Naomba kujuzwa utaratibu wa kufungua kesi ya madai

RALO

Member
Jan 31, 2012
37
95
Habari ya muda huu wakuu.

Kuna jamaa (Fundi furniture) namdai Sh 700,000/= kama fedha ya advance katika kunitengenezea furniture za nyumbani kwangu ila hakufanya hivyo na tulipelekeshana sana hadi ikabidi tuisitishe ile order na anirudishie fedha yangu yote kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Ni muda sasa umepita (ananipiga sana kalenda) na nimeshampelekea hadi demand notice ya kumtaka anilipe hela yangu mapema pamoja na faini ya Sh 500,000/= kutoka kwa mwanasheria. Nina risiti ya ofisi yake inayoonyesha malipo ya awali niliyoyafanya.

Nahitaji kujua utaratibu wa kufungua kesi ya madai na gharama nitakazotakiwa kujiandaa nazo wakati shauri linaendelea mahakamani.

Natanguliza shukrani zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom