Huu ndio muda wa kununua gunia kwa bei rahisi Kama hiyo unayosema sababu wengi ya wakulima wana njaa saa hizi baada ya kutumia hela nyingi kwenye palizi, kuhamisha na kupiga dawa ya panzi (msimu huu maeneo ya morogoro vijijini panzi wamekula sana mpunga).
Haya maelezo ni kwa uzoefu wangu kwenye vitongoji vya morogoro vijijini yaani Wami dakawa, Dutumi na Kisaki.
Changamoto yake ni kwamba utanunua kwa mkopo yaani unampa mtu elfu 30-40 akishavuna anakulipa gunia moja hivyo inabidi uwe na mwenyeji anaye wajua watu. Bila kununua kwa kukopesha ni ngumu kupata gunia kwa bei Hiyo maeneo hayo.
Kwa wale ambao walihifadhi mpunga wao kutoka msimu uliopita gunia ni 100,000-120,000 kwa sasa, otherwise suburi wakati wa kuvuna mwezi wa 6-7 bei huwa 45,000-50,000.