Nahitaji kutoka Android kwenda kutumia iPhone

cetterhutter

Senior Member
Joined
Sep 5, 2017
Posts
167
Reaction score
75
Naombeni msaada wa maelekezo. Nilikuwa nikitumia simu za Android muda mrefu sasa nimeona nihamie kwenye iPhone. Kutokana na kipato changu nimewaza kununua iPhone 6s Plus kwa hiyo naomba mliowahi na mnaotumia iPhone nipeni maelekezo haya:

(1) Nitajuaje kama simu ni original
(2) Nitakuaje kama simu bado haijafunguliwa
(3) Nitakuaje kama battery ya simu haijachoka

Naomba kuyajua haya kabla sijanunua.
 
Najibu kama ulivouliza maswali.

1. Utajua kama ni original kwa kufungua settings>General>About ukifika hapo utachukua serial number na kuichek kwenye website ya Apple.

2. Utajua kama haijafunguliwa kwa kuichunguza kwa jicho makini, wachache tunaweza.

3. Utafungua settings>battery na kuangalia battery health iko asilimia ngapi.
 
Najibu kama ulivouliza maswali.

1. Utajua kama ni original kwa kufungua settings>General>About ukifika hapo utachukua serial number na kuichek kwenye website ya Apple.

2. Utajua km haijafunguliwa kwa kuichunguza kwa jicho makini, wachache tunaweza.

3. Utafungua settings>battery na kuangalia battery health iko asilimia ngapi.
Asante sana mkuu naomba pia kujua hili, kama nitanunua ya mkononi yaani iliyokuwa inatumiwa na mtu tayari, ni njia gani nitumie kujihakikishia usalama maana watu wengine wanauza simu za wizi.
 
Hapo kwenye asilimia,Hivi asilimia ngapi hinakuwa himechoka?
 
Asante sana mkuu naomba pia kujua hili, kama nitanunua ya mkononi yaani iliyokuwa inatumiwa na mtu tayari, ni njia gani nitumie kujihakikishia usalama maana watu wengine wanauza simu za wizi.
Chukua simu kwenye maduka yanayouza used (utapewa receipt), ama nunua kwa mtu unayemfaham
 
Naombeni msaada wa maelekezo. Nilikuwa nikitumia simu za Android muda mrefu sasa nimeona nihamie kwenye iPhone. Kutokana na kipato changu nimewaza kununua iPhone 6s Plus kwa hiyo naomba mliowahi na mnaotumia iPhone nipeni maelekezo haya:

(1) Nitajuaje kama simu ni original
(2) Nitakuaje kama simu bado haijafunguliwa
(3) Nitakuaje kama battery ya simu haijachoka

Naomba kuyajua haya kabla sijanunua.
Hakuna iPhone fake
iPhone 6s ni simu ya mwaka 2015 kwa hiyo huwezi kupata mpya
 
Back
Top Bottom