Nahitaji Critical Thinking hapa tafadhali

Watu wengi kwa makusudi au kutojua wanadhani aliyekua anashtaki ni mama Kanumba?
 
Mkuu umetumia kigezo gani kuniita mimi kuwa Sina Akili na wewe Kujipambanua kuwa una akili kupitia kwa huyo Classmate wako anayepandishwa Vyeo kupitia sheria za Magereza ambazo hazina ushindani???
Kwa Kifupi walikuwa wanachukuwa option yoa kwenda aidha CCP Moshi au Magereza walio wengi hawakuwa wamepata kuchaguliwa kuendelea aidha na Kidato cha tano kwa hiyo from that angle, Kujiiendeleza siyo kigezo kuwa mbobezi kwenye taalum fulani au Kupandishwa Vyeo hasa hivi vya serikalini havina uhusiano na utendaji bali huwa mara nyingi kwa baadhi ya Sekta na Taasisi huangaliwa na Muda uliokaa Nafasi Fulani.

Kwa ushauri siku Nyingine uwe na heshima na unapoongea jinasibu wewe siyo kupitia uliyombiwa na classmate wako.
 
Reactions: Lee
Kwanza nahitaji kujua kuna ushahidi upi wa waziwazi ambao ulimtia hatiani akafungwa, hata hao mashahidi hakuna aliyeona kama kamuua bila kukusudia. Walikuwepo wawili tu ndani, sijaelewa kwa mantiki ipi akahitimishiwa na kufungwa. Niseme tu hapa kuna namna, pia mawakili wa kumtetea ndiyo wamemtia binti shimoni utetezi wao haukuwa msaada.


Tukirudi kwenye mada bado sikuona umuhimu wa kushikilia bango ili ahukumiwe, huyo mama kaona kafanikiwa ila kamvua nguo marehemu. Kupitia kesi hii tumeweza kujua aliyokuwa akimfanyia huyo binti akilewa, huku si kumuadhiri aliyekufa kujua aliyokuwa akiyafanya. Hivi angekaa kimya na kulimaliza hili suala kiamani, mabaya ya marehemu yangejulikana vipi?
Sitetei upande wa binti tuangalie kiungwana zaidi, suala hili halikuhitaji kisasi cha namna hii. Kamwadhiri mwanae aliyemlilia kwa kusikia kafa, kisa anampenda sana
 
Mama Kanumba yupo Dar zamani sana hata kabla ya Kanumba kuwa maarufu alienda kwenye msiba Bukoba wakati mwanae anafariki usipotoshe

Jiandae Kisaikolojia kwa jibu utakalopewa manake leo Matola springs zake zimekata hivyo anashuka hivyo hivyo kama Scania la Mchanga Wazo Hill Tegeta.
 
1/3 ya two years ni mwaka mmoja na miezi minne ndio muda anaopaswa kutumikia Lulu gerezani kwa sheria za Magereza.
Kweli hesabu ni janga la kitaifa!kwa hiyo theluthi ya miaka miwili ni mwaka na miezi nane?
 
UShauri: Mijadala kama Hii Mtu ukitaka kujadili vizuri kwanza unatakiwa Uepuke hisia, Ukubali kutokubaliana, halafu utumie akili, utumie saikolojia,uvae ubinadamu na pia uelewa wa mambo. ukigusa vipengele hivyo unaweza kujadili vizuri kwa kutumia busara na werevu.
SHIDA : wakija akina Team upupu na Team muwasho mjadala utavurugika. yataanza matusi na kashfa. sisi wengine tulifanikiwa kusoma saikolojia inatusaidia sana wakati mwingi kuweza kukabiliana na hisia na pia kuzielewa hisia.

then kila Mhusika ajaribu kusimama katika nafasi hizi
1. lulu
2. wazazi wa lulu
3. wazazi wa marehemu (jina limenitoka)
4. wanafamilia wa lulu
5. wanafamilia wa marehemu
nimependa nitoe hilo angalizo halafu navuta kiti changu pembeni hapa nakunywa maji kulainisha koo na kuendelea kuwasikiliza. hilo nimetoa kama angalizo tu.
 
hapa fafanua dada.. mimi umeniacha gizani kabisa hata sijui hili jambo likoje...

Kosa moja alilolifanya Lulu ni kuweka ukaribu wa kupitiliza na mama Kanumba baada ya kutoka jela. Baada ya kukwaruzana mama alikuwa na jazba na Jana alifurahia kale katoto kanakomkosea adabu na kaliko sababisha kifo cha mwanae kanaenda jela.
 
hapa fafanua dada.. mimi umeniacha gizani kabisa hata sijui hili jambo likoje...

Kosa moja alilolifanya Lulu ni kuweka ukaribu wa kupitiliza na mama Kanumba baada ya kutoka jela. Baada ya kukwaruzana mama alikuwa na jazba na Jana alifurahia kale katoto kanakomkosea adabu na kaliko sababisha kifo cha mwanae kanaenda jela.
 

Oya acha ' mikwara ' Mbuzi basi sawa? Tuheshimiane kwani humu tunajuana kwa Minyago / Misura yetu? Mara ngapi Mimi kwa mfano tena humu humu huwa napigwa ' Madongo ' ya hatari na sometimes yananiuma lakini Mwanamume nakula tu Kobis / nauchuna na wala silii kama unavyofanya Wewe sasa? Jifunze kuhimili changamoto mbalimbali hasa za Kimtazamo au za maneno ya Kuudhi unayokutana nayo humu. Nadhani humu JF hakuna Member ninayepigwa ' madongo ' kama Mimi GENTAMYCINE lakini hutosikia nalalamika kwa Mtu bali na Mimi sasa hujipanga vizuri na nikirudi nami narudi na ' Kitu ' cha maana kisha tunaheshimiana na maisha yanaenda. Hivi kila Member wa JF akiwa analia lia / ana deka deka kama Wewe hivi hili ' jamvi ' litanoga / litapendeza Kweli? Kuwa kama Mwanaume bhana na tuliomzoea Matola humu wala hatumshangai kwa hayo maneno yako na labda kwa kukushauri tu na Wewe mvizie na mpe ' dongo ' kwa Kujenga hoja nae litamuingia vile vile ila siyo kudekadeka. Acha hizo Mkuu!
 
Reactions: Lee
hahahahahahahaha Umenifurahisha hahahahaha
 
Mimi nimwomba tu rais wetu mteule amkumbuke anatoa msamaha kwa wafungwa
 
Nashukuru kwa kunielewa mkuu na sasa ndio naamini kuwa wewe ni great thinker

Hivi Mkuu umefikiria nini mpaka ukaamua kunipiga hilo dongo? Ebhana dongo limeniingia halafu nimecheka sana. Huwa napenda Members kama Wewe wanaojua Utani na wakinipatia wananipa madongo ya uhakika. Na hii ndiyo raha ya JamiiForums.
 
Kesi za mauaji ni Kesi za Jamhuri dhidi ya mtuhumiwa kwa hiyo mama Kanumba hangeweza kusema amesamehe Kesi iondolewe mahakamani mimi naona kosa la mama huyu ni kushangilia adhabu iliyotolewa kwa Lulu


Hicho tu ndiyo, alipaswa anyamaze kuliko kuonyesha wazi.
 
Maelfu na mamilioni ya watanzania wanafiki na hamnazo ndiyo walioomboleza kifo cha huyo mbakaji. Mungu kamchapa yeye na bongo movie yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…