahangaika huku nakule kutafuta miujiza ili wapone tofaut wakat wa raha tu kiufupi tusingekuwa na majanga duniani watu wasinge hisi uwepo wa Mungu wala kumkumbuka Mungu kwa shukrani.

Hujajibu swali.

Kama suala ni kumkumbuka mungu tu, mungu kashindwa kuweka bango kila siku asubuhi iwe shurti kwamba kila mtu alione ili amkumbuke yeye? Aandike kwamba mungu nipo nikumbukeni?

Mpaka atumie njia za kuua watu?

Na mungu gani anayehitaji kukumbukwa hivyo?

He sounds like a needy insecure girlfriend. Totally not someone omnipotent, more like impotent.
 
Dini ni mfumo wa maisha ya mwanadamu...ni zaidi ya katiba

Hata utamaduni nao ni mfumo wa maisha ya binadamu, siasa vivyo hivyo, uchumi pia, hujajibu swali vilivyo.

Unaniuliza kama mimi nina dini wakati wewe mwenyewe unashindwa kunieleza dini ni nini?
 
Ukitaka kujuwa kuhusu ibada za kale za kontinenti linaloitwa Afrika kwa sasa, soma kuhusu Pyramids za Egypt na Sudan.
 
Hata utamaduni nao ni mfumo wa maisha ya binadamu, siasa vivyo hivyo, uchumi pia, hujajibu swali vilivyo.

Unaniuliza kama mimi nina dini wakati wewe mwenyewe unashindwa kunieleza dini ni nini?

Jibu ni hilo hilo dini ni mfumo wa maisha wa mwanadamu. Ila hujataka kuelewa...kama hujataka kuelewa hata waje watu wadunia yote hutaelewa coz umeamua usielewe
 
Jibu ni hilo hilo dini ni mfumo wa maisha wa mwanadamu. Ila hujataka kuelewa...kama hujataka kuelewa hata waje watu wadunia yote hutaelewa coz umeamua usielewe

Nimekutajia mifumo mingine hapo juu, ili kufanya unachotuambia katika mfumo huu wa dini kipate utofauti na mifumo mingine, inabidi unipe tabia au sifa ya dini inayoitofautisha dini na mifumo mingine ya maisha ya mwanadamu.

La sivyo unanipa mwanya wa kukujibu jibu lisilo na maana kwa kufuata definition yako ya "dini mi mfumo wa maisha ya binadamu".

Kwa sababu unanipa mwanya wa kukujibu kwamba dini yangu ni kukusanya hadithi za makatuni (sehemu ya sanaa na utamaduni, mfumo wa maisha ya binadamu).

Au dini yangu ni kutaka maendeleo ya viwanda (uchumi, mfumo wa maisha ya binadamu)

Au dini yangu ni uvuvi wa dagaa (uchumi, mfumo wa maisha ya binadamu)

Hujanipa definition ya dini inayoweza kusaidia kupeleka mjadala mbele.

Labda kwa sababu hata wewe mwenyewe huelewi dini ni nini na hujachukua muda kutaka kujiuliza hilo ama hata ukichukua muda huna uwezo wa kujibu swali hili ama kwa kutokuwa na ustadi au uvivu tu.

Kama unaweza kujibu jibu.

Kama huwezi kuniambia dini ni nini, kwa maana ambayo itakuwa zaidi ya "mfumo wa maisha ya binadamu", jibu ambalo linalundika dini na sanaa, uchumi, siasa, utamaduni etc kiasi cha kulifanya jibu lisiwe na maana, then wewe unayeuliza mimi ni dini gani unaonekana hata huelewi dini ni nini.

Na hivyo jibu lolote utakalopewa litakuchanganya.

Kabla ya kuniuliza mimi ni wa dini gani, niambie kwanza dini ni nini?

Je, ukisema "dini ni mfumo wa maisha ya binadamu", je , binadamu anaweza kuishi bila dini?
 
Kwenye kitabu kimoja cha imani, wanaelezea kundi la watu kadhaa waliokutanika kwa kuwa wanadukuduku la kuona wanamfikishia Mungu maoni yao moja kwa moja, wakaadhimia kujenga mnara utakaofika kwa Mkuu, Mkuu alipoona nia yao ni kubwa kuliko uwezo, AKAWASHUKIA, ila hakuwadhuru sana, aliwatingisha ndimi tu, tofauti na ALIVYO-MSHUKIA nyota ya asubuhi aliponuia kupanda kilima, huyu alimtingisha sana akapata kizunguzungu akaangukia duniani.
Labda Mkuu yupo karibu KUTUSHUKIA maana mara kwa mara tunamtafuta kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom