Nahitaji kuwekeza Tsh. Milioni 170

Toa ujinga wako hapa unasema wabongo eti hawajui kutafuta fursa. Umeitembea hii nchi uone wabongo wanavyochakarika! Kutafuta fursa ni Hadi kutoka nje ya nchi kwani. Nchi yetu Ina Kila kitu kwani ni vibaya mtu kukomaa na nchi yake.

Kipindi cha mwendazake kabla hajachafua soko la korosho ungeenda mtwara ukaona wabongo wanavyosambaza mabilioni kwenye korosho!

Usiongee vitu usivuojua.

Mutual funds ni uwekezaji sio biashara. Sio Kila binadamu anaiweza biashara. Sio Kila mtu anaweza compliance za TRA na regulatory bodies zingine za biashara kwanini asiweke Hela yake BOT au UTT AMIS. Kwani ni dhambi.


Huyo alieenda Kongo na Dola Laki 5 ni sawa na Bilion Moja. Hiyo Hela angepelea BOT akanunua BONDS za miaka 25 angekuwa anavuta milion 10+ Kila mwezi.


Na angeweza kutumia BOND certificate kama collateral kuchukulia mkopo bank hadi nusu kwa alichowekeza BOT. Maana yake bank wangeweza kumpa Hadi mkopo wa milion 500.

Hiyo milion 500 ya mkopo angeweza kuwekeza kujenga nyumba kadhaa Dar akapangisha. Kodi ya hizo nyumba ndio zingelipia mkopo. Na kama Kodi ingekuwa ndogo kwenye kulipa mkopo wa bank angetumia sehemu ya ile milion 10 ya riva ya BOT kusaidia kumalizia mkopo.

Mkopo ukiisha. Anakopa Tena bank Kwa kutumia collateral ya hizo nyumba kujengea hizo nyumba. Kumbuka ile Hela ya BOT milion 10 Iko pale pale.


Matajiri wote duniani hutumia Hela za masikini zihazokaa bank kufanyia projects zao. Wewe masikini unapeleka Hela bank MO DEWIJ anaenda kukopa ajengee ma-apartments.


Sio Kila mtu anaweza kuexport au kufanya biashara. Kila mtu afanye jambo Kwa personality yake. Biashara inahitaji roho ngumu , kujikana na kuwa tayari kwa lolote.

Ukiona huna hizo characters tafuta investment basi. Usione wanaoenda kuwekeza hawajielewi.
Mkuu,
Kuna kitu sijaelewa hapa naomba unieleweshe. Umesema aweke pesa kwenye bond ambazo kuna wadau wamesema ni 12.5% kwa mwaka. Sasa ukitumia hiyo bond certificate kuchukulia mkopo kama collateral. Na mikopo ya Bongo ni pasua kichwa, kuna mtu aliniambia ni 20%. Sasa si hatakuwa analamba hasara? Naomba unieleweshe hapa labda kuna kitu sikielewi
 
Za jioni wadau,

Naomba mchango wa mawazo yenu, nikiwa na milioni 170 za kitanzania naweza wekeza wapi pesa hii nikapata rejesho lenye tija?

Kwangu mimi rejesho lenye tija ni angalau milioni 2 kwa mwezi.

Natanguliza shukrani.
Kakodi shamba nafco unenepeshe ngombe baada ya mwaka unitumie laki yangu
 
Kwahyo kwa pesa yako hiyo tunaweza kujenga nyumba mbili kali sana tukauza na kuziuza ndani ya miezi minne tushajenga nyumba mbili na kuziuza tayari(miezi miwili na nusu ujenzi mwezi mmoja na nusu kuuza)
Nyumba moja labda tunajenga kwa milioni 80 yaani kununua kiwanja na kujenga kilakitu tunakuja kuuza milioni 100 kwahyo unafaida ya milioni 20 kwa nyumba moja,
Kwa nyumba mbili unafaida ya milioni 40 kwa mtaji wa milioni 160,
Kumbuka nyumba hizi tumejenga zote na kuuza ndani ya miezi minne tuu,
Kwahyo ndani ya miezi minne tayari unafaida ya milioni 40 inamaana kwa mwezi unakuwa umetengeneza kama milioni 10 kwa mtaji wa milioni 160,
Kwa mwaka kutengeneza faida ya milioni 100 ni kawaida tuu,
Kumbuka mtaji wako unakua kwahyo kwa mwaka unaofata utatengeneza faida ya zaidi ya milioni 200 mwaka unaofata tena ni milioni 400 na kuendelea,
Aliekuwa serious apige simu tufanye kazi
Njoo tufanye kazi Boss +255 714 122 011
Mkuu inaonekana una uzoefu
 
Back
Top Bottom