Dada huyu fundi tulikuwa tunamwamini sote nyumbani kwakuwa keshatufanyia kazi nyingi tu,ni vile sasa ana wateja wengi sasa ameanza kutojali na anajua hatupo karibu.
Kweli mkuu kweli ni KIPAJI...kwa kuwaamini watu nimepoteza sana na hadi kupoteza marafiki...natamani kuwa na roho mbaya nisikopeshe tena ila ninashindwa
Japo ni kazi na ni vigumu lakini nimeanza kujifunza kusema sina pale nnapoombwa mkopo, watu wanafikiri unapomsaidia kwa kumkopesha una pesa ya ziada kumbe umejibana kwa kujali tatizo lake. Yeye anataka aje akurudishie akipata hela ya ziada ambayo hata hajui ataipata lini na hana uhakika nayo. Mbaya zaidi wewe unashindwa kufanya mambo yako ambayo mdai wako anayafanya na pesa yako hakupi huku msmbo yake yanaendelea.
Ni bora kuvunja urafiki kwa kumwambia mtu sina kuliko hii ya kumpa alaf madai inakua ugomvi. Usamaria kazi sana.
Kuna jamaa ni wa nchi nyingine tunafanya nae kazi, kuna siku nilimwazima pesa yani yeye ndio ananiambia tuandikishane contract anasema ili hata kama akifa kabla ndugu zake hawajachukua mwili wake niwaambie namdai marehem.
Ila kutokana na mazoea yetu ya kuaminiana nikajisikia vibaya kama ataona simwamini
Ha ha haa nimecheka sana, huenda ni kwa vile ameona Mbuni anakufukuza na yuko kwa ukaribu sana akajua hii sio kidume! natania mkuu, unajua hizi ID zetu inabidi kua makini sana kwa sababu hazionyeshi kama mtu ni kijana, mzee, mama, dada, au kaka!