Kweli ni mawazo tu mkuu, hata hivyo naona umezungumzia kitu tofauti kabisa, binafsi wala sijaongelea uchuuzi, mimi ni muumini wa uzalishaji, hivyo unaweza kuona tuko tofauti kidogo kimawazo, kama wewe vitabu vyako vimekufundisha uchuuzi, mimi vya kwangu vimenifundisha uzalishaji. Sina maneno na kusoma, kwani ndiyo hasa ufunguo wa maisha, lakini natofautiana na wewe kuhusu kukimbilia ajira kwa sababu ya security ya "good job", labda hiyo good job inayokuwekea security ya kukopa 50M halafu unanunua "gari la kutembelea" ili na wewe ujione uko daraja la juu kidogo (kwa mkopo!!!!), ni ofauti ya maono tu mkuu, na sijajua ni kwa nini wasomi wengi wabobezi wa mambo ya uchumi hawafanyi vizuri sana wanapojiajiri, na mara wengi wao wanaogopa kujiajiri maka uzeeni utakuta kutwa kuruka na ndege kufukuzia tempo za vipindi!!! Binafsi siamini kama kuna biashara ambayo ni stress free, labda kama mwenye nayo hana mipango mipana, kwangu mimi challenge ni kila siku, nikipata mia nawaza niifanyeje iwe miambili, siyo nikipata mia niumuzike kwa sababu nina uhakika shillingi hamsini imeshalipa!! Ni mawazo yangu hayo mkuu, nadhani ni kwa sababu nimekulia kwenye mazingira hayo, simind sana nikionekana lower class wakati mzunguko wangu wa pesa uko vizuri kuliko hao wanaoonekana barabarani upper au midle class wakati wanalipa mkopo usiozalisha.
Waza nje ya hilo boksi ulilomo!
Poa mkuu endelea kuongeza mia iwe mia mbili, ni vizuri. Lakini ujue kuwa hao hao wasomi unaowabeza unawatamani kwani nao wanaweza kufanya hizo biashara na wakaajiri watu wengi tu. Biashara haiitaji uende shule, kila mtu akiamua anafanya, na ungejua wafanya biashara wengi sana hapa dar pia ni wafanyakazi. Hilo huwez kubisha. Ila kama hujaenda shule kamwe huwez kulingana na mtu mwenye security ya elimu na ajira hapa mjini.
hata sie tuna kampuni zetu na wakati pia tumeajiriwa na hatuna stress zozote na hivo vibiashara vidogo vidogo vya kupata hela ya mafuta na bia hapa mjini tunavipiga na tunawaajiri watu ambao waliona elimu ni time wasting.
Anyway ndo jf tunachat kubadilishana mawazo. So keep with what you see you can do better and make the most out of it.