Nahitaji kuoa mapema, naomba ushauri wa kimawazo kwa wakulungwa humu!

Wrevta

JF-Expert Member
Jan 18, 2023
1,440
1,720
Heri ya siku njema hii ya Ijumaa.

Mimi ni kijana nina miaka 24, nipo chuoni mwaka wa mwisho. Nilileta uzi juzi juzi hapa kuomba ushauri wa vitu gani vya kuzingatia kabla umri haujanitupa mkono. Nashukuru nilishauriwa vema na nauchambua bado ushauri niliopata.

Sasa nimempenda binti mmoja wa mwenyeji wa Moshi, jina nalihifadhi, tumependana na amenikubali nilivyo(sina pesa za kutosha za kumgharamia).
Nimerudi tena kwenu wakubwa zangu.

Hili sijamshirikisha yeyote bado, nimeamua kuja JF kwanza nipate ushauri kwa wasomi wa humu kisha ikibidi ndipo niwajulishe wengine.

Lengo langu ni kuwa nilitaka kuoa katika umri huu, nilitaka nifunge naye ndoa kabisa hata kama ni ya watu watatu au wanne. Kwa kuwa ndoa ni taasisi takatifu, na mwanaume ili awe na familia bora ni lazima aoe, pia ili akamilike ni lazima awe na mke yaani afunge ndoa.

Nimelitii agizo hili la muumba wetu na rasmi nimeamua kuja kusikiliza ni nini mtanishauri humu.

NB: Huyu atakuwa ni mke wangu kabisa na atakuwa wa kuanza naye maisha pia.

Karibuni sana!.
 
Back
Top Bottom