Binaadam hatu fanani, kila mtu ana vitu vyake avipendavyo. Tangu nikiwa mdogo nimekua nikiusikia habari kuhusu UCHAWI, kitu ambacho tangu wakati huo nimekua nikipenda simulizi zake na naham ya kuujua (kivitendo). Kwamfano hapa mtaani kwetu kulikua na mzee alikua nauwezo wakugeuza majani kua fedha na kuitumia kama kawa.
Inasemekana kunasiku alikua akisafirisha pombe (Gongo) wakamkamata na kumpeleka mahakama ya mwanzo pale Chang'ombe, inasemekana alikana mashtaka nakudai kua police waliamua tu kumdhalilisha kwani yeye hakua amebeba pomba ni maji tu, na kweli badala ya ushahidi kuletwa mbele ikaonekana kweli ni maji sio pombe.
Kiufupi huyu mzee anastori nyingi na ninaimani dunia hii wako wengi tu. Binafs sitaku kuroga mtu bali natamani niwe mtu wa maajabu ikibidi niwe napaa kabisaaa!! Natamani niwe nayayuka, niwezekuingia hata IKULU bila kuonekana.
Napenda niwe kama Ng'wana Mapalala (jina sina uhakika nalo) tatizo sijui wapi pa kuipata Elim hiyo, nishajaribu kuwadodosa dosadosa wazee mbali mbali nikiamini labda watanipa mwanga lakini wapi? Kila mmoja wao anajifanya hajui tu, wakati wapo baadhi yao ni wachawi kweli na kila mtu anawajua hapa mtaani, sasa sijui nakosea njia ya kuwaomba au labda wana sheria zao za kujiunga? Kiufupi ni hayo tu, kama 'unamsaada wakuweza kuniba nitashukuru .