Nahitaji kujifunza uchawi, wapi ninaweza kutimiza lengo langu?

Nahitaji kujifunza uchawi, wapi ninaweza kutimiza lengo langu?

Uchawi upo, uchawi hautafutwi, ila ushirikina unatafutwa, unaweza kutafuta dawa ya kumzuru mwenzio laini wewe si mchawi, uchawi unarithishwa, au unaweza kuchaguliwa kupewa mkoba na mchawi kama amekupenda kwa mashariti fulani, unaweza kurithishwa uchawi kwa ridhaa yako au kwalazima.

Hakuna kitu kama uchawi mzuri, uchawi ni uchawi tu, huwezi kuwa uchawi just for funny, kwamaana uchawi unamashariti na miiko yake pia unaibada zake za makafara, huwezi kuwa mchawi tu peke yako lazima uwe katika society fulani ya kichawi, kila society ina mfumo wake na mashariti yake.

Katika uchawi kafara ni lazima, na kafara kuu ni damu kwamaana uchawi unaongozwa na nguvu za kiroho na roho hizo chakula chake kikubwa ni damu. Ukiwa katika society za kichawi kisha ukavunja miiko fulani au ukashindwa kutimiza matakwa fulani ya kisociety adhabu yake ni kifo. Uchawi ni ibada kabisa, ibada ya kishetani kuna nyakati fulani katika siku au wiki hukutana kufanya ibada zao, na hii huwa wakati maalum na mahali maalum.

Tofauti ya uganga na uchawi, wachawi wengi wanajificha katika kivuli cha uganga, japokuwa wapo waganga wa kweli wenye taaluma ya miti shamba, hapa nasema taaluma nikimaanisha kurithishwa ujuzi au kusomea sio kuoteshwa, taaluma nyingi za uganga za kuoteshwa ni za kichawi zaidi.

kwa mfano unakwenda kwa mganga wa mitishamba anakupa mzizi wa papai kisha anakwambia chemsha maji yake kishwa unywe saa saba za usiku tu, huku umezima taa kisha usimame kwenye kizingiti cha mlango huku ukielekea upande wa magharibi, huu ni uchawi kamili.

Utoaji wowote wa mitishamba unaoandamana mashariti yasiyo eleweka au yasio na uhusiano na ugonjwa wako au uhusiano na dawa huo ni uchawi ni sawa sawa na kuambiwa chukua maji ya magadi uogee ilikutoa nuksi na mikosi huo ni uchawi, au kuvisha mtoto kamba nyeusi mkononi ili kumkinga na balaa na mikosi huo ni uchawi.

Sikunyingine nitazungumzia uchawi unavyo tumiwa kwenye dini ( Ukristo na uislamu).
Mkuu kuna sehemu umepuyanga sana.
Hebu niambie mgonjwa aliyedhuriwa na mambo ya kichawi anatibiwaje bila kufuata kanuni za kuuzingua uchawi?au ulitaka mgonjwa wa kichawi umpe panadol?
 
Kenya kuna Chuo Kikuu utapata Hadi degree, practice utafanyika nigeria Congo na Tzn
 
Mkuu mifano yako inaonyesha wazi kuwa hauuhitaji uchawi kutokana na wewe kuogopa kutake risk za kichawi, mkuu unachohitaji ni kitu kingine kabisa, nikiwa ninamaanisha unahitaji kuwa "ILLUSIONIST"(not sure if i'm correct with the word) au kwa kiswahili rahisi ni "mwanaVIINI MACHO"
nikipata wasaa ntarudi na madini kazaa

.made in mby city.
au magician-mwanamazingaombwe
 
Ushirikina ni kitu kibaya saaana mbele ya Mungu. Ni kufuru kabisa, acha kabisa hilo wazo we mtu. Tafuta furaha yako kwa njia nyingine iliyo njema.
 
Mimi kuna uchawi ambao nahangaikia kila sku kumasta stail ya moto na maji. Uchawi. Wa kujifunza na kuuingiza mwilini na sio uchawi wa mizizi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom