Nahitaji kuanza kutumia pombe

Nahitaji kuanza kutumia pombe

Kama unaweza kutokunywa Pombe achana nayo..

Pombe haina faida yeyote zaidi ya kukuletea majuto baada ya kunywa..
 
Kijana
Sikushauri kunywa pombe na zaidi tafuta starehe nyingine pombe kama huna hela nzuri utaishia kwenye madeni .

Pombe usipoweza kujidhibiti utakuwa na magonjwa ya zinaa kila uchwao .

Pombe ukiendekeza utafeli mipango ya maisha

Mwisho pombe ni uraibu mbaya kuacha sio rahisi .

Siongei nikiwa nyumbani naongea nikiwa bar nakunywa pombe kwa hela yangu ila sitamani uje huku .

Nilianza kunywa pombe nikiwa na miaka 14 , sasa mimi kwa maelezo yako ni baba yako , nilitamani kuacha nikiwa na miaka 29 sijafanikiwa mpaka sasa na uzee huu .

Pombe imenipunguzia heshima kwa jamii kubwa iliyodhani mimi ni mtu wa heshima kwa elimu yangu na kazi yangu .

Pombe imenipunguzia ufanisi kazini , pombe imepelekea sasa nina gonjwa lisilotibika japo lipo katika early stage hivyo naweza kupambana kupona nikiamua .

Pombe imenifanya vitu vingi kuamuliwa na ndugu na mke hata kama kitu naona naweza kuamua mwenyewe lakini bado naamuliwa kwa nguvu .

Ndugu sikushauri kunywa pombe , watakuja vijana sio muda watasema nakunywa matuputapu wambie sijaanza kunywa pombe Tanzania hivyo wakumbushe nje hakuna mataputapu .

Usinywe pombe .
Kwasasa Mbeya pazuri .
Huu ndio ushauri mzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom