Kwanini hoja imejengwa na "Angekua na biashara zake angekazana na kesi?" kesi ya mauaji mlalamikaji ni jamhuri, hata kama mama angekaa kimya jamhuri ingeweza kuendelea na kesi bila uwepo wake.
Kwanini mama kafurahi? Ni kwakua kapata closure. Articles nyingi zinazozungumzia abduction cases na murder huonyesha kua familia huridhishwa na hukumu ya kesi kwakua wanapata hitimisho.
Kuna kesi ya mama mmoja, Marekani, kajfungua kichanga akaletewa akaambiwa kimefariki, akataka akaone mara ya mwisho akagomewa.
Siku ya mazishi akapoint kua anahisi jeneza halina kitu ndani, wakampinga, na akawa diagnosed na postnatal distress.
Hiyo ilikua ni miaka ya 70.
Akaishi kwa miongo kumi akifanya kampeni akitaka kaburi lifukuliwe ili ajiridhishe na adhihirishe kua kichanga chake hakikufa siku ile. Akagewa ruhusa 2017 kaburi likafukuliwa ndani ya jeneza zikakutwa nguo bila dalili ya kuonyesha kua ndani kuliwahi kua na kiumbe.
Mama wa watu akasema nilichokua napambana nacho kwa miaka yote ni kupata hitimisho/ closure, haina maana kua mwanangu atarudi.